Mimi Magufuli ninamkubali Sana, baada ya Nyerere anakuja Magufuli, ameifanya Tanzania iheshimike na kujulikana duniani baada ya kupoteza heshima yake ya kipindi cha Nyerere, lakini Kuna maeneo alifanya vibaya, wakati Nyerere alisisitiza haki za binadamu na demokrasia lakini uchumi ulimshinda, Magufuli alifanya just opposite ya Nyerere.
Nyerere wakati anaondoka madarakani alikiri kwamba sera zake za uchumi hazikufanikiwa Kama alivyotarajia, alikubali na kukiri mapungufu yake, bahati mbaya Magufuli hakupata muda huo, lakini ninaamini Kama angepata muda mrefu wa kuishi na kuandika kitabu Kama alivyofanya Mkapa, angekiri madhahifu yake katika hayo maeneo ya demokrasia, haki za binadamu na mapungufu katika kukabiliana na UVIKO 19