Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 10,419
- 17,735
Kila kitu kina faida na hasara, horizontal vs vertical city building zote zina faida na hasara
Binafsi napenda Tanzania way of building cities, zinachukua sehemu kubwa kwa sababu kila mtu anataka kujenga nyumba yake, badala ya kubanana kwenye appartments, na watu wakijenga nyumba lazima huduma ziwafuate huko ndio maana unaona Dar 30km from the city bado kuna banks, markets etc though I agree it's costly
Halafu miaka 300 ijayo hizo nyumba hazitakuwepo mkuu, ardhi inatosha sana, lazima baadhi ya nyumba zitakuwa demolished, ardhi haijawahi kuwa kikwazo
Both ways zina faida na hasara, na kwa maoni yangu napenda style yetu ya ujenzi, kuliko ya Kenya ya kukaa kwenye appertments ili kuminimize land usage
Sisi hatuna uhaba wa ardhi
lkn siyo realistic kwamba kila mtu ajenge nyumba yake, kuna nchi kubwa klk tanzania na zina watu wachache klk tz lkn hawachezei ardhi hovyo kama vile tz, tz kila mtu akipata milioni 5 anakwambia najenga nyumba, hiyo ndiyo sababu sehemu kubwa ya wakazi wa dar ni informal settlement, sehemu kubwa hawana maji, hakuna drainage system mvua kidogo mafuriko mji mzima sababu hakuna mifereji au imezibwa na majengo ya watu, watu hawana address kwamba anaishi kwenye mtaa wenye jina na namba ya nyumba n.k. zamani karibia kila nyumba dar ilikuwa na namba na jina la mtaa official kabisa, ulikuwa unaweza kuchukua teksi na kumwambia dereva teksi nakwenda labda temeke mtaa fulani nyumba namba fulani na akakufikisha bila ya shida leo hii huwezi kuchukua teksi ukasema akufikishe labda kibamba au sijui mabibo yoote karibia ni makazi yasiyo rasmi hakuna maji, barabara wala viwanja vya watoto kucheza, hakuna open spaces sasa mji gani huo wenye watu zaidi ya milioni 5 na hakuna parks za wananchi kupumzika? ...