Barabara ya Mwendokasi kutoka Maktaba hadi Tegeta kuanza kujengwa, Ubungo Kimara kufumuliwa

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Kwa ufupi sana

Serikali ya Tanzania kupitia Tanroads leo 30 Juni 2023 inasaini Mikata Minne ya ujenzi wa miundombinu ya Usafiri wa haraka wa Mabasi (BRT) awamu ya nne.

Inaanza kujenga barabara ya Magari yaendayo haraka kutoka Katikati ya Mji (Maktaba) hadi Tegeta, ambayo itajengwa na Wakandarasi wawili. Mmoja kutoka Maktaba kadi Morocco na mwingine kutoka Morocco hadi Tegeta ikiwemo ujenzi Madaraja.

Pia Serikali imesaini Mkataba wa upanuzi wa barabara ya Morogoro kutoka Ubungo hadi Kimara kuwa ya njia nane kutoka Njia sita za sasa.

Pia inasaini Mkataba wa barabara Vikawe kutoka Mapinga hadi kuunganisha barabara ya Dar Morogoro na ile ya Dar Bagamoyo

Ipo hivi:

1. Mkataba wa kwanza ni Km 13 kutoka Maktaba hadi Mwenge then inakata Kona hadi Ubungo kupitia barabara ya Sam Njuma

2. Mkataba wa pili ni Ujenzi wa barabara ya Mwendokasi kutoka Mwenge hadi Tegeta km 15. 63.

3. Mkataba wa tatu ni kwamba pale Mbuyuni kutajengwa kituo, Simu 200 patajengwa kituo na Kivukoni Terminal watajenga kituo hizi ni Depot. Zitajengwa na Mkandarasi mmoja.

4. Upanuzi wa Barabara Ubungo hadi Kimara kuwa ya Njia nane badala njia 6 za sasa

5. Mkataba mwingine ni barabara kiwango cha lami kutoka TAMCO Vikawe Mapinga km 23 na sehemu ya Pili Pangani hadi Mapinga km 13.59

Stay tuned


=====
-2034873106.jpg

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta leo tarehe 30 Juni 2023, akisaini mkataba kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkandarasi kutoka Kampuni ya China Geo – Engineering Corporation ya China kwa ajili Ujenzi wa Miundombinu ya barabara yenye urefu wa Km. 13.5 kuanzia Maktaba ya Taifa mpaka Mwenge ikijumuisha kipande cha Barabara ya Sam Nujoma kutoka Mwenge mpaka Ubungo.

Mkataba pia unahusisha upanuzi wa Daraja la Selander, Uenzi wa Vituo Vikuu Viwili vya Mabasi, Vituo vya Kawaida vya Mabasi Ishirini (20) na Vituo Mlisho (Feeder Station) kumi (10).

Mkataba huu ni wa gharama ya Shilingi 174,380,157,323.00, na umepangwa kukamilika katika muda wa miezi 18.
-25576279.jpg
1994089566.jpg

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta leo tarehe 30 Juni 2023 akisaini mkataba kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya barabara yenye Urefu wa Km 15.63 kuanzia Mwenge mpaka Tegeta.

Mkataba huu pia unahusisha upanuzi wa Madaraja matatu, (Mlalakuwa, Kawe na Tegeta), Ujenzi wa Vituo Vikuu vya Mabasi, Vituo vya Kawaida vya Mabasi Kumi na Tisa (19) na Vituo Mlisho (feeder station) Vitano (5).

Mkandarasi aliyeshinda kutekeleza mradi huo ni Kampuni ya Shandong Luqiao Group Co., Ltd kutoka China kwa gharama ya Shilingi 193,855,936,443.00, Ujenzi umepangwa kukamilika katika muda wa miezi 18.
-1489397948.jpg
-417414297.jpg
-715725483.jpg

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Geofrey Kasekenya akishuhudia Utiaji Saini wa Mikataba Minne ikiwemo Ujenzi wa Karakana (Depot) Mbili na Kituo Kikuu cha mabasi kimoja.

Mikataba hiyo imesainiwa leo tarehe 30 Juni 2023 na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar- es Salaam.

Mkandarasi aliyeshinda tuzo ya Ujenzi huo Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd kutoka China kwa gharama ya Shilingi 60,984,151,987.18, Ujenzi umepangwa kukamilika katika muda wa miezi 18.
75369357.jpg
-696699830.jpg

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Geofrey Kasekenya akishuhudia utiaji saini wa mikataba minne ikiwemo Ujenzi wa Karakana (Depot) Mbili na Kituo Kikuu cha mabasi kimoja.

Mikataba hiyo imesainiwa leo tarehe 30 Juni 2023 na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar- es Salaam.

Mkandarasi aliyeshinda tuzo ya Ujenzi huo Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd kutoka China kwa gharama ya Shilingi 60,984,151,987.18. Ujenzi umepangwa kukamilika katika muda wa miezi 18.
2021336279.jpg
948084998.jpg

Serikali kupitia TANROADS imesaini mkataba wa Uenzi wa Barabara ya TAMCO – Vikawe hadi Mapinga kwa kiwango cha lami, sehemu ya Pangani hadi Mapinga (Km 13.59).

Mkataba huo umesaini leo tarehe 30 Juni 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar- es Salaam na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya.

Taarifa ya Mtendaji Mkuu TANROADS imesema aliyeshinda tuzo ya utekelezaji wa mradi huo ni Kampuni ya Kings Builders Ltd ya Tanzania, Mradi utajengwa kwa gharama ya Shilingi TZS 17,859,098,225.00, Muda wa utekelezaji wa mradi ni Miezi 12.

Barabara hiyo ina jumla ya km 22, inaanzia katika Mji wa Kibaha ambapo ni Makao Makuu ya Mkoa wa Pwani inakwenda hadi Mapinga katika Wilaya ya Bagamoyo

Aidha Barabara hiyo ni kiungo muhimu kati ya barabara ya kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na barabara ya kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro, Arusha na Tanga kupitia Bagamoyo.

Hata hivyo Mhandisi Mohamed Besta ameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo serikali ilielekeza kuanza Ujenzi wa Sehemu ya Kwanza yenye urefu wa km 8.41. Ujenzi ulianza mnamo mwaka 2013/14 na maendeleo ya mradi yamefikia asilimia 40%.
 
Mama hii miradi yako ni heavy, tuliona hapa bwana yule akitujengea kibarabra cha cha pale Mwenge kwa kuwakamua pesa zao wabunge.

Leo umeamuwa mama. Jioneeni"




Jamani hii ni mi Dirham ya Dubai nini?
 
Mama hii miradi yako ni heavy, tuliona hapa bwana yule akitujengea kibarabra cha cha pale Mwenge kwa kuwakamua pesa zao wabunge.

Leo umeamuwa mama. Jioneeni"




Jamani hii ni mi Dirham ya Dubai nini?
Miradi sio sindano mpaka uitafute sana ndio uione. Miradi ikiwepo kila mtu anaiona
 
Back
Top Bottom