The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,516
- 14,186
I wish na Tzn tuwe na uchumi wa kama Kenya kwamba proportion kubwa iwe ni kwa ajili ya ndani.Wewe unaelewa economics vizuri kweli wewe? Eti unadanganya kwamba SGR ya Kenya haiwezi kuleta faida mpaka iunganishwe na Uganda. Unajua unachosema kweli au unaongea kufurahisha watu? Hivi wewe unajua kwamba hata SGR ya Kenya ikiunganishwa na Uganda bado zaidi ya 75% ya mizigo ya SGR itakuwa ni mizigo ya Kenya? Kati ya hio 75% karibu yote inakwenda Mombasa na Nairobi. In fact Kenya inaweza kupata hasara zaidi kwa kutumia mabilioni ya dollar kuconnect Naivasha hadi Malaba ukizingatia kwamba chini ya asilimia 20% ya mizigo ya Sgr itakuwa mizigo ya Uganda. Zingatia pia kwamba Waganda wengine watakataa kutumia treni na wataendelea kutumia lorry. Market ya Uganda ni ndogo sana ikiilinganisha na ya Kenya. Customers wengi wa SGR ni Wakenya sio Waganda. Mombasa port inapitisha 35 million tonnes of cargo na chini ya 25% ya hii inakwenda Uganda na around 75% inabaki Kenya, most of it inakwenda Nairobi. Tukiangalia hii kitu kiuchumi hakuna jinsi unaweza kuniconvince kwamba Kenya haitapata hasara zaidi ikiamua kujenga SGR kutoka Naivasha hadi Malaba ukizingatia kwamba Uganda ni market kadogo. Mimi sina ushabiki wa kijinga, mimi sioni jinsi Naivasha-Malaba itakuwa na faida kushinda Mombasa-Nairobi kwa hivyo uwache kudanganya watu. Najua hio ndio sababu kuu iliyowafanya Wachumi wa China Exim bank kukataa kutoa mkopo. Tukiangalia hii kitu kiuchumi na kiutaalam kabisa bila kuweka siasa au propaganda, ukweli ni kwamba route ya Naivasha- Kampala haitaleta faida ya kutosha kuoffset the cost of construction. SGR route ya Mombasa to Nairobi ina faida sana na itajilipa virahisi kwa sababu 70% ya mizigo ya Mombasa port inakwishia Nairobi na haipiti hapo. Nairobi- Malaba japo itagharimu Kenya $3 au $4 billion kwa ujenzi, najua haitajilipa virahisi ukizingatia kwamba mizigo inayokwenda Uganda ni kidogo sana. Tukifanya simple ROI (return on income) ni wazi kwamba kipande cha Naivasha Malaba hakitajilipa kwa urahisi. Kwa hivyo tukianalyse hili jambo kiutaalam bila ushabiki utaona kwamba hio route ya Kampala haina faida kwa Kenya kushinda route ya Mombasa-Nairobi ambayo ndio most profitable route in East and Central Africa. Mombasa-Nairobi ni route ambayo inaconsume zaidi ya 20 million tonnes of cargo per year wakati Uganda inaconsume 8 million tonnes of cargo per year. Mizigo nyingi za Kenya zinachezea Mombasa-Nairobi na hazipiti hapo. Mombasa-Nairobi route lazima itajilipa lakini huko kwingine sina imani nako.
Hii dhana ya kujenga reli kwa ajili ya jirani sio sawakwa hiyo nguvu kubwa tuiweke kukuza Uchumi wa ndani.
Kwa hapa Wakenya hongera kwa sababu reli inatumika ila mngejenga kwa ajiri ya Uganda ingewakata vibaya sana.