Naona kama unachanganya mambo mawili hapa. Kuna ile kutaka kuwa always right na kuna ile kukataza mwenzako kuongea jinsi anavyotaka. Kupenda kuwa always right sio tatizo kubwa kwa sababu Wakenya wengi na Watanzania wengi wanaipenda nchi zao kwa hivyo wana haki ya kutetea nchi zao. Ila tatizo la kukandamiza haki ya mwenzako kuzungumza au kutoa maoni yake ndio tatizo hapa mkuu kwa sababu hio ni kukandamiza freedom of speech na freedom of association. Yaani Mkenya au Mtanzania ana haki ya kuongea na kutangamana na mtu yeyote yule bila haki yake kukandamizwa.
Hapana Tony, haya Mambo yanahusiana kwa karibu na kwa ujumla ni kitu kimoja. Wakenya mnahisi ninyi mpo sahihi kwa Kila jambo, katika kusema na kutenda.
Kawaida mtu yeyote anayejiona kwamba wakati wote yeye yupo sahihi, basi hataki kuona watu wengine wanaofanya tofauti na vile anavyopenda au anavyotaka yeye.
Kenya Kama nchi au Kama wakenya mnalo Hilo tatizo Sana, na ndio sababu Kenya inakwaruzana na majirani wake wote, mara utasikia Kenya na Uganda wanagombania Mambo ya maziwa ya lato, mara sukari, mara ushuru wa magari, ukija Kenya na Tanzania ndio kabisaa migogoro haikatiki.
Tanzania tukichoma vifaranga ni makosa, lakini Kenya mkizuia mahindi yetu kwa kisingizio cha "aflotoxin" hiyo ni sawa.
Anachokifanya "Nairobiwalker" hapa kukuchagulia nini la kusema, ndicho mlichomfanyia
Geza Ulole huko Skyscraper city mwisho alizuiliwa na mkampiga ban. Jambo la kushangaza, wewe unasifia kwamba Geza ni miongoni mwa watanzania hapa JF ambaye yupo independent, lakini huko Skyscraper city, hiyo indepence yake hamuhitaki[emoji23]
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app