Sijui Egypt ilitakiwa ifanye nini. Ila ninachojua ni kuwa jirani yako hawezi kukupiga ngumi ya kisogo na wewe uanze kucheka na yeye. Egypt wakiamua kulipua bwawa basi kisheria Ethiopia wana haki ya kulipiza mapigo. Sidhani kama unafahamu umuhimu wa Aswan HIgh dam kwa uchumi wa Egypt na jinsi itaumiza Egypt ikilipuliwa na Ethiopia in a retaliatory strike. Aswan ina umuhimu mkubwa sana kwa Egypt kwa sababu inatumika kuregulate flow of water in the Nile wakati wa kiangazi. Wakati kuna kiangazi Egypt, maji yaliyohifadhiwa ndani ya Aswan high dam huwa yanakuwa released kidogo kidogo ili kukidhi mahitaji ya Egypt kwenye irrigation na domestic use. Bila Aswan high dam, maji katika Nile upande wa Egypt utakuwa chini sana wakati wa Kiangazi na watu watakosa maji kwa matumizi mbalimbali. Hii dam ina act kama valve ya kurelease maji polepole wakati wa kiangazi na kuzuia famine na drought. Egypt sio wajinga. Wanajua fika kuwa wakibomb dam ya Ethiopia, basi dam yao pia itabombiwa.