1) Bandari ijengwe ila.masharti magumu katika huo.mkataba pia yaangaliwe

2) Bandari ijengwe kwa pesa za ndani..hata kama itachukua miaka 23 Ili kuhakikisha faida yote inaingia Serikali.

3) Bandari ijengwe kwa kushirikiana na hizo nchi Kama Ilivyo..Kisha kuundwe kampuni ya pamoja Kama Ilivyo swala kwenye Mambo ya gesi na madini, kampuni hio iwe na wajumbe sawa kutoka kila nchi na pia zipokezane kwenye nafasi ya CEO wa hio Bandari kwa kipindi cha miaka miwili miwili...

faida inaweza kugawanywa kwa kuzingatia nani kawekeza kiasi Gani,..ama faida kila nchi ipokezane kwenye kuchukua faida..mfn.mwaka huu ni tz, mwakani ni China, mwaka ujao keshokitwa ni oman mpaka hao wakorea.

4) Bandari isijengwe mpaka.pale Taifa litakapokuwa na uwezo wa kuijenga yenyewe bila kuhitaji msaada kutoka nnje..

5) Badala ya kuhangaika na hio Bandari ya bagamoyo Tanzania iwashawahishi hao wawekezaji..wajoin kwe mpango wa kuiboresha na kuipanua Bandari ya sasa ya Dar..ikiwemo kuongeza ukubwa wake wa eneo..kwa kuchimba kina bahati I..na kuvunja baadhi ya majengo ikiwemo feri na soko lake..na ofisi zingine pale Ili kupata eneo kubwa sawa na la bagamoyo Ili kuufanya eneo hilo lifanane na eneo la bagamoyo
Mkataba umeusoma kama unaona siombaya ukaudondosha hapa na sisi tukaupitia
 
Wasepe waende wapi? Wana pa kwenda penye uchochoro wa bwereree kama Tanzania? Nchi nyingine zinajitambua na haziwezi kuingia mkataba wa kijinga namna hiyo. Ni Tanzania tu yenye viongozi wenye uchu wameona uwezekeno wa kuhonga ili wachukue hicho kipande. Hawa ni watu hatari sana sana na wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote.
Kwanini mikataba inafichwa?
 
hivi kwa akili ndogo tu mimi niweke sh 100 kwenye mtaji halafu wewe uweke sh 1 then mimi ninufaike pakubwa kwenye mradi inakuja akilini kweli yaani bila haya unasema mwekezaji anaweka trilion 20+ hlf tanzania inaweka bilioni 40+ halafu tanzania inufaike upo serious kweli!!!!

ni akili ya mku.....ndu tu ndio inaweza kukubaliana na huo ufala
Mzigo sasa uenda kufanyika
 
Mama samia tujengee bandari.sisi fuko nyuma yako tunakupenda...hatuwez kuacha kujenga bandar eti kutegemea kuishi kwa kudra za mwenyez mungu
 
Nakubaliana nawe 100%, na hasa tatizo la Ujamaa kwa nchi yetu. Yaani ujamaa ni uovu. Ujamaa umeharibu fikra na uweo (ability) wa ku functiom as normal human beings.
Nachukia umaskini, nachukia ujinga, nachukia ufisadi, nachukia dhuluma na pia nachukia unafiki lakini hivyo vyote viko kwenye furushi la ujamaa. Ujamaa na umaskini + uvivu + ujinga ni kitu kimoja.
Nimetembelea baadhi ya nchi za iliyokuwa Soviet Union, nimeishi na kufanya kazi na watu wenye asili ya kijamaa yaani wanafanana mno. The effect of brainwashed education and mass opiom of silly politics vimewaharibu. Halafu wanajiona wako sawa.

Hawa leo wanaojiita "wanyonge" na eti "wazalendo" ni waganga njaa, wabinafsi na watu wenye chuki tu. Most of them ni "nationalists" not not and never "patriots". There's a vast difference between "Utaifa na "Uzalendo". Utaifa ni uovu uliofungashwa kwa ustadi. Ni hali ya kutaka madaraka na kujinufaisha wao tu. Nationalism ina hila nyingi, ubaguzi, dhuluma na uharibifu. Hao wnaojiita wazalendo ni wasaka madaraka, vyeo, fursa kwa gharama ya wananchi na umoja wa kitaifa. NI waharibifu, wezi na wahuni tu.

Ndio maana mwaka 1967 hayati Mwl alipotangaza ku-Taifi(a)sha (nationalization) mali za watu wenye uwezo (kama hayati Magufuli naye alivyofanya) kwa kigezo cha Utaifa (kipropaganda akakiita uzalendo na eti kulinda mali za nchi) wasio na akili, wenye wivu, "wanyonge" walimuunga mkono. Lakini ile ya Mwl mwaka 1967 ilikuwa dhuluma ya wazi na ina adhabu yake - pengine ndio maana hadi leo watoto wa wale wale "wanyonge" na "makabwela" bado wako kule chini na wanateseka kiuchumi na kifikra. Hawakujifunza makosa ya wazazi wao, nao mwaka 2015 wakamshangilia Mwendazake aliposema "yeye ni Rais wa wanyonge (ubaguzi + kisasi) .....na kuwa atawafanya matajiri kuishi kama mashetani....." Akapora mali na fursa za matajiri.Swali, Je hao wanyonge sasa wanaishi kama malaika? Wamekuwa matajiri? au je sasa hivi wanaishi kama matajiri ? (majibu ya kipuuzi kuwa kuna elimu bure, mashule kujengwa, mahospitali, barabara na reli au kununua ndege - ni majibu ya kukariri na kusadikika sio ya kweli wala halisi). Kwa kila tajiri aliyefilisiwa, nafasi yake wamezaliwa au kutenegenezwa maskini kwa mamia kama sio maelfu. Ile ni sera ovu, katili na mbaya sana kiuchumi. That's idiocy and fallacy is the direct product of Ujamaa and nationalism mantra, respectively. Na huu uporaji na uharibifu wa hayati Magufuli una gharama na watalipa wao na watoto wao - ndivyo ilivyo.
Sababu kubwa ya Magufuli na Mwl Nyerere kupata uungwaji mkono na "wanyonge" ni ujinga na upofu wa fikra. Kwa Magufuli ni Ujinga na Ujamaa. Wajamaa wanachukia utajiri. Wajamaa ni watu waharibifu. Mimi Ronald nawachukia wajamaa, ndio, nauchukia ujamaa damuni!

Uzalendo (patriotisms) ni nini? Upendo na heshima kwa watu/wananchi wenzako (bila ubaguzi) na mapenzi kwa nchi yako.
Tena ni muhimu kujua kwamba uzalendo unajengwa, yaani hauzaliwi au kuzuka tu; na unajengwa kwenye misingi ya haki, ukweli na upendo unaotoakana na ukuombozi wa fikra, na kupevuka kwa jamaa na tamaduni husika. Uzalendo unathamini, kuheshimu, unatetea na kulinda Katiba ya nchi na sheria halali zilizopo; uzalendo unaheshimu na kutukuza mambo ya kweli, yaliyo mema na yenye sifa njema kwa nchi yako, watu wako na familia yako. Uzalendo hauna ubaguzi au ubinafsi. Uzalendo sio itikadi na kuimbishwa nyimbo au kukaririshwa vitu. Uzalendo ni kuwa tayari kwa mambo "ideas/ideology" sio vitu au kuganga njaa na kupewa vyeo. We just need to RESET as a nation.

Moja ya sababu kubwa za mimi kutaka na kutamani katiba mpya ni ili tuzike ujamaa. Kisha tuanze na sera mpya za uzalishaji mali ili kujenga uchumi halisi na sio wa ki propaganda, kama huu uliopo sasa. Uchumi ambao baada ya miaka 60 ya uhuru, Mtanzania kweli atakuwa huru kiuchumi na kifikra na mwenye maisha bora - na sio hizo takwimu zenye kuonyesha maendeleo huku wananchi wengi wakizidi kuzama katika ziwa la umaskini, ujinga, maradhi, siasa chafu na mambo kama hayo.
Kama tatizo ni ujamaa basi ondoeni kwenye katiba kipengele hicho kinachosema "Tanzania ni nchi yenye kufuata mfumo wa siasa ya vyama vingi" kwamba "Tanzania ni nchi inayofuata siasa ya ujamaa na kujitegemea"
 
Kama tatizo ni ujamaa basi ondoeni kwenye katiba kipengele hicho kinachosema "Tanzania ni nchi yenye kufuata mfumo wa siasa ya vyama vingi" kwamba "Tanzania ni nchi inayofuata siasa ya ujamaa na kujitegemea"
Hata China ina hayo maneno ya Ujamaa kwenye constitution lakini Private Capital and invest leads the economy
 
4. Masharti Magumu

Hoja nyingine inayosemwa ni kuwa masharti ya kuendesha mradi wa bagamoyo ni magumu. Inawezekana kuwa hoja hii ina mashiko na ndio maana ni hoja pekee ambayo Serikali inaitaja. Hata Bungeni ndio hoja Waziri wa Uchukuzi ameizungumza katika hotuba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka 2019/2020.

Lakini tuulizane, hivi mahala ambapo watu wanazungumza, kila upande una wajibu wa kuja na mapendekezo yake (proposal) na upande wa pili una haki ya kuja na counter proposal. Kuweka mpira kwapani sio njia sahihi hata kidogo, ni udhaifu uliopitiliza.

Kama serikali iliweza kwenda hatua ya ziada kuvutia mradi wa Bomba la Mafuta la Uganda kwa kutoa vivutio maalum vilivyopelekea hadi kufanyika mabadiliko ya sheria Bungeni iweje ishindwe kufanya hivyo kwa Mradi wa Bagamoyo? Kwa faida za ajira na kodi zinazokuja na mradi wa Bagamoyo kwa hakika zinazidi faida za mradi wa bomba la mafuta ambalo sehemu kubwa ya ajira zake zitatokea wakati wa ujenzi wa bomba lenyewe na likishakamilika ajira zitapungua kwa 80%.

Ukiachilia faida za moja kwa moja zilizotajwa kuhusu mradi wa Bagamoyo, ni wazi kwamba ujenzi wa mradi huo pia utasaidia kuufanya mradi wa reli ya Kati ya Standard Gauge kupata idadi kubwa ya mizigo ya kusafirisha ili uweze kurejesha mikopo iliyochukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo. Serikali yetu inashindwa kuona fungamanisho hili kati ya Mradi wa Reli ya Kisasa na Mradi wa Bagamoyo SEZ? Kwa ujumla na vyovyote iwavyo, faida za mradi wa Bagamoyo SEZ ni kubwa kuliko madhara tunayodhani tunayaepuka.
Kwa kuwa unakubaliana na hoja ya kuwa mradi huu una masharti magumu, basi hoja ya kwanza iwe ni kufanya majadiriano upya ili kupunguza ugumu wa masharti hayo. Kulinganisha vivutio vilivyotolewa kwa mradi wa bomba la gesi na mradi huu wa Bagamoyo, si hoja nzito hata kidogo.
Nikupe kichekesho kidogo. Wakati tuko vijana, kuna wenzetu walikuwa hawajui kuwasomesha mashairi wasichana ili wawakubali, walikuwa wanasubiri kujua nani kampata msichana fulani, naye anakwenda na gia kwamba mbona fulani umemkubalia kwa nini mimi usinikubalie pia!
Kwa hiyo kama masharti ya Bagamoyo ni magumu, tusiweke mpira kwapani wala tusiende na gia ya bomba la gesi; turudi kwenye meza tuone namna ya kupunguza ugumu wa masharti hayo.
 
Back
Top Bottom