Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Na wewe unaongea tuu kwaiyo magufuli city dodoma ni nini na kuhusu kigamboni ni mradi wa mda mrefu sio miaka mitano tuu mji ushasimama kwani jitihada za serikali huzioni kama kigamboni economic zone/ industrial zone ambayo ni part ya kigamboni city na miradi mingine kama dege eco village

Huwa nawaambia kila siku humu kwenye mambo ya msingi muache ushabiki muwe objective kama kweli mnataka kuisaidia nchi yenu. Yes najua huu ni uzi wa ushindani na majirani zetu tunatakiwa kuonesha umwamba wetu ambapo tuna mengi tu ya kusema na wao wanajua. Lakini la mipango miji tumefeli sana, kwa kuwa watu wengi wanafuatilia huu uzi, nadhani pia ni fursa nzuri ya kuambizana ukweli.

Kati ya sehemu huwezi kuniambia kuhusu development yake ni Kigamboni, hayo maeneo mnayopiga picha na kurusha humu mimi ndio zone yangu kila siku. Hiyo Dege mwaka wa saba huu magofu tu, utasikia mara sijui tuifanye chuo, mara sijui tuuze…..hakuna mwenye majibu hadi leo nini tunaenda kufanya pale…..hata Rais ukimuuliza atakwambia sijui. Estates kama Dungu Farm, Mwongozo n.k miaka sasa hazijaisha in totality, huwezi kabisa kulinganisha na za wenzetu au standard inayotakiwa kuwa. Usiniambie kuhusu sijui hiyo industrial/economic zone ambayo miaka karibu kumi sasa hakuna chochote.

Kigamboni eneo lililotakiwa kupangwa upya na kuendelezwa ni kuanzia feri mpaka mji mwema kuelekea Kibada, huko ndiko kulitakiwa kujengwa mji mpya baada ya kufidia watu na kuondoka. Pengine kuanzia mji mwema hadi Geza Ulole palitakiwa napo papangwe vizuri upya. Baada ya kuleta siasa na uswahili wetu mchezo ukafia pale.

Kigamboni ndio future ya Dar es Salaam, kasi ya watu kuhamia uko ni kubwa sana. Sasa una mji uko in a very potential area, costline ndefu na safi ajabu, mita 300 toka CBD lakini haueleweki na umeachwa tu na sasa hivi watu wanajijengea Tanzania style sababu mtu mmoja alimua kuvunja KDA na kuachia mambo yaendeshwe na madiwani ambao ndio wameifikisha Dar hapa ilipo.

I can swear to you guys, hate it or love it……Dar wasipoleta Masterplan na kuisimamia kikamilifu bila siasa ndani ya miaka 5, utakuwa ni mji wa ajabu sana in 20years to come. Kama tutajaaliwa uhai nadhani tutakuwa hapa tunasikitika pamoja. I love this city na nasikia uchungu sana kuona watu wanalichezea.
 
Si eti ni uzembe, watanzania wote ni wazembe to begin with. Hawa ni umaskini uliokita mizizi ndio inawafanya watoroke Tanzania. Do you think having 28 million people living in extreme poverty is a joke?
We jamaa mbona unapenda kuongea uongo si nimekupa jana TU taariifa mpya kuhusu idadi ya maskini Tanzania kwa mujibu was data zetu za ndani ?
 
Tutajie miji yenye urban planning nzuri Tz zaidi ya Tanga na Moshi
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Tanzania na urban planning ni kama Mbingu na Nchi. Japokuwa kuna juhudi nyingi za serikali zinahitajika, Moshi kuna afadhali kwasababu ya ustaarabu wa Wachagga. Maana wameweza kujitengenezea town yenye miundombinu mizuri, Usafi, na mpangilio mzuri. Sijawahi kukaa sehemu yoyote Tanzania yenye ustaarabu kama Moshi!
 
haya makazi yana nafuu kuliko slum ya aina yoyote kutoka kenya tena hzo nyumba ni nzuri sana na zina maji na umeme na barabara zipo

mm nimetokea mwanza bro huna cha kueleza chochote hapo na ujue mwanza ni mkoa uliozungukwa na milima mingi sana

na hzo picha unazopost ww still ni za muda mrefu sana kwann usitafute hzi πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡







Kwa Mwanza hutanidanganya chochote. Wala usijaribu. Unataka kuniambia kuwa hayo makazi niliyopost Kwa sasa hayapo? Tena Kwa aibu kubwa, ukiingia mjini kutoka south, kitu cha kwanza kuona ni hayo makazi. CBD ya Mwanza yenyewe haina nafuu. Ni maeneo tajiri tu kama Capripoint ndio utaona ahueni.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Tanzania na urban planning ni kama Mbingu na Nchi. Japokuwa kuna juhudi nyingi za serikali zinahitajika, Moshi kuna afadhali kwasababu ya ustaarabu wa Wachagga. Maana wameweza kujitengenezea town yenye miundombinu mizuri, Usafi, na mpangilio mzuri. Sijawahi kukaa sehemu yoyote Tanzania yenye ustaarabu kama Moshi!

Hujafika Tanga wewe. Moshi mji wa matambiko haukui. Hata ka kijiji ka Hai kwa sabaya na mbowe walioko gerezani kanakuwa kuliko Moshi.
 
this city reffered to as mombasa city. tz wako na darslam pekeyake
images (42).jpeg
 
Back
Top Bottom