Hapa Tony umeongea bila ushabiki bali kwa Facts.
Kikwete aliwahi kuulizwa huko nje kwanini nchi yako ni masikini pamoja na utajiri wa nchi yako ulionao akajibu sijui, aibu hii sana.
Hii nchi ilikuwa na viongozi wazembe, wasio na maono ya uongozi hasa mambo ya uchumi, rushwa, ufisadi, wizi, incompetent leaders, kuhodhi vyeo vingi kwa mtu mmoja,usimamizi mbovu wa rasilimali, mikataba mibovu, sera mbovu ya kuitangaza ikiwemo na kutokutangaza vivutio vya utalii, ukwepaji kodi, utoroshaji wa madini na mali asili nyingine.
Sasa alivyokuja Magufuli ndio akawazindua usingizini, sasa hivi unaona kama ndio wamekurupuka usingizini wanahaha kutaka kufukia mashimo ya huko nyuma.
Kwa ardhi tuliyo nayo ingepeswa tuilishe Kenya mpaka mshindwe wenyewe ndipo tufikirie kutafuta masoko mengine, lakini bado hatujawatosheleza maana yake hatuzalishi vya kutosha.
CCM kwa kuandaa mipango wako vizuri sana ila kinachowaangusha ni utekelezaji wake, kama wakiamua kuwabana viongozi angalau wakatekeleza Ilani yao kwa robo tatu tu nchi itapiga hatua sana.
Ulivyowaza wewe mimi huwaza kila siku mpaka kichwa kinauma, kuna Viongozi hawana muda huo as long as they get paid each month what else to think about others.