tuusan
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 17,973
- 20,198
Umeongea kwa weledi sana!!Tuusan, nadhani hapo unawazo, ila ntakukosoa kidogo, hivi vitu vyote unaona vikifanyika Kenya vimewekwa kwenye blueprint ya Vision 2030, na kila moja ina dateline yake. Kuna mipango mahsus ya kuwezesha haya mambo,
1. Ugatuzi - Kwamba nchi ni kubwa hivyo serikali huenda isione ama kujua kila kona, nchi imeganywa kwa gatuzi 47. Gavana anauwezo wa kutatua maswala ya jimbo rahisi kuliko raisi mmoja,
2. CDF Projects, hizi ni projects zina fanywa chini ya mbunge akipewa pesa na Serikali kuu.
Kwa hivi vigezo viwili, Hospitali, zahanati, Shule, Barabara ndogo ndogo, Ujenzi wa polythenique upo kwenye ratiba ya hawa, Kwa sasa, ukipata shule haina viti na madarasa mazuri, hiyo itakuwa taarifa na utasikia mbunge na Gavana wakikemewa,
3.Rural Electrification, Kwenye Blueprint ya Rural electrification by 2018, kila shule itakuwa na stima, kila mtaa wa Kenya hadi Mandera utakuwa na stima, sahi wamefika 85%, ndio maana reli yetu si ya Umeme.
4. Laptop Project- huku mambo ya stima yakiendelea, Laptop project inaendelea, maana ni kwamba ifikapo 2020, kila mwanafunzi darasa la nane atakuwa akifanya mtihani kwenye tarakilishi, 2020 iwe kila mwanafunzi anatumia laptop na amekaa vizuri.
5. Free and easy movement. Every constituency inaunganishwa kwa nyingine kwa barabara nzuri ilibiashara viwe rahisi, kwa sasa kila constituency inamradi wa barabara.
6.Access to water, projects zinafanywa kila upande na wizara ya maji. hii ni kulingana na target kwamba kila Mkenya awe na maji ya mfereji ifikapo 2020.
Mimi nakupa barabara na kadhalika vitu vinavyoonekana, sio kwamba ni hivyo tu vipo
Ukiwa na wakati pitia hii President's Delivery Unit - Home
Raisi wetu yeye ameanza na laptop kwa walimu wa sekondari, Wanakaribia kutoa mikopo kwa vijana katika vijiji vyote nchini mikopo yenye masharti nafuu ambapo watatoa Tsh million 50 kwa kila kijiji
Mbali Ngapi hilo kuhusu umeme mradi wa tatu wa umeme vijijini unaendelea na kwa upande upande mji yote umeme upo kama kawaida na hakuna mgao
Barabara zinapitika zile muhimu kwa asilimia kubwa sana mpaka hivi sasa na zilizobaki wakandarasi wamelipwa nchi nzima kuendelea na ujenzi ili zikamilike kwa wakati
Serikali inapanua viwanja vya ndege vyote muhimu na vile vya mikoani sambamba na kununua ndege
Serikali inatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza katika viwanda na tayari investor zaidi ya 200 wameshaomba na kupata vibali kutoka mataifa mbalimbali
Huduma za afya changamoto za vifaa tiba na dawa pamoja na watumishi ndio imekua changamoto ya muda mrefu sana lakini wanajitahidi kwa kiwango pia japo bado hatujafkia malengo yetu kwa wakat....
Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app