Serikali kuanza rasmi ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Septemba 2023

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Serikali kupitia mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania TPA itaanza rasmi mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo kuanzia septemba mwaka huu.

Mradi huo mkubwa ni sehemu ya uboreshaji wa sekta ya uchukuzi kwenye eneo la bahari ambao umo katika mpango kazi wa serikali kupitia wizara ya uchukuzi.

Mhandisi Juma Semhando Kijavara ni naibu mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania TPA amewaeleza Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea bandari hiyo kuwa mpango wa ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo utagharibu kiasi cha shilingi trilioni 3.

" Kwakuona na kutambua kuwa bandari ya Dar es Salaam imezidiwa na eneo lake kumalizika mwaka huu wa fedha 2023/2024 tunakwenda kuanza rasmi kujenga Bandari ya Bagamoyo kwa fedha zetu za ndani"
Mhandisi Kijivara amefafanua kuwa bandari ya Bagamoyo itakuwa ya kisasa yenye uwezo wa kupokea meli kubwa za kizazi cha nne kwakuwa itakuwa na kina kikubwa kikubwa kinachotosheleza.

Amesema moja ya changamoto inayopelekea TPA kuanzisha mradi wa bagamoyo ni uhaba wa gati za kushushia mizigo bandari ya Dar es Salaam ambayo inazo gati 12 tu zenye urefu mdogo ukilinganisha na bandari ya Mombasa Kenya yenye gati 26 zenye urefu wa zaidi ya mita 300.

"Tuna changamoto ya bandari ya Dar kimiundombinu na ukubwa wa eneo hivyo lazima tuifikirie sasa Bagamoyo pamoja na kuwa hatujapata mwekezaji lakini tumeona tuanze wenyewe kujenga na mwekezaji atatukuta mbele huko" Alisema Kijavara.

Awali Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Mrisho Selemani aliwaeleza wahariri kuwa Bandari ya Dar ndio mhimili wa uchumi wa nchi hivyo jitihada zinafanywa kufanya maboresho katika kuhudumia meli zinazoingia kushusha na kupakia shehena pamoja na kusimamia mapato.

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wamepata fursa ya kutembelea na kujionea shughuli mbali mbali bandarini hapo.
 
Fedha za Ndani za nini? kama watakapo maliza wanajua wanaenda kuwakabidhi Waarabu-DPW-Wawekezaji?

Kwanini wasiwatumie hao "wenye fedha"waje wawekeze fedha zao wenyewe!

Kizazi kijacho kitakuwa na kazi sana ya kujenga magereza ya hawa Malimbukeni.
 
Fedha za Ndani za nini? kama watakapo maliza wanajua wanaenda kuwakabidhi Waarabu-DPW-Wawekezaji?

Kwanini wasiwatumie hao "wenye fedha"waje wawekeze fedha zao wenyewe!

Kizazi kijacho kitakuwa na kazi sana ya kujenga magereza ya hawa Malimbukeni.
Wakati utafika hata makaburi yao itabidi kuyapiga pingu
 
Wakimaliza ujenzi wampe DP world aendeshe maana wao hawawezi
Kipengele kimewekwa kwenye Mkataba, wakimaliza wanagawiwa. Halafu yanakuja majitu humu wanadai ati "Mwekezaji ana hela" kwanini wasiweke hela zao huko? Tunaacha wawekezaji wetu(uendeshaji) wanakuja na mazingaombwe kwa sababu ya chaguzi tu!
 
Back
Top Bottom