Chamoto
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 9,883
- 22,305
Unaweza kueleza ilikuwaje kipindi cha Magu hakukuwa na wizi?Duuh hapa kinachopingwa ni kuwa magu kafanya mengi kuliko Marais wote, watu wanashindwa tofautisha vipato vya nchi kipindi kwa vipindi vyote vya urais na kwamba kipindi Cha magu hakukuwa na wizi.
Kuhusu hii ya kikwete kwenye ujenzi wa barabara, iko technical kidogo. Kumbuka waziri aliyesimamia hizo barabara alikuwa huyo huyo Magu. Kwa haki ya marais wote wawili tungelinganisha miradi mingine ya kikwete ambayo haikuwa chini ya wizara ya ujenzi ili tuwe fair kwa wote.Kwamba kikwete alitakiwa akakope 10bil USD ili ajenge reli wakati alipokea nchi ikiwa kwenye GDP ya 18 bil na akaondoka na 49bil USD.
Wengi hatutaki angalia uhalisia hata ukiingia TANROADS Official Website :: Projects
Kikwete awamu ya 1 alikuwa na miradi mingi sana tena ya kufungua nchi kuliko hata huyu magu , ukija barabara tu jk awamu ya kwanza anazaid ya km 3000 huku jpm akiwa Hana hata 2000km mpaka anaingia kaburini.
Kaka, hatukatai anayoyafanya mama Samia, kuendeleza miradi ya awamu ya tano, ambaye yeye mwenyewe alihusika. Tofauti ya Magu na wengine ni kuwa miradi yake ilikuwa ni a game changer, yaani alifanya a paradigm shift kwa watanzania na Afrika kwa ujumla, alionesha tunaweza. Yale mawazo ya kuwa Afrika haki yetu ni treni za gari moshi aliondoa, wakubwa walitaka tuifufue MGR tuu. Eti, tukitaka kupanda mchongoko twende kwao, Kha!Kila rais ana jambo lake alilolifanya hata Samia Kuna mengi anayafanya ila kwa sababu watanzania Huwa tunapenda kuwa na yule kiongozi anayeropoka ndo maana tunaona magu alifanya mengi sana
Ndiyo maana hadi watu wa mataifa wakaja na slogan za "magufuli effect" na "what would Magufuli do". Nitajie kiongozi mwingine wa Africa aliyepewa hash tags kama hizo?