Wewe, huu mkataba uklivujishwa na haukuletwa na wabunge kama unavyodai hapa. Mikataba kibao imesainiwa upi umejadiliwa? Huko Dubai ilisainiwa mikataba kama 14, mingine iko wapi isijadiliwe?
Umeuona mkataba wa $40B LNG project? wewe vipi??
Mpaka ivuje ndio utaona wabunge wakihaha kuinusuru serikali.
Mkuu, ninarudia tena, jambo lolote ambalo halipo katika ratiba ya bunge, haliwezi kuzungumzwa na bunge hadi mbunge atoe hoja rasmi kusimamisha bunge, na ikitokea hoja ya kusimamisha bunge Ili kujadili hoja ya huyo mbunge, hilo linakua ni jambo kubwa, lazima nchi nzima tutasikia na kujua.
Mkuu, katika bunge hili linaloendelea, je Kuna siku ulisikia kuna hoja yoyote ya dharura ya kusimamisha bunge Ili kujadili huo mkataba?, jibu ni hapana. Hilo swala la mkataba lilikuwepo katika ratiba za bunge na ndio sababu lilizungumzwa bila hoja ya dharura, hiyo maana yake ni kwamba, wajumbe walipata dondoo zote za yatakayozungumzwa miezi kadhaa nyuma kabla ya kwenda Dodoma.
Kuhusu mikataba mingine kutozungumzwa bungeni, Mkuu, kazi ya serikali chini ya rais aliyechaguliwa na sisi wote, ni kuingia mikataba kwa niaba yetu Ili sisi tuendelee na kazi zingine, yeye na wasaidizi wake hawaendi shamba Wala kufanya kazi zingine, kazi zao wao ni hizo za kuingia mikataba kwa niaba yetu tukiamini kwamba wanafanya hivyo kwa mujibu wa maslahi, taratibu na mamlaka waliyokabidhiwa kikatiba ya nchi yetu.
Bunge ndilo lenye jukumu la kuisimamia serikali endapo itakengeuka jinsi ya kuingia mikataba hiyo, serikali inapaswa kuomba kibali toka bungeni pale inapotaka kuingia mikataba mikubwa Kama huu wa DPW, lakini mikataba mengine mingi, serikali haiwajibiki kulishauri bunge, hiyo ipo chini ya uwezo wao, ni sehemu ya kazi zao.
Kwa mfano SSH alipokwenda ufaransa, aliingia mkataba na kampuni Ili kuja kukarabati uwanja wa ndege Dar "terminal ll", bila hata kushauri bunge, au mikataba ya Air France kuja Dar, au mikataba ya Ujenzi wa Meli na kampuni la Korea.