Tatizo hujui unalozungumza, unarukaruka bila kujua nini unazungumza
1)Kuhusu Dangotte kuajiri raia wa Nigeria kule Mtwara, kwani hao wanigeria ni raia wa Tanzania?, Nimesema mtu yeyote yupo huru kumuajiri raia yeyote wa Tanzania anayempenda, hakuna Sheria ya nchi inayomtaka kuajiri watu, yeye anachojali ni mafanikio ya biashara yake, hata akiamua kuajiri ukoo wake pekee, hiyo ni haki yake.
Kama Dangotte akifanikiwa kuhamisha ndugu zake na kuwapa urai wa Tanzania na kwa idadi Yao inatosha wao pekee kufanya kazi anayo haki ya kuajiri wao pekee tu, hakuna Sheria yoyote inayomzuia. Habari ya kwamba kutoa fursa sawa kwa ajira, Hilo ni jukumu la serikali sio la mtu binafsi, mtu binafsi anachoangalia ni ufanisi wa kazi na familia yake.
Kuhusu wajapani kwamba huko 99% ni Wajapan na wakati hapa Tanzania sio hivyo, hapa ndio hasa wivu na hasira zako kwa wahindi unapojitokeza, kote huko ulikua unapita tu, ukweli ni kwamba una chuki Sana kwa watanzania wenya asili ya India na Arabuni kwasababu ya mafanikio Yao, hii ndio sababu nilidhani wewe ni Mkenya.
Hawa ni watanzania kama watanzania wengine. Wewe ni kaburu mweusi, unajihisi wewe ni mtanzania zaidi ya wengine(mzawa),punguza wivu na chuki zako. Hizo ni biashara zao Kama zilivyo biashara zetu nyingi tu ambazo tunaziendesha na tumeajiri ndugu na jamaa zetu, tofauti ni kwamba hizo zao zimekua kubwa kutokana na juhudi na bidii zao, ila lengo ni kusaidia familia zetu, Sheria za ajira zinazotawala biashara ya duka, daladala au kiosk, ni ileile inayotawala makampuni ya Azam.
Mkuu, tujitahidi na sisi kuwekeza ili watoto wetu wapate uhakika wa ajira, hii tabia ya kulalamika na kuwachukia watu wa jamii Fulani kwasababu hawatoi fursa kwa wengine katika biashara zao binafsi ni tabia ya kishamba na kichawi, achana nayo.
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app