joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,111
- 46,621
Demokrasia ni Jambo lililotafsiriwa na kukubalika" Internationally", kwahiyo lazima kuwepo na "standard definition" ambayo itatumika Kama "benchmark" ya kusema Kama kweli nchi Fulani imefikia kuitwa ni nchi yenye demokrasia.Demokrasia huwezi kuiweka kwenye kapu moja. Huwa inabadilika kutokana na muda na utamaduni wa watu katika sehemu husika.
Kuna nchi mwanamke anatakiwa kujifungia ndani wakati wote, kama wananchi wa nchi hizo wameikubali hali hiyo (kwa mama, bibi na dada zao) basi hiyo ni demokrasia kwao. Kuna nchi nyingine huo unaonekana ni unyanyasaji wa wanawake, wakati miaka 100 tuu iliyopita nchi hiyo hiyo ilikuwa hairuhusu wanawake kupiga kura.
Kuna vigezo vya kimataifa vilivyokubalika duniani vinavyotumika kuzipanga nchi zote duniani kuanzia nchi yenye demokrasia zaidi, hadi nchi isiyo na demokrasia duniani, Kama ilivyo katika kujua "Peace index", GDP, corruption perception index, Life expectance index, Literacy rate, na vigezo vinginevyo ambavyo kwa pamoja vinatengenaza "Human development index".
Inakuaje kote huko tunakubali lakini inapofika kwenye demokrasia unataka kila nchi ijichagulie vigezo vyake yenyewe?, Ukitaka hivyo basi nchi zenye kusumbuliwa na rushwa pia zitasema kwamba kwao kutoa pesa ili kupata haki wasiyostahili sio rushwa kwasababu huo ni utamaduni wao wameuzoea





joined 25 sept, and all of his/her replies/comments are in this thread