Hiki ndicho watanzania wanakipigania humu ndani. Mama aendeshe nchi kwa mawazo yake,atoe maamuzi kama Amiri jeshi mkuu wa Tanzania kwa maslahi ya wananchi wake na siyo kupangiwa na mtu mwingine.
Watanzania hawataki aletewe vimemo vya teua huyu, tangua huyu, fanya hivi na vile kwa mambo asiyoyataka.
Bora afanye akosee kwa maamuzi yake lakini siyo kuelekezwa na mtu mwingine. Wakenya mkiona Watanzania wanapiga kelele humu kuhusu nchi yetu muongee machache maana hamjui kinachoendelea.
Walioko jikoni ndio husikia vizuri harufu ya mapishi kuliko walioandaliwa chakula mezani.