Ndio sababu kila eneo moja la radar halipaswi kuhudumiwa na radar mbili tofauti, Kama kungekuwa na uwezekano wa Radar moja kufika maeneo yote Tanzania, tusingejenga Radar 4, tungeweka moja tu.
Kwa upande wa SGR kwasababu inatumia fiber, kuna sababu gani ya kujenga Control centres nyingi wakati moja tu inafikia trains zote popote pale nchini?.
Kuhusu vituo vya redio, mfano uliotoa hauendani na maelezo yako, Kila redio inarusha matangazo yake kutoka katika kituo kimoja tu, TBC lazima wawe na center moja ya kurusha matangazo, ITV, Clouds au Wasafi, kila moja lazima iwe na Centre moja tu.
Kama kutajengwa reli nyengine ya SGR, nayo itakua na Control Center yake, wanaweza kuijenga mkoa wowote watakaochagua, lakini watakua na Control Centre moja tu.
Logic ya kuwa na backup control centres apart from the main centre ya Dar in Kwamba Kama kukitokea hitilafu kwenye main centre ya Dar (lets say hitilafu ya moto etc etc) shughuli za treni bado zitaendelea.
Kumbuka kuwa treni zetu zitakuwa zinaendeshwa kwa kiwango kikubwa kutokea kwenye control centre, dereva yuko pale kwa ajili ya kufanya vitu vichache sana, Watu wa control centre watakua na uwezo hata wa ku-commanda treni isimame au iongeze speed etc etc.
Nimeona pia mnajaribu kutumia anlogy ya RADAR coverage
Vs. Fiber optic cable coverage katika mfumo wa SGR
🙂
RADAR:
RADAR ni mfumo wa mawasiliano bila waya unaotumika ku-detect vitu kwa kuvimulika na signal na kutumia returning/bouncing signal kutoka kwenye hivyo vitu vilivyomulikwa ili kujua vitu hivyo viko katika umbali gani au maeneo gaini. Vitu hivyo vinaweza kuwa ndege, missiles, drones etc.. Kwa kifupi coverage area ya RADAR station inategemea na nguvu yake ya kutuma signal (transmit power) pamoja na aina ya antenna zinatotumiwa. Kwa hio tunapokuwa na RADAR 5 za civilian nchi nzima maana yake ni kuwa kila RADAR station moja ina-cover eneo (sector) fulani la anga la nchi na zikiwa combined nchi nzima inakuwa covered. Hivyo basi hakuna ndege itakayopita kwenye anga letu bila ya watu wetu kuitambua, ofcourse tunazo pia RADAR stations za kijeshi ambazo ziko classified na hutuwezi kuzijadili hapa.
Fiber Optic Cables:
Fiber optic ni mfumo wenye kutumia nyaya ndogo ndogo sana zilizowekwa pamoja kama mkongo kwa lengo la kusafirisha mawasiliano kwa kutumia speed ya mwanga.
NJIA ZA MAWASILIANO KWENYE SGR YETU:
Kati SGR yetu kunajengwa aina mbili za mawasiliano kama ifuatavyo:
1 - Fibre optic - Huu ni mkongo umejengwa kandokando ya reli na utatumika kwa mambo makuu mawili (1)
Traffic Management yaani kupokea mawasiliano ya data moja kwa moja toka kwenye treni itakapokuwa inapita kwenye reli na kupeleka katika
control center na pia kutoa mawasiliano ya data kutoka kwenye
control centre na kupeleka kwenye treni. (2)
Backhaul kwa mitambo ya mawasiliano ya wireless yenye kutumia standard ya GSM-Railway (GSM-R).
2- GSM-R - Hii ni standard ya mawasiliano ya kutotumia waya (radio communication) maalumu kwa ajili ya matumizi ya kwenye reli. Katika SGR yetu mfumo huu umejengwa kwenye njia nzima katika kila kilometer kama 15 (hii ndio typical coverage radius yake) hivi utaona kuna minara au Base Transmit Station (BTS) ya GSM-R. Mfumo huu utatumika kwa ajili ya
Controll and Signalling ya SGR yetu ambapo
madereva wa treni wanatumia kwasiliana na
control centre pamoja na mawsiliano mengine yote ya data na SMS ndani ya treni. Backhaul yake itakuwa ni mkongo wa fiber optic.
MIFUMO YA UENDESHAJI YA SGR YETU:
Sasa njia hizo mbili za mawasiliano hapo juu ndio zitatumiwa ku-feed data kwenye mifumo miwili ya uendeshaji ya SGR yetu ambayo ni European Train Control System - level 2 (ETCS-2) na European Railway Traffic Management System (ERTMS).
Nadhani hii sasa itaeleweka.