joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,111
- 46,621
Hakuna "economist" yoyote makini atakayesema kwamba "remittances" ni Bora kuliko "brain drain". remittance/money vs job creation within the country.Sasa kama wewe sio mchumi nani alikuambia kwamba watu wanaokwenda kufanya kazi abroad faida yao kwa uchumi ni mdogo kushinda wale waliobaki nyumbani. Sio lazima uwe mchumi ili ujuwe kwamba watu wanaokwenda abroad wanafanya contribution kubwa sana kwenye uchumi za nyumbani. Ila sikulaumu kwa maana nyie hamna hio diaspora kubwa sasa unaona kama remittance ni utopolo mtupu. Kwa habari yako Kenya ina zaidi ya 20,000 trained but unemployed teachers, zaidi ya 10,000 trained but unemployed nurses. Sasa wakati mwingine ni vizuri kutulia na kuelewa kwamba ajira ni tatizo hapa Afrika. Hata nchi yenye emmigrants wengi zaidi ni India na Wahindi wanakwenda kufanya kazi, USA, Canada na UK kwa sababu hakuna ajira nyumbani India. Lakini wakifika ulaya wanaanza kutuma nyumbani hela ndefu kwanza in dollars na wanatuma dollars nyingi kushinda hata ile inayoingia kupitia tourism. Kenya sasa hivi tunapokea dollars nyingi kupitia remittance hata kushinda tourism au uuzaji wa chai au maua. Economist yeyote atakuambia kwamba remittance ni muhimu hata tu kwa kupunguza umasikini. Ni watoto wangapi wanasomeshwa na mama au baba zao wanaofanya kazi ulaya? Ni familia ngapi zimejengewa majumba na relatives wao wanaofanya kazi ulaya? Economist gani atasema kwamba remittance ni upuuzi kama wewe unavyosema?
Hao wasomi walikosa ajira huko Kenya, ufumbuzi sio kwenda kutafuta ajira huko nje, ufumbuzi ni kutumia Elimu Yao kutengeneza ajira.
Ukweli ni kwamba 70% ya waafrika wasomi wanaofanya kazi huko nje ni "cream and most intelligent" wengi walikuwa wameajiriwa, tena serikalini, hao unaosema waalimu na nurses ambao hawajapata ajira, wengi ni daraja la chini ukilinganisha na waliotoroka, Sasa Kama hata Kenya ameshindwa "competition"ataweza huko nje?