Tuanzie na Japan population yake ni 128mil haina utofauti sana na Tanzania tukija kwenye suala la population , hapo biashara ya mabasi ni kama haipo kabisa.
Kinachotakiwa ni efficiency tu.
Nani alifikiria dar- Dom ingewez leta maporomoko ya abiria kwa kiwango hiki.
Kwa sasa ni nadra sana kupata ticket ya siku hiyohiyo na kutokana na watu kulala ofisini hata hawajisumbui kuongeza train nyingine.
Ukienda Moro dar kuna wasafiri kibao sana na wengi wanapanda mabasi kwa sababu ya kukosa ticket
Kwahiyo tungesema hakuna abiria kama tungekuwa tunatembeza letsay 20 kwa siku na hakuna abiria wa kujaza.
Tukija kwenye operating cost, trc wenyewe ndo wanaziongeza , hivi Japan kweli kuna wahudumu wa kuuza bites kwa Kila behewa?
Karibia Kila kitu Japan ni automatic ila leo sisi tuna madirisha karibia sita pale Dom wakati tulitakiwa tuwe na mashine za ticket tu ambazo hatulipi mshahara.
Hata ukienda kwenye waendeshaji si ajabu unakuta kwa treni 4 tu za abiria zinazofanya kazi sasa hivi kukawa na madereva 200 . Hiyo efficiency utaitolea wapi na faida itoke wapi?
Kwanini trc isiwatoe wahudumu ibaki na wakaguzi ila iweke mashine za kuuza vitu kwenye Kila steshen kama
Kona na milima option yake ni kuongeza vichwa ili kuweza kufanya distribution ya msukumo
Tunaweza kufanya installation ya hizo dpu kama hazipo ila nachokumbuka miaka ya nyuma pale salanda treni za mizigo zilikuwa zinaweza vutwa na vichwa mpaka 4 sasa utasemaje hazina huo mfumo?
Hivyo vyote ni vitu vinaweza kufanyiwa maboresho ambayo si ya dharama kama sana .
Wewe ndo unalazimisha trc ni sasa hivi tu ndo inavuta mabehewa kidogo, miaka ya 90 ilikuwa Inaweza vuta hata behewa 40 na bado ikifika salanda vikaunganishwa mpaka vichwa vinne kwa ajili ya kupandisha mlima utasemaje haiwezekaniki kuvuta kwa sababu train hazina mfumo wa mawasiliano , ebu tuambie hii video chini iliwezekanaje vikafungwa vichwa viwili bila kuwa na mfumo wa mawasiliano ?
View: https://youtu.be/qgH4Gse_mr8?si=FiUvlsJwKn2lnJwX
Ebu tusaidie kuhesabu idadi ya behewa hapo ziko chini 40?
Kama tumeweza funga mabehewa 40 kwa vichwa viwili Kumbe zamani tulipokuwa tunafunga vichwa vinne tungeweza vuta behewa 80🤣🤣🤣🤣🤣