Rais Samia, ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni mtego

Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
783
525
Vile ambavyo serikali ya awamu ya tano iliwaaminisha wananchi kuwa bandari ya Bagamoyo ulikuwa mradi usiotufaa kwa masharti yake, na ikafikia hatua ya kuuita kwamba ni mradi ambao ungekubaliwa na mtu mwendawazimu. Je, serikali imegeuka kuwa mwendawazimu?

Inawezekana maslahi yapo lakini mashaka yakiwa makubwa ni vyema kujiuliza na pengine kuahilisha zoezi. Inawezekana kuna shinikizo la kujenga mradi huo ama kutoka nje au ndani, tafakari kwanza huu ni mtego kwako ukizingatia aliyekataa umefanya naye kazi na ulikuwa mshauri wake.

Madai ya kuanza na pesa ya ndani si wazo baya lakini limepitishwa bungeni? yapo mengi yanayotegemewa na budget hiyo kuanzisha vitu vinavyoweza kusubiri ni kuipa mzigo mzito Nchi ukizigatia tuna miradi mingi iliyoko kwenye utekelezaji tuna madeni ya kututosha tupumue kwanza Bagamoyo itajegwa baadae Tanzania ni yetu wote.
 
DP w wameshachukua ya Dar, kwani hii nchi inazalisha Nini Cha ku export Hadi tuhangaike na bandari ya Bagamoyo? Tanga na Mtwara Kuna siku hakuna meli kabisa bandarini.
 
Vile ambavyo serikali ya awamu ya tano iliwaaminisha wanaNchi kuwa bandari ya Bagamoyo ulikuwa mradi usiotufaa kwa masharti yake, na ikafikia hatua ya kuuita kwamba ni mradi ambao ungekubaliwa na mtu mwendawazimu je serikali imegeuka kuwa mwendawazimu, inawezekana maslahi yapo lakini mashaka yakiwa makubwa ni vyema kujiuliza na pengine kuahilisha zoezi. inawezekana kuna shinikizo la kujenga mradi huo ama kutoka nje au ndani, tafakari kwanza huu ni mtego kwako ukizingatia aliyekataa umefanya naye kazi na ulikuwa mshauri wake. madai ya kuanza na pesa ya ndani si wazo baya lakini limepitishwa bungeni? yapo mengi yanayotegemewa na gudget hiyo kuanzisha vitu vinavyoweza kusubiri ni kuipa mzigo mzito Nchi ukizigatia tuna miradi mingi iliyoko kwenye utekelezaji tuna madeni ya kututosha tupumue kwanza Bagamoyo itajegwa baadae Tanzania ni yetu wote
Tunalipa fadhira ili Bwana yule aamuru fomu iprintiwe moja tuuu!
 
Back
Top Bottom