Mkuu bila ushahidi wa data utakua vigumu Sana kueleweka, tunataka kujua katika hicho kipindi cha mwendazake, ni kiasi gani kilikua kikitumika katika hizo "peak hours" ukilinganisha na hivi Sasa.
Wananchi wanataka kujua ni viwanda gani vipya, au ni uzalishaji gani ulioongeza katika hiki kipindi hadi tatizo la umeme kuwa kubwa ghafla.
Kinachotatiza watu ni kwamba, tatizo la umeme kukatika kwa sababu ya kuongezeka kwa uzalishaji, haliendani na ongezeko la uzalishi, tatizo linaonekana,lakini huo uzalishaji uliongezeka kutokana na kufunguka kwa uchumi hauonikani.
Tuneambiwa ni kiasi gani ongezeko la bidhaa viwandani Kama viwanda vya Cement, bati, nguo, chuma,na bidhaa zingine umeongezeka kwa kiasi gani ndio tungeelewa, vinginevyo itabaki ni maneno ya wanasiasa tu kupiga domo
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app