Hata ukiwaonyesha certificate yako, blank out your name. Cover your name. Hawa watu wanadhani Wakenya hawajasoma. Hawajui kwamba the biggest problem in Kenya right now is graduates lacking employment. Basically we have more educated people than even the local job market can handle. Ndio maana unaona Wakenya wengi waliosoma wanaenda majuu kutafuta greener pastures.
Tony254, nchi zote za Africa na nchi za Dunia ya tatu zinasumbuliwa na matatizo yafuatayo
1)High unemployment rate
2)Upungufu wa wataalamu wa sekta mbalimbali( Lack of skilled labour)
3)Brain drain
Hivi unaweza kuelezea vipi hayo matatizo yanaweza kutokea kwa wakati mmoja?,
I)Inawezekanaje katika nchi/bara ambalo Kuna tatizo kubwa la Ukosefu wa ajira(high unemployment rate), lakini ndio nchi/bara hilohilo ndio kwenye upungufu mkubwa wa (skilled labour), na ndio bara linaongoza kwa tatizo la (Brain drain).
Sio kweli kwamba Kenya/Afrika Kuna wasomi wengi zaidi hivyo ajira ni chache, ukweli ni kinyume chake, kwamba Kenya/Africa Kuna tatizo la kutengeneza ajira za kuweza kuajiri hao wasomi wachache.
Japan Kuna vyuo vikuu vingi kuliko vyuo vikuu vilivyopo Africa nzima, 80% ya wajapan wamefika Universities, hapo Kenya wasomi waliofika Universities hawafiki 3% ya wakenya wote, lakini Kati yao hao 3% wanaopata ajira hawazidi 20%, wakati Japan yenye universities nyingi kuliko idadi ya universities zote za Afrika nzima, na 80% ya Wajapan wamefika Universities Kati yao 90% wanapata ajira.
Sijawahi kusikia Wajapan wakilalamika kwamba Wana wasomi wengi kuliko ajira, lakini Kenya ambayo Universities hazizidi 100, wasomi hawazidi 3% ya wakenya wote, eti mnasema wasomi ni tatizo kwahiyo ni Bora watafute kazi nje ya nchi. Hivi mtu Kama wewe ukiwa kiongozi utaweza kweli kulisaidia bara la Afrika?
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app