Braza umesoma nadharia. Tunaongelea MGR ya Tanzania siyo any MGR
MGR ya Tanzania katika hali yake ya sasa haiwezi kufanya hilo kwa ufanisi, usalama, na kwa mnyororo wa operesheni wa kila siku.
Mawazo yako yapo kwenye nadharia zaidi, Je, Miundombinu ya MGR Tanzania Iko Tayari? jibu ni HAPANA
| Kipengele | Hali halisi ya MGR Tanzania |
|---|
| Axle Load | Ni ndogo (16–18 tons/axle), ukilinganisha na reli za uwezo mkubwa (SGR 35 t/axle) |
| Urefu wa vituo (loops) | Passing loops nyingi ni fupi – haziwezi kupokea treni ya wagons 100 |
| Braking System | Ni ya zamani (pneumatic) – haifanyi kazi salama kwa treni ndefu sana |
| Mteremko na curves | MGR ina kona nyingi na milima (hasa kati ya Morogoro–Tabora) – inahitaji traction control ya kisasa |
| Haijasanifiwa kwa DPU | Distributed Power Unit (injini mbele, katikati, nyuma) haipo kwenye MGR yetu – hii ni teknolojia muhimu kwa treni ndefu. |
Kwa hivyo, hata kama ki teknolojia inawezekana lakini miundombinu yetu ya sasa haiiungi mkono hilo.
Ndiyo, unaweza kuongeza injini hadi nne. Lakini hilo linafanyika kwa mazingira maalum ya miundombinu iliyosanifiwa kufanya hivyo. MGR ya Tanzania kwa sasa haijajengwa wala kujiandaa kuvuta mabehewa 100 kwa usalama na ufanisi wa kiuchumi.