Wawekewe mazingira mazuri ya uwekezaji itakuwa labda kuna shida somewhere kwenye government
Waongoze kasi za viwanda sema serikali inazingua sana
Viwanda viwe vingi mbalimbali wasiishie hicho cha pombe ili wakulima wauze kwa sana malighafi ndani na nje hapo tunapunguza ku import . Hizi nido, blueband , nakadhalika .
Hapo inakuwa game over
Umeme unazingua.bei ya umeme ni kubwa sana kwa Nchi kama yetu. China unapata unit moja kwa US cents 8.1 Ambayo ni kama shilingi 190 za kitanzania. Lakini hapa kwetu unauziwa unit shilingi 350 ukiongeza na matozo basi unalipia unit sh 370.
kwa bei hii ya umeme,huwezi piga hatua kubwa kiviwanda. Viwanda pekee vinavyoweza shamiri bongo ni light industries kama utengenezaji magodoro,vinywaji,sabuni,n.k, viwanda ambavyo havina matumizi makubwa ya umeme.
Lakini ili uibadilishe TZ kiviwanda na uchumi,inabidi ujenge viwanda vyenye kutumia malighafi zetu za ndani.Na hapa ndio suala la umeme rahisi linapohitajika. Tukiweza kua na umeme huo rahisi, viwanda kama vya chuma vitashamiri sana,na tunacho chuma ghafi. Viwanda vya bid has za shaba, viwanda vya ceramic, vioo, vitakuwa sana kwakua madini kama feldspar,dolomites,n.k. tunayo ya kutosha. Hata viwanda vya cement vitaongezeka kwakua tuna gypsum na chokaa ya kutosha.Hayo ndio mapinduzi.
Lakin imekua aibu tunaagiza hadi majembe toka China kisa tuu umeme wetu ni ghali na wakati tumebarikiwa mito mingi ya kuzalisha umeme bei nafuu. Cha ajabu, eti wanataka kujenga umeme wa jua na wind power ambao ni ghali sana
Serikali kama wameshindwa kushusha gharama za umeme Nchi nzima pengine kwasababu ya maslahi ya viongozi wachache,basi waache baadhi ya mikoa ijengewe umeme maalum kwaajili ya viwanda.Mfano, mkoa kama morogoro wangepewa umeme wa maji kwa bei nafuu ili viwanda vyenye mahitaji makubwa ya umeme vingejengwa huko. Mikoa ya ruvuma,njombe, rukwa,na mbeya nao wangejengewa vinu cha umeme wa makaa kila mkoa kwa kua wana makaa mengi ya mawe,Na viwanda vyenye kuhitaji umeme mwingi vingejengwa huko kwani malighafi za chuma,gypsum, shaba, zinc ziko Tele huko.