Mkuu, wafanyakazi serikalini hawazidi 1M, wakulima ni zaidi ya 30M hapa Tanzania, mbona sisikii ukizungunzia maslahi ya wakulima ambao ni zaidi ya 70% ya watanzania badala yake unazungumzia maslahi ya watu 1M ambao ni chini ya 2% ya watanzania wote?, hivi unadhani nchi hii inajengwa na wafanyakazi wa serikalini pekee?.
Mkuu, sisi wote tulishawahi kuitumikia serikali katika nyadhifa tofauti, Kuna tafiti zilionyesha kwamba, wafanyakazi wengi serikali wanapaswa kulipwa 30% ya kile wanacholipwa kwasababu wengi wanaofanya kazi, wanazalisha 30% ya kile wanachopaswa kuzalisha.
Tafiti hizo zilizofanywa katika utawala wa Kikwete zilisema kwamba, utendaji wa kazi serikalini hauwezi kuongezeka kwa kuongeza mapato, Bali kwa kuweka usimamizi mzuri kwasababu hakuna utamaduni wa kupenda kufanya kazi kwa kujituma.
Mkuu, mishahara imekua ikiongezwa kila baada ya vipindi kadhaa toka enzi za Nyerere, lakini ufanisi maofisini haukuwahi kuongezeka *accordingly". Lakini pale ambapo usimamizi umeongezeka, basi ufanisi umeongezeka kwa Kasi Sana bila hata kuongeza mishahara, kumbuka uongozi wa Augustino Mrema, Keenja alipokabidhiwa Jiji la Dar es Salaam, na Utawala wa Magufuli, hiyo ni baadhi tu ya mifano.
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app