Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Tumia akili kuongeza mishahara hakuna tofauti na kuchapa pesa mpya kwa ajili ya kuongeza mishahara kuna mahesabu makubwa hapo kinyume chake wafanyakazi mnadanganya kuwa mmeongezwa mishahara kumbe mmepunguziwa mishahara mfano mshahara ni sh1000 na kilo ya mchele sh1000 kisha ukaongezewa mshahara sh1200 na kilo ya mchele ukapandishiwa kutoka sh1000 hadi sh1700 sasa hapo umepata faida gani kwa kupandishiwa mshahara ? Kwa kuwa kiwango ulicho pandishiwa ni chini ya kilichopanda kwenye gharama ya maisha ,kwa kifupi hapo utakuwa umeshushiwa mshahara ila kwa kuwa wafanyakazi wa serikali ni MAZUZU WENGIWAO WATASHANGILIA
Hahahaha, japo sina Elimu kubwa kukuzidi lakini sidhani Kama upo sahihi, wafanyakazi serikalini hawazidi laki Moja Tanzania, hata wakiongezewa kila mmoja Tshs 300000 kwa mwezi, hiyo inakua ni 3B kwa mwezi, kweli unataka kusema TSH 3B kwa mwezi ikiingizwa katika mzunguko wa uchumi wa Tanzania kwa mwezi inaweza kutumbisha uchumi wa Tanzania kiasi cha kusababishwa mfumuko wa Bei?,

Kwa siku Moja tu wachimbaji wadogo wadogo hapa Tanzania wanaingiza zaidi ya Tsh20B kila siku na bado hawasababishi mfumuko wa Bei, wewe unazungumzia 3B kwa mwezi.

Sababu kubwa ya mfumuko wa Bei ni upungufu wa bidhaa hasa chakula usioendana na mahitaji ya wananchi, ndio sababu mfumuko wa Bei hupungua kipindi cha mavuno na kupanda kipindi cha kilimo. Jaribu kufuatilia kwa makini mienendo ya mfumuko wa Bei hapa Africa
 
Why would anyone compare Chengdu to Chicago?

Chicago has the 9th highest city GDP in the world and all the cities ahead have way more population.
Tunalinganisha maendeleo sio theories, hivi ninyi mpo na shida gani?. Mzee wa kimasai mwenye kundi la Ng'ombe 8000 anayeishi porini katika vibanda vya nyasi bila maji wa umeme, na mfanyakazi anayelupwa $1000 kwa mwezi anayemiliki usafiri wake, amejenga Nyumba yake ndogo yenye huduma zote Kama maji, umeme, choo na watoto wake anawapeleka shule kwa usafiri wake, nani mwenye maendeleo?
 
Yani hivi unapima utajiri wa Jiji kwa majengo marefu? Sasa tuseme Dar es Salaam ni Tajiri Kulikov Zurich?
Tunapima maendeleo sio utajiri wa maneno, Sasa Nigeria na South Africa ipi imeendelea?, Nigeria na GDP kubwa, South Africa na GDP ndogo. Kenya na GDP kubwa na Mauritius na GDP ndogo?, tumia akili.
 
Mm na wamarekani wenzangu hatupendi sema basi tu, na ndiyo maana unaona tunaona hata uvivu kujibu mana tulishajengwa kisaikolojia tangu tukiwa wadogo kwamba US ni noma
 
Huu uzi umewafanya Wakenya kuanza kufikiri upya kuhusu GDP
Walikua wanalishwa matango pori na vyombo vyao vya habari na wanasiasa wao, ukitazama TV stations zao wakifanya mijadala kitu pekee wanachoshikilia ni "We have the biggest Economy in East Africa", baada ya hapo hawasemi huo uchumi mkubwa umewasaidiaje katika maendeleo ukilinganisha na hao wenye uchumi mdogo, hovyo Sana.
 
Wachina waliamua kuendelea kama Nchi, Africa tuliamua kutopiga hatua Hadi kuendelezwa huwa nawashangaa sana Waafrika wanaotaka kujifananisha na Watu Wamagharibi....

Miji yote ya Magharibi tayari ilikuwepo tangu miaka 1800s ila China, Korea, Japan walikuwa ni hermit Kingdoms au kwa maana nyingine walikuwa wako nyuma na hakutaka kuwa kama wageni wa Kimagharibi.

Japan ndio ikawa ya Kwanza katika kipindi kinaitwa Meiji Restoration mwishoni mwa Karne ya 19 na mwanzo mwa Karne ya 20 walitumia muda mfupi sana kupata maendeleo ambayo Ulaya walitumia Karne nyingi.

Wakaja China (Qin Dynasty) Na Joseon (Korea) Hawa wote walisumbuliwa na Japan kidogo ila Baada ya vita ya pili ya Dunia wakaanza kujiamulia Nchi zao zitaendelea....

Just imagine haya mataifa yaliathiriwa sana na vita za ndani na hata Ile ya Dunia lakini leo hii hawapangini Nini cha Kufanya na Watu wa Magharibi na tena wanaheshimiwa sana.

Kuna mtazamo mbaya sana na Taifa la North Korea ni maskini, Umaskini unaosemwa wa North Korea unatokana na Kutopewa fursa sawa ya kushindana na kuishi kama Kila mtu.
North Korea inaweza Kurusha Satellite yake yenyewe iliyotengenezwa na Watu wake wa ndani, ila ukija Afrika hakuna nchi Africa kuanzia Misri Hadi South Africa anayeweza kwa sasa. North Korea inawataalam wa Nuclear ambao wanatengeneza hadi mabomu, ila Africa Nzima hatuna....

Africa lazima tujue Nini tunataka na tunavipataje.
NOTE: Uhuru wa kuwatukana viongozi sio maendeleo
 
Hahahaha, japo sina Elimu kubwa kukuzidi lakini sidhani Kama upo sahihi, wafanyakazi serikalini hawazidi laki Moja Tanzania, hata wakiongezewa kila mmoja Tshs 300000 kwa mwezi, hiyo inakua ni 3B kwa mwezi, kweli unataka kusema TSH 3B kwa mwezi ikiingizwa katika mzunguko wa uchumi wa Tanzania kwa mwezi inaweza kutumbisha uchumi wa Tanzania kiasi cha kusababishwa mfumuko wa Bei?,

Kwa siku Moja tu wachimbaji wadogo wadogo hapa Tanzania wanaingiza zaidi ya Tsh20B kila siku na bado hawasababishi mfumuko wa Bei, wewe unazungumzia 3B kwa mwezi.

Sababu kubwa ya mfumuko wa Bei ni upungufu wa bidhaa hasa chakula usioendana na mahitaji ya wananchi, ndio sababu mfumuko wa Bei hupungua kipindi cha mavuno na kupanda kipindi cha kilimo. Jaribu kufuatilia kwa makini mienendo ya mfumuko wa Bei hapa Africa
Watumishi wa umma tuko takribani laki 7 kasoro iyo laki moja sio sahihi
 
Bro hii Chengdu ni mji ambao upo ndani ya province inaitwa Sichuan ambapo ndani ya Sichuan kuna mji mwengine unaitwa Chongqing, hiyo kwa high-rises mbona ni New York .. Chongqing CityView attachment 2065607 . Yani kwa kifupi US atafute tu wakubishana nae kuhusu maendeleo ila sio China.. and guess what bro, Chengdu ni mji wa 9 kiuchumi na Chongqing ni mji wa saba kiuchumi.. yani miji ya US ambayo inaweza angalau kuleta ushindani na miji ya china, haizid miji mitano .. China ni balaa bro
Mnanifrahisha sana mbona hamuweki video za Chicago nazo mnaogopa nn?
 
download (6).jpeg
 
Mzee tunachongelea hapa ni infrastructure za miji hii miwili ambapo Chicago imepigwa hands down na chengdu ofcoz utajiri wa Chicago unaweza ukawa juu ila kimaendeleo based on infrastructure na technology Chicago hatii guu mzee Acha kukaza kichwa
Infrastructures gan unazungumzia?USA kati ya watu 1000 karibu 900 wanamagari yap binafsi unlike china most of them anatumia public transport...unajua kwa barabara pekee USA ina zaid ya 6m km ambazo ziko paved against china yenye 4m km? Usiwe unaongea tu kwa kuangalia picha za downtown Chengdu ukaona umeshamaliza kila kitu
 
Watumishi wa umma tuko takribani laki 7 kasoro iyo laki moja sio sahihi
Sawa, hata wafike milioni Moja, bado ongezeko la mishahara Yao haiwezi kutikisa uchumi wa nchi, Kama nilivyosema, uzalishaji wa bidhaa na huduma ndio sababu kubwa wa kupanda au kupungua kwa mfumuko wa Bei.

Tanzania na Uganda tunazalisha chakula zaidi kuliko Kenya na Rwanda, ndio sababu mfumuko wa Bei Kenya na Rwanda ni mkubwa kuliko Uganda na Tanzania
 
Back
Top Bottom