Mradi wa Bandari ya Bagamoyo uliingia laana baada ya wakazi wake kudhulumiwa na EPZ

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
2,209
4,767
Bagamoyo ni Bagamoyo tu na siyo Sehemu nyingine yoyote.

Wazee wa Bagamoyo waliwahi kumzuia Magufuli kupitisha barabara kuu inayoelekea Tanga kutokea Dar isipite mjini kwa sababu barabara hiyo ilitakiwa kwanza, kubomolewa kwa nguzo moja hivi ya kimakumbusho ambayo pia hutumika kwa mambo ya kiutamaduni na vitu vya kizaramo na kikwere. 😂

Wazee wa Kikwere na Kizaramo wakamwambia Magufuli asifanye hivyo bali atafute namna nyingine ya barabara hiyo kupita, ama angani na ama eneo lingine lolote.

Matokeo yake, barabara hiyo, ikachepushwa mbali kabisa na mji wa Bagamoyo mjini, ingawa pia kwa sasa, wapo wanasema maamuzi yao hayakuwa sawa kwa sababu barabara hiyo ingepitia mjini, ingebadilisha hali ya wananchi hapo kwa kufanya biashara n.k.

Tukija kwenye suala la Bandari ya Bagamoyo, iliingia laana ya wenyeji, wengi wa waliokuwa wakikaa katika maeneo ya Zinga, Kiromo na Mbegani, walihamishwa kwenye maeneo hayo kwa malipo kiduchu huku wakitoa maeneo yao makubwa yasiyolingana na fidia hizo.

Inasemekana, maafisa wa kipindi hiko waliokuwa wakisimamia zoezi la fidia kwa wananchi, walikuwa wakiwaandikia cheq wananchi, pindi wanaposaini, baada ya wananchi kusaini kwa malipo waliyoona kwenye cheq, kazi waliyokuwa wakifanya maafisa hao, wanachukua cheq kisha wataongeza sifuri zingine mbele watakazoona wao inafaa, kisha wanachukua wao hizo pesa na wananchi kulipwa kiasi kidoogo huku wao wakijineesha mapesa lukuki bila jasho.

Tangu zoezi hilo kukamilika, wananchi tena wakasikia kwamba, wataletewa mradi wa bandari ambapo mwekezaji atakuchukua kipande cha ardhi ya wanabagamoyo na kuifanya kuwa yake.

Wazee waliguna, walipoguna hakujawahi tena kudhaniwa kama mradi utajengwa Bagamoyo.

Dhuluma hamani, hata Mungu huungana na wanaodhulumiwa!

Wanabagamoyo waombwe radhi na kisha waridhiane nao ili mradi uanzishwe, la sivyo, watatangaza mno habari za mradi na hakutatekelezwa chochote.
 
Inasemekana, maafisa wa kipindi hiko waliokuwa wakisimamia zoezi la fidia kwa wananchi, walikuwa wakiwaandikia cheq wananchi, pindi wanaposaini, baada ya wananchi kusaini kwa malipo waliyoona kwenye cheq, kazi waliyokuwa wakifanya maafisa hao, wanachukua cheq kisha wataongeza sifuri zingine mbele watakazoona wao inafaa, kisha wanachukua wao hizo pesa na wananchi kulipwa kiasi kidoogo huku wao wakijineesha mapesa lukuki bila jasho
 
N

Nasikia mzee na wewe ni miongoni mwa wahenga wasiozoeleka kwenye mambo fulani fulani, na wewe ni mbagamoyo? 🤔
 
Inasemekana, maafisa wa kipindi hiko waliokuwa wakisimamia zoezi la fidia kwa wananchi, walikuwa wakiwaandikia cheq wananchi, pindi wanaposaini, baada ya wananchi kusaini kwa malipo waliyoona kwenye cheq, kazi waliyokuwa wakifanya maafisa hao, wanachukua cheq kisha wataongeza sifuri zingine mbele watakazoona wao inafaa, kisha wanachukua wao hizo pesa na wananchi kulipwa kiasi kidoogo huku wao wakijineesha mapesa lukuki bila jasho
Duh hiyo ilikuwa ni awamu ipi mkuu
 
Inasemekana, maafisa wa kipindi hiko waliokuwa wakisimamia zoezi la fidia kwa wananchi, walikuwa wakiwaandikia cheq wananchi, pindi wanaposaini, baada ya wananchi kusaini kwa malipo waliyoona kwenye cheq, kazi waliyokuwa wakifanya maafisa hao, wanachukua cheq kisha wataongeza sifuri zingine mbele watakazoona wao inafaa, kisha wanachukua wao hizo pesa na wananchi kulipwa kiasi kidoogo huku wao wakijineesha mapesa lukuki bila jasho.
Najua kweli kulikuwa na mambo machafu katika zoezi la ulipaji fidia. Lakini acha kuongeza chumvi unaharibu mada yako. Uliona wapi cheque inaandikwa kwa tarakimu pekee bila maneno?
 
Unasema hivi kwa sababu wewe si mwizi!

Unachokisema hapa, kwa mwizi hakina maana tena
 
Kwa kawaida Cheque huwa inaandikwa amount kwa tarakimu na pia kwa maneno. Hivyo siyo rahisi kuongeza sifuri mbele, bila kubadilisha na amount iliyoandikwa kwa maneno. Hivyo ni rahisi kufuatilia copies za cheque kuona kama maneno pia yalibadilishwa na nani ame sign kuapprove malipo
 
Back
Top Bottom