Siamini Kama "argument" ya hovyo kiasi hiki inatoka kwako, kwahiyo GoK ilivyowekeza kujenga reli hadi Malaba na kubembekeza nchi za Uganda, DRC, Rwanda na South Sudan kutumia reli ya Kenya, hawakujua kwamba huko hakuna biashara?, hadi Leo serikali yenu inaendelea kuwekeza bandari ya Kisumu ili kukamata masoko ya hizo nchi.
Hivi nikuulize swali, Kama itategemea mizigo ya Mombasa Nairobi, Je hiyo reli kurudi toka Nairo hadi Mombasa itabeba mzigo gani?.
Hivi unatumia akili kweli wewe?, taja ni nchi gani hapa Afrika ambayo reli yake inategemea "domestic market" pekee na ikatengeneza faida?, Ili reli itengeneze faida, lazima kusafirisha mizigo mikubwa, ndio sababu reli itakayofanikiwa kufika DRC ndiyo itakayofanikiwa Sana, kutokana na madini mazito, mbao na bidhaa za mazao ya miti yanayopatikana kwa wingi DRC. Wacha kujidanganya, msikilize Dr. David Ndii anaeleza vizuri kuhusu hili.