Uchumi wowote duniani lazima uanze katika kujitosheleza kwa mahitaji muhimu ya binadamu, ni jambo la kuchekesha na kusikitisha kwa nchi yenye uchumi unaotegemea kilimo kutegemea chakula cha kunununua toka nchi za nje, ni sawa na kusikia nchi yenye uchumi unaotegemea madini kama Almasi, lakini nchi hiyo hiyo ananua Almasi toka nchi za nje, au nchi inayochimba mafuta kama Qatar na nchi zingine za Kiarabu na Iran, kuagiza mafuta toka nje.
Ukweli ni kwamba, uchumi wa Kenya unategemea zaidi investors wa Kigeni ambao ndio walioshikilia ardhi kubwa yenye rutuba, wao wanazalisha mazao kwa ajili ya matakwa ya masoko yao nje ya Kenya, hawa wawejezaji kamwe hawajali mahitaji ya Kenya na wakenya, ndio sababu hakuna "connection and association", kati ya vinavyozalishwa Kenya na mahitaji ya soko la Kenya.
Wawekezaji hawapaswi kumiliki ardhi ya kilimo ambayo ndio msingi wa uchumi wa Kenya, wao wangebaki katika sector zingine kama utalii, Banking, Communication, Manufacturing and others.