Mimi sijawahi kufika Nairobi,lakini kwa kuuangalia mji wa Dar naona bado haujawa na hadhi ya kusifiwa
Sawa labda hayo ndio yanayotokea huko Nairobi
lakini katika masuala ya mji kama uwe mji kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia kwa wale waliopata kutembelea nchi za wenzetu na kuona miji yao
Mfano Amsterdam,Copenhagen,na miji mingine ya Ulaya utaona kuwa kila katika kla katika jimbo(subburb) kuna sehemu za wazi zaidi ya kumi(10) kwa matumizi tafauti..
Cha kustaajabisha kuwa wakoloni waliyachia ramani nzuri tu ya mji wa Daresalam lakini tulipochukua nchi sisi wenyewe tumeshindwa kuyaendeleza mazuri tuliyoachiwa
Mfano Mkoa wa Temeke kulikuwa na zaidi ya viwanja vya wazi 800,hivi sasa sijui vimebakia vingapi kama sio zero(0),viwanja vyote vya wazi kama havijajengwa vilabu vya pombe basi itakuwa zimejengwa ofisi za chama na serikali...
watawala hawauoni umuhimu wa viwanja vya wazi wanahiyari watoto wacheze vichochoroni au barabaani,halafu watawala hao hao wanalalamika kwanini vipaji vya watoto wetu kimichezo havikui,