.
Ni hivi; neno 'koko' kwa kiswahili chetu ni kitu cha uvuguvugu (hakieleweki kipo upande gani), mfano 'mbwa koko' ni mbwa mpole asiyebweka au yule ambaye hawezi kung'ata. Sasa 'wazungu koko' ni wale waafrika ambao wanajifanya wazungu kwa kuibia ibia vitabia viwili vitatu vya kizungu lakini siyo wazungu halisi.
.
Namanga ni mpaka wa Tanzania na kenya kwahiyo ukivuka to boda ya namanga kuja Tanzania, uzungu unauachia hapo hapo.
.
Haya maneno ni ya kiutamaduni na kihistoria zaidi. Miaka ya nyuma hapo Dar, kulikuwa na misemo kama;
"unashanga shangaa nini, kashangae feri meli kuzama, shilingi kuelea".
Mshangao huu ulitokana na kuona meli ambayo ni kubwa na nzito, kuelea, wakati shilingi (coin) kuzama (law of flotation).
Watu wengi wanaotembelea maeneo ya baharini (feri) kupunga upepo, huonekana kana kwamba wemekumbwa na bumbuwazi (being stunned) kwa jinsi bahari ilivyo kubwa. So goes "unashanga shangaa nini".
Neno feri limetokana na neno 'ferry' yaani kivuko. kihistoria, wakazi wa Dar ili kwenda ng'ambo ya pili ya Dar (kigamboni) ilibidi watumie, 'a ferry' kuvuka. Waswahili tukapaita pale kwenye kivuko, kivukoni au feri. Utamaduni huu wa kubatiza maneno ya kiingereza upo sehemu nyingi mfano carrier corp (kariakoo) na Michael chain (mikocheni) n.k.
Kwahiyo nilitumia hayo maneno kwasababu hao wakinamama kwenye picha walikuwa wanatoka feri kununua samaki huku wakibeba ndoo za samaki kichwani (utamaduni huo).
.
Unaweza kufikiri hawa wamama hawajastaarabika lakini wanajua ku-apply physics kuliko unavyodhani.
Hizo ndoo unazoziona zimekuwa balanced vizuri kabisa, wenyewe tunasema "all forces are concurrent". Yaani hapo ndoo imeganda kichwani vizuri kabisa ikiwa imekaa kwenye khanga (as a damping mechanism) with 'resultant force' approaching to zero. Any excessive force acted at any angle will be corrected by the 'superior brain cells' of these women. Concept hiyo hiyo ya ku balance ndoo ndiyo inayotumika kutunda 'suspension bridge' (kama Golden bridge ya San Fransisco) au ku fly an airplane.