Mkuu tofautisha kati ya inflation rate ya chini ya 2% hadi 8% ambayo wachumi wanaikubali na kuamini kwamba ni nzuri kwa afya ya uchumi na inflation rate kubwa ya zaidi ya 20% ambayo wachumi wanaamini ni mbaya kwa afya ya uchumi. Hii ya Turkey ya 73% ni mbaya na ina madhara mabaya sana hata kwa matajiri kwa sababu utajiri unapungua kwa kasi kwa sababu ya high inflation. Kwa mfano ksh 1,000,000 katika mwaka wa 2001 inaweza ikawa value yake ni ksh 30,000 mwaka wa 2022 kwa sababu ya inflation. Sasa Zimbabwe wakati walipata inflation kubwa unajua kuna watu wengi walikuwa millionaires lakini ndani ya miezi michache wakapoteza umillionaire wao kwa sababu ya bei ya bidhaa kupanda kishenzi kiasi cha kwamba milioni moja ya zimbabwe ilikuwa haina thamani tena, haingeweza kununua hata mkate dukani. Inflation ya juu inawaumiza hata matajiri.
Inflation is effectively the reverse of compound interest. Take a closer look at how inflation destroys your wealth every year and effect of inflation on wealth.
www.valueresearchonline.com
Hayo nayafahamu na mimi nimesoma uchumi vilevile.., madhara yatakuwepo kwenye biashara/assets ambazo zina nature ya savings .
Hoja yangu ni kwamba kwani ukitrade kwenye Biashara zinazohusisha transactions za papo kwa papo hiyo hasara itatoka wapi?
Erdogan pamoja na kwamba anaamini kwenye mambo ya Imani ila ni kwamba ameamua kuweka uchumi kwenye mentality hiyo na it works so far hakuna hasara Nchi imepata..
Nimefuatilia trend za inflation rate kwenye Nchi nyingi kama Ghana,Nigeria,Sudan,Zimbabwe na hii ya Turkey,,nilichobaini ni kwamba kile kinaelezwa kwenye literature za Economics na kinachotokea kwenye uhalisia ni kama vile kuna shida kwenye hizo theories,kuna haja ya study zaidi..
My conclusion ni kwamba,naona inflation rate ina effects zaidi kwenye Nchi ambazo ziko assumed kwamba their economies are at fully employment level na pia zile ziko kwenye below 2% annul population growth..
Lakini kwenye Nchi zenye zina ukuaji wa zaidi ya 2% ya population growth inflation haina shida kwa sababu ya consumer behavior..
Pia Nchi ambazo bado zinaendelea na hazijafikia full employment ya resources sioni effects za inflation hata ikiwa higher than 10%..
Mwisho inflation ambayo inasababishwa na shortage ndio yenye athari mbaya kwenye uchumi wa Nchi..