Kwahiyo unataka kusema kwamba Ukosefu wa (Maintainance and Repair) ya miaka yote huko nyuma ghafla tu madhara yake yalikua yanangojea uingozi mpya ndio uanze kujitokeza?.
Mkuu Kama kweli upo "fair"katika kuangalia hili tatizo, tuanzia kipindi cha Kikwete, hali ya umeme ilikua mbaya Sana, mgao, kukatika kwa umeme hovyo hadi waziri mkuu Edward Lowasa likamsababishia kujiuzulu.
Alipoingia Magufuli alifanya mageuzi makubwa Sana katika sector ya umeme, kumbuka alikua ni vijiji 2000 tu vimeunganishwa umeme Kati ya vijiji 12000 Tanzania nzima, hadi anakufa alibakisha vijiji 2500 tu kuunganishwa umeme.
Sihitaji kutaja Mambo Kama kuondolewa kwa "service charges", kuondolewa kwa gharama za kununua nguzo au transformar kwa wanaotaka kuunganishiwa umeme, vijijini kuunganishiwa kwa Tsh 27000,
Mgao kutokuwepo tena na mengi Sana siwezi kuyamaliza kuyataja.
Huwezi kueleweka Kama mafanikio yote haya yanapoanza kutoweka na kurudi enzi za Kikwete, sio rahisi watanzania kuelewa. Kwahiyo athari za kutofanya Maintainance zilikuwepo enzi za Kikwete, alipoingia Magufuli yeye hakufanya Maintainance yoyote kwa miaka mitano, tulitegemea umeme ungeendelea kukatika Kama ilivyokua katika utawala wa Kikwete, lakini hatukuona kukatika kwa umeme katika kipindi chake, ghafla tu baada ya kuondoka, athari za uchakavu zinaanza tena kujitokeza, hivi kweli watu wazima tunadanganyana kirahisi kiasi hiki?
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app