Kuna njia nyingi za kuongeza pato la serikali tofauti na kodi.
Huyu bimkubwa kwishafeli.
Umeona ee, yaani mimi kila sehemu naona pesa.
1. TTCL pesa zipo nyingi sana sana tena nyingiiii.
Home Internet, TTCL wana miundombinu nchi nzima hadi ndani ndani ambao wengine hawajafika, wakiamua kuunga watu mbona pesa ipo nyingi tu. Kila mwezi serikali ni kujikusanyia pesa.
Kujenga Recreation Areas za kisasa mjini, Parks, rest area za jiji, pesa hiyo yaani hata mia tano tano mbona watapata sana plus litakua jiji la kitalii.
2. BRT ina pesa waweke Luti ya Morroco Mbagala waone, Gongo La Mboto Morroco, Kivukoni Mbagala, Kimara Mbagala. Iwe na usimamizi wa hali yajuu pesa ipo yote.
3. Bandari ina pesa ila hawaoni wakagawa. Wanadhani Magu mjinga kila siku na ruti zake bandarini, hiyo pesa mwekezaji anayochukua Imagine ndio wanachukua?
4. POSTA
Siku hizi parcels na cargos ni nyingi posta wana magari.na vitengea kazi vingi plus office kila sehemu ya nchi wanaweza kuwa the most reliable wakiwa serious na serikali itapata pesa nyingi, wafanye partnership na Air Tanzania Cargo, alafu waende kufungua office China, kingine wawe wanatengeneza packaging za parcel, storage facility.
5. MSD ina pesa naweza sema SADC, EAC MSD ni ya kipekee so ilitakiwa serikali iipe nguvu via Air Tanzania Cargo, POSTA SERVICES alafu tukaingie mkataba na nchi zingine kusambaza na kuwanunulia Dawa, Kustore dawa zao (Sio nchi zote umeme ni stable hapa Africa kwa kuwa tuna umemem wa kumwaga ni muda wa kuwaza kila njia Storage facility ya Dawa ingefaa kwa MSD)
7. TANESCO, mita za kujitegemea kila mtu hasa kwa wapangaji, mbona pesa itaongezeka kwa kua tayari nyumba ishaungwa so ukiweka submita zenye uhakika zaidi, nyumba moja itakuingizia pesa nyingi instead ya kuwaza huu upumbavu wa kukata 2000.
8. CNG matumizi ya vyombo vya moto hata ikiwa changa wanawaza tozo (WTF) badala ya kufanya hivi wajaribu kuweka ruzuki ili vifaa vinunuliwe vingi maana CNG ni yetu hivyo serikali itapata pesa nyingi ikinunuliwa na watu wengi like UMEME na pia itapunguza purchase ya petroleum ambayo itaokoa Dola zinazopotea kufanya shilling iporomoke.
9. Agriculture badala ya kuuza Mahindi kila siku why wasiuze unga na other goods na sio malighafi. Hivyo zao moja pesa maradufu.
10. Ondoa Matozo ya kiwaki kwenye mafuta ili pesa inayotumika sehemu moja ipungue ili volume ya manunuzi (Purchasing Power iwe kubwa sehemu nyingine) ili kodi pia itoke kwingine.
11. Tourism - waache kukalili maisha kila siku ZNZ, SERENGETI, NGOROGORO Tanzania imejaa kila mbunga, Rwanda mbunga yao inayowalipa ni ya Masokwe (Gorilla) ambayo tunayo Gombe na Mahare. Mwanza beaches ziwe za kisasa, waone kama pesa haitakuwepo. Kurundikana sehemu moja kila siku haisaidii.
12. TBS waweke watu wa kueleweka ili bidhaa za Tanzania Quality iwe inacompete na huko majuu na waangalie namna tunaweza pata chata za CE, alafu wapunguze VAT kwa bidhaa inayozalishwa ndani na wazuie bidhaa hiyo hiyo kuagizwa nje, hivyo volume ya mauzo ya viwanda iwe kubwa waanze kupokea pesa ya uhakika.
13. Madini - wafate ile plan za Magufuli zilikua very helpful, sio ukisifiwa unaona eeh!.
Yote yanahitaji kutocheka na mtu yoyote anayeharibu pesa ya serikali anatakiwa asichekewe ndio pesa zote wataziona.
Kila namba hapo nina mengi ya kuelezea ila acha tu iwe hivi, hii nchi ina option nyingi za pesa kila sekta asee.