Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 9,355
- 15,081
Kutopangilia mji ni kosa la serikali sio mwananchi anaenunua kiwanja. Sheria za mipango miji zipo ila rushwa na uzembe serikalini ndio sababu hazifuatwi. Hata huduma serikali ndio jukwaa lake. Zoezi la kuweka address sasa hivi hadi porini huko mitaa ina majina na namba. Hata unayoiona haina ukienda serikali za mitaa utapiewa jina na namba.
hakuna mahali nimelaumu mwananchi, najua ni kosa la serikali kuruhusu kila mtu kujenga vibanda kiholela kila mahali.
siyo kila mahali ni pakujenga kila kibanda, dar ina square km >1500 ni nyingi sana lkn hakuna hakuna park ya watu kupumzika, viwanja vya michezo vya watoto na vijana vyote vimejengwa vibanda, ukiangalia bird eye view ya dar unaweza kulia, ushawahi kutua dar na ndege halafu ukaangalia chini mabati kutu kila mahali, not good.
ukiingia dar unatokea nje ya nchi kwa hali ya kawaida mtu anakuwa na shauku ya kuona mji lkn kuanzia kibaha kushuka haivutii kabisa, vibanda, gereji bubu kila mahali magenge ya nyanya na mkaa just chaos, ukiangalia mabondeni kimara wamejenga kiholela no planning, mji una watu zaidi ya milioni 5 lkn hakuna highway system ya kuzunguka mji, kuna watu wanatumia masaa 4 kwenda na kurudi kazini kila siku kwenye usafiri tu, not good, dar siyo mji beautiful kabisa yaani, na ukiniuliza mimi dar is a lost cause, labda tujaribu dodoma na miji mingine kwa kujifunza kutokana na makosa tuliofanya …