Kwa hivo unadhani Nairobi hamna nyumba za compound ama Nini? Hujui Nairobi utachagua unapotaka kuishi? Halafu pia usidhani apartment za kuuza zinazojengwa Nairobi ni vi-apartment ovyo ukigombana na bibi neighbor anaskia. Hizi ni apartment za maana zenye sound proofing ndio maana ni Bei ghali kuliko kujenga nyumba yako mansion mitaa kama ya Syokimau.
View: https://www.youtube.com/watch?v=T633izGubto&pp=ygUXZ3RjIHJlc2lkZW5jZSBwZW50aG91c2U%3D
Kumbuka pia mitaa yetu ya kujenga nyumba za chini imepangika na ina Barabara za lami, sio kama hapo kwenu watu wanajenga kiholela.
Linganisha Hii mitaa. Hapa ni Kahawa Sukari. Huu ni mtaa nje ya Nairobi ambao unanunua shamba lako unajijengea. Tazama ulivyopangika. 100% Barabara ni lami.
View attachment 3063440
Huu hapa ni Syokimau, pia nje ya Nairobi. Unanunua shamba lako unajijengea nyumba yako jinsi unavyotaka. Tazama ulivyopangika. Hapa barabara 60% ni lami, the other 40% ziko mbioni kupigwa lami.
View attachment 3063441
Haya,linganisha ni hii Mbweni yenu ambayo kila siku mnajichocha nayo humu. Tazama ilivyo disorganized. Ukitoa Main road, hamna barabara nyingine yoyote yenye lami.
View attachment 3063442
Mwengine hapa Mbezi. Huu mtaa nimeuskia sana hata kabla nikanyage Dar niliskia Wabongo wengi sana wakiongelea jinsi ulivyo mtaa wa kitajiri. Sasa naulinganisha ni mitaa ya Nairobi ya kawaida kama Syokimau hata haufikii kwa kupangika wala infrastructure.
View attachment 3063443
Ndio maana mimi hucheka sana nikiwaskia mkiongea eti ooh Dar tunajijengea nyinyi mnaishi kwa apartments. Hapa Nairobi kila kitu kipo.
Ukitaka kununua shamba ujenge mansion utapata, ukitaka kununua mansion kwenye gated community utapata, ukitaka kupanga mansion utapata, ukitaka kununua apartment utapata, ukitaka kupanga apartment utapata. Kitakachoongea ni preference yako na mfuko wako.