Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

Hii ni screenshot ya baadhi ya wanafunzi Bachelor of Science in Prosthetics and Orthotics (BSC.P/O)
event-201011f.jpg

kwani chuo cha pharmacy ndo hicho cha prosthetics and Orthotics? wewe unachanganya! Mimi naongelea school of pharmacy!
 
Hayo ni mawazo yako and ur entitled to your own opinion, hatuwezi wote kufanana mawazo na ndio maana kuna wapinzani na sheria inakulinda na inakupa uhuru wa kuwa na mawazo tofautii kwaiyo usitake tufanane kama wewe unaona alikua mbaguzi kupeleka maendeleo chato wengine na watanzania wengi hawaoni hivyo na ndio maana maza anaendeleza palepale alipoachia jpm, unasema alipendelea, kama kuna sehemu ilipendelewa hapa bongo ni dodoma kwa sababu investment inayofanyika huko sio ya kitoto mfano mdogo tuu international airport dodoma kwa sasa haina umuhimu wowote lakini inajengwa huko ilihali mikoa inayaongoza kupokea watalii wengi manyara na arushha hawana facility kama Iyo inayojengwa dom

Uzuri jpm hatokei dodoma angekuwa anatokea huko tusingepumua umu
Dodoma ipo kisheria toka 1977! Ni Azimio la Bunge kama ilivyo Geita Town ila mwendazake akaamua kuipuuzia kwa sababu zake binafsi.
 
Nitajie wilaya nyingine Tanzania iliyopata upendeleo Tanzania kama Chato kipindi cha Urais wa Marehemu Magufuli, yaani imejengewe uwanja wa ndege wa Kimataifa, ikapewa ferry, ikaanzishiwa mbuga ya wanyama, ikajengewa uwanja wa mpira, ikajengewa soko la dhahabu, ikajengewa machinjio na soko la mnada la kisasa, soko la kisasa, ikajengewa ofisi ya Tanesco ya kisasa, Ofisi ya CRDB ya kisasa, ikajengewa stendi ya mabasi ya kisasa, chuo cha VETA cha kisasa, hospitali yenye hadhi ya rufaa ya kanda, mabarabara na mataa ya barabarani, nyumba za polisi n.k.! Mind you Chato ina idadi ya watu 365,000 vs watu 807,000 Geita Town (sensa 2012)! Wacha kufuru mzee!


sorry mkuu.. Chato ipo burundi au vip mbona sielew? Au ulioa mke kutoka Chato akakuacha ndo inaichua chato nzima? (joke)
 
dodoma ipo kisheria toka 1977! Ni Azimio la Bunge!

Kwaiyo chato haipo kisheria hawastahili kupata maendeleo yoyote na kingine vitu kama burigi national park sio vitu vya kutajaa unakua kama mpinzni umekosa hoja burigi ilikua upgraded from game reserve to game park for conservation purposes sasa sijui ukanda hapo unatokea wapii
 
Kwaiyo chato haipo kisheria hawastahili kupata maendeleo yoyote na kingine vitu kama burigi national park sio vitu vya kutajaa unakua kama mpinzni umekosa hoja burigi ilikua upgraded from game reserve to game park for conservation purposes sasa sijui ukanda hapo unatokea wapii
Uwekezaji wake kipindi cha Magufuli ulitumia pesa za serikali bila kupitishwa na Bunge hilo liko wazi refer ujenzi wa uwanja wa Chato na majadaliano Bungeni!
 
Nlikuelewa, sema na mimi nlitaka wengine wajue kuhusu tatcot
Wanafanya kazi nzuri nawafahamu leo ndo nimejua kuna KSP japokuwa bado haitoi Pharmacy degrees! Halafu ipo tangu 2002, very strange! Nadhani ipo underfunded ndo maana haijaweza kuanzisha degree courses in Pharmacy mpaka leo.
 
Sisi wa wilaya ya Musoma Mjini tumejengewa Hospitali ya rufaa iliyowashida maraisi wa 4 waliomtangulia JPM na uwanja wa ndege unapanuliwa, sas sijajua na sisi tulipendelewa au?au utakua sisi tupo kisheria na Chato haipo kisheria.., nlitaka kusahau na barabara za lami za mitaani na mitaa km yote...
 
Sisi wa wilaya ya Musoma Mjini tumejengewa Hospitali ya rufaa iliyowashida maraisi wa 4 waliomtangulia JPM na uwanja wa ndege unapanuliwa, sas sijajua na sisi tulipendelewa au?au utakua sisi tupo kisheria na Chato haipo kisheria.., nlitaka kusahau na barabara za lami za mitaani na mitaa km yote...
Musoma Mjini ni mji na makao makuu ya mkoa wa Mara! Chato ni wilaya si mji wala makao makuu ya mkoa wa Geita!
 
Chato ilipendelewa na matokeo yake Geita Town ikabaki nyuma! Kama JPM ange-concentrate effort kuendeleza Geita Town basi ungekuwa mji mmoja very modern ila kwa sababu anazozijua yeye binafsi akagawanya rasilimali na awamu yake ya pili alikuwa awekeze zaidi aliona aibu kufanya yote awamu ya kwanza. Matokeo yake ubinafsi huo unawafanya wana Chato sas hivi kutaka kujitenga maana wanajiona bora zaidi ya wenzao wa Geita! Huo ndo ukweli najua mtatukana humu ndani!


Geita-Travel-Guide-806x440.jpg





Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Geita Town
ErsCxhHXAAAVb7m




VS


Hospitali ya Wilaya Chato
chato-pic.jpg




VETA Chato
ErJWk14VkAY4Hy-
Hapa ☝️ mzee geza umetupiga changa la macho, umewahi kufika hizi sehemu au unaokota picha Google na kuropoka tu.? Geita town pameendelea zaidi, mara hata 100 mbele ya chato, chato ni kijijini tu mzee wangu, kuanzia individual development level na kila kitu geita ipo mbele ya chato... Kuhusu kupendelewa naeza sema ndio au hapana, kwa mfano kujengwa kwa uwanja wa ndege chato ni sahihi since kuna mbuga ya wanyama kubwa tu (CHATO BURIGI) ili watalii washuke moja kwa moja (this the reason ule uwanja wa ndege wa KIA kutengenezwa Moshi while Arusha ndio tourism hub na ni jiji kubwa kulinganisha na Moshi) alafu hata hivyo chato ipo karibu sana na Geita mjini, pia ulikua ni mpango wa serikali kujenga/kuboresha airports kila mkoa.... kujengwa kwa tawi la CRDB chato ni sahihi, rudi kwenye makusudio ya benki hiyo na lengo la kuanzishwa kwake, Anza hapa CRDB means COOPERATIVE RURAL DEVELOPMENT BANK (benki ya maandeleo ya vijijini) hizi zipo kila mahali hapa tz kuna ubaya gani katawi Chato kujengewa yakwao.? na ni wilaya kubwa tu.?.. kuhusu VETA pia hakuna ubaya kujengwa Chato, ukiwa kiongozi lazima uongozi huo uanzie nyumbani, lazima nyumbani kwako na penyewe pawe mfano, wazungu wanasema "Charity begins at home" haikua dhambi kuwatengezea wakwao chuo Ili wapate ujuzi na hatimae kujikwamua katika umaskini na kuleta maendeleo CHATO na taifa Zima kwa jumla wake.. kuhusu HOSPITALI kubwa, kidogo kuna kaupendeleo raisi magufuli alifanya, kwasababu moja, makao makao makuu ya mkoa wa Geita ni Geita mjini hivyo basi hospitali Ilibidi itengenezwe makao makuu ya mkoa, lakini hata hivyo bado hospital kutengenezwa kule sio dhambi since Chato ni sehemu ya mkoa wa Geita, na pia ilikua ni mpango wa serikali kuwapunguzia Safari watu Kagera watakafuata huduma za afya mkoani Geita.. chukua hii mzee geza HUWEZI KUWA KIONGOZI WA TAIFA UNAFANYA MAENDELEO MAKUBWA NCHI NZIMA ALAFU NYUMBANI KWENU WATU WANAKUFA NJAA, huo utakua ni uhanangwa, kila siku tunawacheka wakenya humu raisi wao Moi alivyokufa nyumbani kwao hakutengeneza hata kipange cha barabara ya lami na jeneza lake lilipekwa kwa chopa

usilazimishie mikoa mingine nimekutolea mfano candid wa jinsi Geita Town ilivyokuwa disadvantaged wewe unalazimishia Dodoma!
Chato haikupendwlewa ni chizi pekee ndio utamuaminisha huu ujinga
 
Sisi wa wilaya ya Musoma Mjini tumejengewa Hospitali ya rufaa iliyowashida maraisi wa 4 waliomtangulia JPM na uwanja wa ndege unapanuliwa, sas sijajua na sisi tulipendelewa au?au utakua sisi tupo kisheria na Chato haipo kisheria.., nlitaka kusahau na barabara za lami za mitaani na mitaa km yote...
Nchi nzima iko hivyo mpaka vijijini kule ni hivyo hivyo, ukiona 90% ya wananchi wanakukubali juwa kwamba kazi umeifanya, hawa wachumia tumbo wa mitandaoni wala wasitusumbue.
 
Kikwete alitaka kuingiza nchi kwenye mkataba wa kipumbavu kwa bandari ya Bagamoyo amabapo mzigo wa madeni ungekuwa mkubwa kwa wtz, alijenga chuo kikuu Bagamoyo nk, hivi, mradi wa hii bandari gharama yake inalingana na pesa za chato? Hospital ya Chato ni kanda, iweje ww uiweke kuwa ni ya Chato? Usifanye watu wajinga bhana
 
Back
Top Bottom