Ikiwa TZ mtatinga $500 billion na population yenu iwe chini ya watu 100 million then ni kweli Mtanzania mmoja mmoja atakuwa tajiri mno. Kila Mtanzania atakuwa anamiliki gari. Lakini ikiwa gdp yenu itatinga $500 billion lakini kwa bahati mbaya iwe kwamba mumezaliana kama panya na kufika watu 300 million basi tegemea umasikini kubaki pale pale. Hii ndio sababu China walisema kila familia izae mtoto mmoja tu ili uchumi unapokua by 10% kila mwaka basi mapato ya kila familia inaongezeka lakini ikiwa kwamba kila mwaka kuna mdomo mpya umezaliwa ya kukula chakula ndani ya familia basi mapato ya familia yanakwenda chini.
Wachina waliwaza kiuchumi zaidi. Sasa hivi bila kupanga uzazi, population ya China ingekuwa 2 billion people na kila Mchina angekuwa masikini wa kutupwa. Sasa India ambao hawapangi uzazi watapita China kwa wingi wa watu soon na japo uchumi wa India unakuwa kwa kasi, idadi ya watu pia inakuwa kwa kasi kwa hivyo umasikini wa India utabakia pale pale.