Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Kuna watu wanauliza kuwa nina elimu gani 😂😂😂😂 Hii ni article ya Mwananchi. Msije mkasema ninawaonea.




Mwanza. “Watu wengi tunakimbilia kuishi milimani kwa sababu tunapata viwanja kwa bei nafuu; pia tunaepuka mizunguko mingi tukitaka kununua viwanja kwenye maeneo ambayo siyo ya milimani.”

Hayo ni maneno yanayosemwa na baadhi ya wakazi wanaoishi kwenye maeneo ya milimani jijini hapa.
Wakazi hao wanaeleza kuwa asilimia 75 wanaishi milimani na kwamba kwa kawaida umbali kutoka eneo la tambarare hadi kufika juu ya milima hiyo huanzia mita 50 hadi 300.
Gazeti hili lilitembelea mitaa mitano ya maeneo ya milimani mkoani hapa ambayo ni Mtaa wa Nyerere A, Nyerere B, Mbugani, Mabatini Kusini na Mabatini Kaskazini na kuzungumza na wakazi wa maeneo hayo, ambao walieleza kuwa kwa kiasi kikubwa wapo mbali na huduma za jiji.

Kwa nini watu wanakimbilia milimani
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao wanasema wanakimbilia kuishi milimani kwa sababu viwanja vinauzwa kwa bei nafuu, kwani sehemu ya kujenga chumba kimoja unapata kwa Sh150,000 hadi Sh200, 000.

Mkazi wa Mtaa wa Nyerere A, Msila Majonge na mkewe Rose Mary Majoge ambao ni wazazi wa watoto wanane, wanasema watu wengi wanakimbilia kuishi maeneo ya milimani kwa sababu ya upatikanaji wa viwanja hausumbui tofauti na maeneo mengine.

“Mimi nina familia ya watoto wanane, tunaishi huku juu kwa muda mrefu, lakini chanzo cha kuja kuishi huku ni tatizo la upatikanaji wa viwanja, ukitaka eneo zuri huwezi kupata kwa wakati, kwani kuna kuwa na mizunguko mingi, lakini huku unapata kwa muda mfupi tena kwa bei nafuu,” anasema Majoge.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Hassan Maulid anasema, watu wanaoishi milimani wana changamoto nyingi hasa upatikanaji wa huduma za kiutawala kutoka jiji, kutokana na maeneo hayo kuwa mbali.

“Huku milimani tunaishi tu, lakini masuala ya kiutawala hakuna, Jiji wametutenga hauwezi kupata huduma yoyote ya kijamii kutoka Halmashauri kwa haraka kwa madai kuwa maeneo ya huku hayafikiki kwa urahisi,” anasema Maulid na kuongeza: “Mimi ninaishi huku tangu mwaka 2002 na niliamua kuja kwa sababu ya hali ya maisha niliyokuwa nayo kwa wakati ule, kwani nilinunua eneo kwa bei ndogo na kujenga chumba kimoja maisha yakaendelea kama kawaida.”

Anasema asilimia kubwa ya wakazi wa Jiji la Mwanza wanaishi milimani, katika mtaa wake ana kaya 1, 068, watu 6, 587 na nyumba 658, na kwamba huo ni mtaa mmoja tu.
Hali ya usafi kwenye maeneo ya milimani ikoje
Akizungumzia hali ya mazingira na usafi kwenye maeneo hayo, Athumani Hussein anasema, watu wanaoishi milimani changamoto yao kubwa ni usafi, kwani maeneo ya kutupa taka hakuna na kwamba wamekuwa wakiishi kwenye mazingira magumu.

“Licha ya kwamba watu wengi tunakimbilia kuishi huku milimani, tuna changamoto kubwa ya usafi, kwani maeneo ya kutupa taka ni ya shida kulingana na jiografia ya maeneo husika,”anasema Hussein.
Kuhusu huduma za afya
Maulidi anasema: “Kinachotusaidia watu tunaoishi milimani ni umoja tuliokuwa nao, mtu akiumwa usiku wa manani kwa kuwa vituo vya afya vipo mbali, tunapiga filimbi tunakusanyika pamoja na tunamkimbiza mgonjwa hospitali.”
Anasema kutokana na umbali uliopo kufika barabarani wamekuwa wakishirikina kwa kila jambo la maendeleo, ili kuhakikisha maisha yao yanakwenda vizuri.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza anasemaje?

Akizungumzia makazi hayo, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida anasema siyo sahihi watu kuishi kwenye maeneo ya milinani na kwamba wengi ni wavamizi kwani maeneo hayo hayajapimwa.
Anasema Jiji haliwezi kupeleka huduma za kijamii kwenye maeneo hayo, kwa kuwa wakazi wake wengi wanaishi kinyume na utaratibu.
“Naomba nikwambie kwamba watu wengi wanaoishi milimani kwa hapa Mwanza ni wavamizi, kwani Jiji hatujapima viwanja hivyo na kwamba hata huduma za kijamii ndio maana hazifiki kwenye maeneo hayo,”anasema.

NEMC wanasemaje?

Ofisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Kanda ya Ziwa (Nemc), Edika Masisi anasema kwamba maeneo mengi ya milimani siyo salama, kwani hayana miti na kwamba sababu hiyo inaondoa uoto wa asili.

Masisi anasema, “Shughuli za ujenzi zinazofanywa kwenye milima mfano hapa Mwanza siyo salama, kwani uchimbaji wa mawe unaofanyika ili kujenga nyumba unasababisha kuondoa nguvu ambayo imeshikilia mawe hayo.”

Anaongeza: “Ikinyesha mvua kidogo, lazima kutatokea madhara, maeneo hayo hayana uoto wa asili, hivyo kutokana na jambo hilo inasababisha maeneo hayo kutokuwa salama kwa makazi ya binadamu.”
Anaongeza kwamba sababu kubwa inayosababisha watu wa milimani kupata madhara nyakati za mvua ni kwamba maisha yao ni ya kawaida, hivyo hata ujenzi wa nyumba zao zinakuwa siyo imara.

Akizungumzia usafi wa mazingira kwenye maeneo hayo Masisi anasema watu wanaosihi milimani wengi mazingira yao siyo salama kiafya na kwamba hayana vyoo kutokana na maeneo hayo kuwa na miamba mikubwa inayofanya zoezi la kuchimba vyoo kuwa gumu.
“Kwa kweli maeneo mengi ya milimani hakuna vyoo kwa sababu uchimbaji wake ni mgumu kutokana na miamba iliyopo, wanasubiri nyakati za mvua wanafungulia baadhi ya vyoo au wengine kujisaidia kwenye mifuko.

Kauli ya TMA

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema watu wanaojenga milimani wanapaswa kuchukua tahadhari, kwa kuangalia usalama wa eneo husika ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi, anasema ni vyema watu kabla hawajakimbilia kujenga milimani wakaangalia usalama wa eneo husika ili kuondoa madhara ambayo yanajitokeza, kwa kuwa maeneo hayo yanachangamoto zake hasa nyakati za mvua.

“Kitu ambacho naweza kusema kwa watu wanaoishi milimani ni kwamba wanatakiwa kuchukua tahadhari kabla ya kujenga, kwani siyo mawe tu yanaweza kuleta madhara hata udongo unaweza kusababisha athari kama hautatazamwa vyema,”alisema Dk Kijazi na kuongeza:
“Mwezi Septemba mwaka huu tutatoa taarifa ya hali ya hewa ambayo itaonyesha viwango vya mvua nchi nzima, hivyo wakati huo ukifika kila mtu atafahamu kitu gani kinaendelea kwenye hali ya hewa.”

Matukio ya vifo

Hivi karibuni watu wanne walipoteza maisha baada ya kudondokewa na jiwe kwenye eneo la mabatini kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
 
261383205_3076403625975001_3641088034174243776_n.jpg
 
Hii cable stayed bridge viaduct iko kwenye final touch, soon itakamilika, nina uhakika na hii road wataikarabati mana imechoka sn hii barabara since uhuru alafu viongozi wanapita hapo wakitoka Airpot kuelekea Magogoni, inaleta view mbaya na yenye kukera machoni nna uhakika itakarabatiwa mana BRT ipo karibu na hapo hawawezi kuiacha hivyo hivyo.
IMG_20211127_085654_679.jpg
IMG_20211127_085801_256.jpg
IMG_20211127_085740_291.jpg
IMG_20211127_085723_670.jpg
IMG_20211127_085727_606.jpg
IMG_20211127_085639_296.jpg
 
Hizi Asante Mchina kiukweli kabisa hizi nyingine ni trash, yn ugly huu ndio ukweli, dizain za kale sn kwa majengo ya hivi kukaa CBD
Screenshot_20211127-201736.jpg
 
Back
Top Bottom