Mimi naamini Tanzania bado tunawatu wanaofilia kwa kutumia kichwa kama profesa Assad na wengine waitwe watoe maoni yao,siyo tuwaache wanaofikilia kwa kutumia tumbo kama
 
Acha ujuha cc huku Tanga tuko bandarini tunashinda tumelala hakuna mizgo bado huko mtwara nako hali ndo ileile af ijengwe nyingine bagamoyo au unafikili kwa kutumia matako?
MATUSI SI UTANZANIA;
BANDARI TARAJIWA ITATUMIKA ZAIDI KATIKA EXPOTATION INFACT PARAMETOR YA MRADI HUU NI KUBWA MNO MAANA KUNA VIWANDA VITAJENGWA PEMBEZONI VYA UZALISHAJI MALI NA MALI HIYO ITASAFIRISHWA NJE HIVYO HILI JAMBO SIO LA WAGANGA NJAA ISPOKUWA TU LINAHITAJI MIKATABA YA KIZALENDO MIKATABA SAHIHI MIKATABA ITAKAYOKUWA NA MASLAHI NA TAIFA LETU HATUTAKI KUJA KULAANIWA NA WAJUKUU ZETU.
 
Viwanda ni story tu...wazungu wanasema a means to an end...km wangekua wana nia na ujenzi wa viwanda wangekua washaanza kujenga wakati wakisubiri mustakabali wa bandari...
Heb niambie ni viwanda vingapi vya wachina unajua hapa TZ ni vya production na sio assembly line?vingi ni assembly, wanaleta mapipiki yashatengenezwa wao wanafanya kuunga unga then wanauza.
Wajenge viwanda 700 na bidhaa za viwanda vyao kutoka china wakauze wapi?
Wanataka bandari ili iweze kupokea bidhaa kutoka China na sio kusafirisha bidhaa nje zitakazoshindana na wanazozalisha huko kwao.
Unaakili sana big up

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Tunajenga reli ya SGR na bwawa la umeme kwanza,tukikamilisha iyo miradi ndio tuangalie Huo mradi wa bagamoyo tunatoa wap fedha tuujenge wenyewe hata kwa awamu
 
tatizo siyo kujengwa tatizo ule mkataba unasema umiliki wa miaka 99 hapo ndipo palipo na hitilafu kubwa vinginevyo nyie mnaopigia debe mna maslahi yenu makubwa

hakuna mtu atakayekubali huo ukichaa wa miaka 99
 
Tuutafute wote, lakini bado ukweli utabaki kuwa, maradi unafaida kubwa sana suala la masharti linazungumzika mbona kwenye madini tulikaa tukazingumza sasa tunaona faida yake
haya ndio majizi menyewe yanataka kwa nguvu zote yachukue 10% yao
 
1. Faidi kwa wananchi pamoja na bandari kutajengwa viwanda zaidi 700 ambapo kutazalisha ajira zaidi ya 250,000

2. Mwekezaji ndiyo anaweka fedha yake trilioni 23, sisi tunaweka 48b tu za kulipa fidia wananchi

3. Masharti yanazungumzika
hivi kwa akili ndogo tu mimi niweke sh 100 kwenye mtaji halafu wewe uweke sh 1 then mimi ninufaike pakubwa kwenye mradi inakuja akilini kweli yaani bila haya unasema mwekezaji anaweka trilion 20+ hlf tanzania inaweka bilioni 40+ halafu tanzania inufaike upo serious kweli!!!!

ni akili ya mku.....ndu tu ndio inaweza kukubaliana na huo ufala
 
Nikiri kuwa sikusoma hoja zako kwa sababu moja tu unaposema watanzania tunapenda kuwaamini viongozi! Naomba ujue kuwa tunawachagua kwa vile tunawaamini. Sioni sababu yoyote ya Rais aliyekuwepo kusema uwongo! Hoja yake ya kuukataa ilisifika dunia nzima. Leo hii hiyo bandari ikijengwa basi tuiambie dunia kuwa masharti ya mwekezaji yamebadilika vinginevyo kama alivyosema hayati JPM tutakuwa wendawazimu
 
Kwa taarifa za karibuni toka kwa Waziri wa Uchukuzi Engineer Leonard, ambaye sio mchumi kama ZZK, ni kwamba mradi huo sio viable kwani idadi ya mizigo bado ni kidogo, hivyo najiongezea wawekezaji anaweza kukaa miaka 200 badala 99
Aliongea akiwa wapi, lete link
 
Nakubaliana nawe 100%, na hasa tatizo la Ujamaa kwa nchi yetu. Yaani ujamaa ni uovu. Ujamaa umeharibu fikra na uweo (ability) wa ku functiom as normal human beings.
Nachukia umaskini, nachukia ujinga, nachukia ufisadi, nachukia dhuluma na pia nachukia unafiki lakini hivyo vyote viko kwenye furushi la ujamaa. Ujamaa na umaskini + uvivu + ujinga ni kitu kimoja.
Nimetembelea baadhi ya nchi za iliyokuwa Soviet Union, nimeishi na kufanya kazi na watu wenye asili ya kijamaa yaani wanafanana mno. The effect of brainwashed education and mass opiom of silly politics vimewaharibu. Halafu wanajiona wako sawa.

Hawa leo wanaojiita "wanyonge" na eti "wazalendo" ni waganga njaa, wabinafsi na watu wenye chuki tu. Most of them ni "nationalists" not not and never "patriots". There's a vast difference between "Utaifa na "Uzalendo". Utaifa ni uovu uliofungashwa kwa ustadi. Ni hali ya kutaka madaraka na kujinufaisha wao tu. Nationalism ina hila nyingi, ubaguzi, dhuluma na uharibifu. Hao wnaojiita wazalendo ni wasaka madaraka, vyeo, fursa kwa gharama ya wananchi na umoja wa kitaifa. NI waharibifu, wezi na wahuni tu.

Ndio maana mwaka 1967 hayati Mwl alipotangaza ku-Taifi(a)sha (nationalization) mali za watu wenye uwezo (kama hayati Magufuli naye alivyofanya) kwa kigezo cha Utaifa (kipropaganda akakiita uzalendo na eti kulinda mali za nchi) wasio na akili, wenye wivu, "wanyonge" walimuunga mkono. Lakini ile ya Mwl mwaka 1967 ilikuwa dhuluma ya wazi na ina adhabu yake - pengine ndio maana hadi leo watoto wa wale wale "wanyonge" na "makabwela" bado wako kule chini na wanateseka kiuchumi na kifikra. Hawakujifunza makosa ya wazazi wao, nao mwaka 2015 wakamshangilia Mwendazake aliposema "yeye ni Rais wa wanyonge (ubaguzi + kisasi) .....na kuwa atawafanya matajiri kuishi kama mashetani....." Akapora mali na fursa za matajiri.Swali, Je hao wanyonge sasa wanaishi kama malaika? Wamekuwa matajiri? au je sasa hivi wanaishi kama matajiri ? (majibu ya kipuuzi kuwa kuna elimu bure, mashule kujengwa, mahospitali, barabara na reli au kununua ndege - ni majibu ya kukariri na kusadikika sio ya kweli wala halisi). Kwa kila tajiri aliyefilisiwa, nafasi yake wamezaliwa au kutenegenezwa maskini kwa mamia kama sio maelfu. Ile ni sera ovu, katili na mbaya sana kiuchumi. That's idiocy and fallacy is the direct product of Ujamaa and nationalism mantra, respectively. Na huu uporaji na uharibifu wa hayati Magufuli una gharama na watalipa wao na watoto wao - ndivyo ilivyo.
Sababu kubwa ya Magufuli na Mwl Nyerere kupata uungwaji mkono na "wanyonge" ni ujinga na upofu wa fikra. Kwa Magufuli ni Ujinga na Ujamaa. Wajamaa wanachukia utajiri. Wajamaa ni watu waharibifu. Mimi Ronald nawachukia wajamaa, ndio, nauchukia ujamaa damuni!

Uzalendo (patriotisms) ni nini? Upendo na heshima kwa watu/wananchi wenzako (bila ubaguzi) na mapenzi kwa nchi yako.
Tena ni muhimu kujua kwamba uzalendo unajengwa, yaani hauzaliwi au kuzuka tu; na unajengwa kwenye misingi ya haki, ukweli na upendo unaotoakana na ukuombozi wa fikra, na kupevuka kwa jamaa na tamaduni husika. Uzalendo unathamini, kuheshimu, unatetea na kulinda Katiba ya nchi na sheria halali zilizopo; uzalendo unaheshimu na kutukuza mambo ya kweli, yaliyo mema na yenye sifa njema kwa nchi yako, watu wako na familia yako. Uzalendo hauna ubaguzi au ubinafsi. Uzalendo sio itikadi na kuimbishwa nyimbo au kukaririshwa vitu. Uzalendo ni kuwa tayari kwa mambo "ideas/ideology" sio vitu au kuganga njaa na kupewa vyeo. We just need to RESET as a nation.

Moja ya sababu kubwa za mimi kutaka na kutamani katiba mpya ni ili tuzike ujamaa. Kisha tuanze na sera mpya za uzalishaji mali ili kujenga uchumi halisi na sio wa ki propaganda, kama huu uliopo sasa. Uchumi ambao baada ya miaka 60 ya uhuru, Mtanzania kweli atakuwa huru kiuchumi na kifikra na mwenye maisha bora - na sio hizo takwimu zenye kuonyesha maendeleo huku wananchi wengi wakizidi kuzama katika ziwa la umaskini, ujinga, maradhi, siasa chafu na mambo kama hayo.
 
MATUSI SI UTANZANIA;
BANDARI TARAJIWA ITATUMIKA ZAIDI KATIKA EXPOTATION INFACT PARAMETOR YA MRADI HUU NI KUBWA MNO MAANA KUNA VIWANDA VITAJENGWA PEMBEZONI VYA UZALISHAJI MALI NA MALI HIYO ITASAFIRISHWA NJE HIVYO HILI JAMBO SIO LA WAGANGA NJAA ISPOKUWA TU LINAHITAJI MIKATABA YA KIZALENDO MIKATABA SAHIHI MIKATABA ITAKAYOKUWA NA MASLAHI NA TAIFA LETU HATUTAKI KUJA KULAANIWA NA WAJUKUU ZETU.

Stupid
 
MIAKA sita iliyopita, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania ulikuwa ukitajwa kama mmoja wa miradi ya kimkakati yenye fursa kubwa ya kuzimua uchumi wa taifa hilo. Midomoni kwa watumishi wa umma na viongozi wa serikali, neno bandari ya Bagamoyo halikutoka.

Hata hivyo, miaka miwili iliyopita, upepo ukaanza kubadilika. Aliyekuwa Rais waTanzania wakati huo, hayati John Magufuli, alizungumza hadharani kuhusu mradi huo na kusema ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali.

Watanzania ni watu ambao kwa tabia wanapenda kuwaamini viongozi wao. Kauli hiyo kutoka kwa Kiongozi Mkuu wanchi ilizua mkanganyiko miongoni mwa wananchi; wengine wakiamini wale waliosema bandari hiyo ijengwe na wengine wakiamini mradi huo ni wa hovyo.

Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameirithi linapokuja suala la ujenzi wa bandari hiyo. Kwenye kujibu swali kubwa la makala haya, ni muhimu kurudi nyuma kidogo kufahamu kuhusu mradi wenyewe.

Kuhusu mradi wa Bandari Bagamoyo
Kwa sadfa ya kijiografia, Tanzania imejikuta ikiwa nchi yenye bandari katika eneo ambalo wengi wa jirani zake hawana bandari. Miongoni mwa jirani zake nane; Malawi, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia, ni Kenya na Msumbiji pekee ndiyo wenye bahari.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari, Hata hivyo, ingawa huduma za bandari hiyo zinahitajika sana, bandari ya Dar es Salaam- kwa sababu tofauti ikiwamo udogo wa eneo lake na ongezeko la mahitaji ya huduma na teknolojia za kisasa za meli, imeanza kuzidiwa.

Iliyokuwa Mamlaka ya Bandari wakati huo, iliona changamoto hiyo na ndiyo ikapendekeza kujengwa kwa bandari nyingine kubwa zaidi katika eneo la Bagamoyo - umbali wa takribani kilomita 75 tu kutoka Dar es Salaam ili kuendelea kuwa kitovu cha usafiri wa maji katika eneo la Afrika.

Katika kutimiza azma hiyo, Mamlaka ya Bandari ikaja na Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania - ambao, pamoja na mambo mengine, ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022.

Sadfa nyingine ya kijiografia ni kwamba eneo la Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo ambayo China imeyatambua kama ya kimkakati katika Mpango wake Kabambe wa Belt and Road - ambao kimsingi unaunganisha dunia kupitia njia ya maji.

Tanzania iko katika eneo la kimkakati kwa sababu inazungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari, tayari ina reli mbili zinazounganisha na nchi jirani; TAZARA kwa maana ya Zambia na ile ya Kati inayokwenda mpaka Kigoma ambako ni jirani na Congo, Rwanda na Burundi pia.

Kama ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ukikamilika, Tanzania itakuwa na reli ya kisasa ya kusafirisha watu na mizigo kutoka Tanzania kwenda katika nchi jirani kwa haraka.

Kwa hiyo, wakati Tanzania ikipanga kuwa na Bandari ya Bagamoyo kubwa na imara, wawekezaji kutoka China na Oman waliona fursa ya Eneo la Uwekezaji wa Biashara (EPZ) katika mji huo kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Maziwa Makuu kwenda kwingineko duniani.

Faida nyingine ya Bandari ya Bagamoyo ilikuwa kwamba kwa sababu ya ukubwa wake, itakuwa na uwezo wa kupokea mizigo zaidi ya mara 20 ya Bandari ya Dar es Salaam na pia kupokea meli kubwa za kisasa ambao kwa sababu ya ukubwa wake, haziwezi kuja Dar es Salaam.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.

Kupitia mradi wa EPZ, ilielezwa vitafunguliwa zaidi ya viwanda ya 700 na kuajiri takribani watu 250,000 - ukiwamo mradi wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini. Huu ulikuwa uwe mradi mkubwa zaidi katika historia ya Tanzania ambako wawekezaji hao kutoka China, Oman na Korea Kusini wangeingiza nchini mtaji wa zaidi ya dola bilioni 10 (zaidi ya shilingi trilioni 23).

Wawekezaji hao na nchi wanazotoka kwenye mabano ni China Merchants Ports Limited(China), Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), na Science and Technology Policy Institute(STEPI)Korea Kusini.

Hofu ya Mradi wa Bagamoyo
Maneno ya Magufuli yalikuja katika wakati ambao kulikuwa na taarifa nyingi kuhusu namna China inavyotwaa mali zisizohamishika za nchi zilizokopa fedha kutoka kwake na zikashindwa kurejesha kwa wakati. Mifano iliyokuwa ikitolewa sana ilihusu nchi kama Zambia na Sri Lanka.

Katika mkutano wake na wafanyabiashara wa Tanzania, Magufuli alizungumza waziwazi kwamba kwa namna makubaliano yale ya Tanzania na wawekezaji yalivyokuwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi na Tanzania naye asingekubali kuona mradi huo ukiendelea kwa namna hiyo.

"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli.

Spika Job Ndungai aliwahi kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa.

Rais huyo aliyefariki dunia Machi 17 mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu Rais wake, alisema masharti mengine ya kufanyika kwa mradi huo ni kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotakiwa kwenda kukusanya ushuru wala kodi katika eneo hilo, umiliki wa eneo hilo kwa miaka 33 na kufidiwa kwa gharama za uwekezaji wa ujenzi huo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, alizungumza katika nyakati hizo na kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa na hizo ambazo zinaonekana kasoro zinaweza kuzungumzika.

Kuna ukweli kwenye madai ya "mkataba wa hovyo"?
Mmoja wa viongozi wa juu katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete ambao mradi huo ulikuwa unaelekea kukamilika, ameniambia mengi ya yanayoyosemwa kuhusu mradi huo hayana ukweli na kwamba kulikuwa na upotoshaji mkubwa.

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yake, kiongozi huyo alisema gharama pekee kubwa ambayo serikali ingetakiwa kuingia katika mradi huo ni ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa kupisha ujenzi wa bandari hiyo ambao kwa makisio ya mwaka 2016 yalikuwa kiasi cha dola takribani dola milioni 20.9 (shilingi bilioni 43).

" Gharama yetu ni hizo dola milioni 20 za kulipa wananchi lakini mengine yote ni siasa tu. Wanaokuja wanaleta shilingi trilioni 23 na ni uwekezaji wala si mkopo. Ni sawa na kampuni zinazokuja kuchimba madini hapa kwetu. Huwezi kusema wanakuja kutukopesha hela za kuchimba madini. Ni biashara yao.

" Jambo la muhimu kuliko yote ni kwamba huo mpango wa kuwa na Bandari ya Bagamoyo tulikuwa nao hata kabla wawekezaji hawajaja. Na wala hakuna masharti ya kutuzuia kujenga barabara wala miundombinu mingine. Hilo suala la miaka 33 ni la kawaida, yaani mtu aweke shilingi trilioni 23 na halafu asiweke muda wa kurudisha hela zake? Mwisho kabisa, baada ya miaka 33, bandari na hivyo viwanda havitahamishwa Tanzania na nina imani nchi yetu itakuwepo bado," alisema kiongozi huyo.

Huku Lamu, kule Bagamoyo
Kenya, kwa muda mrefu, ilikuwa ikitegemea Bandari ya Mombasa kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo kwa wateja wake wa ndani na katika eneo la maziwa makuu. Kwa sababu ya ongezeko la mahitaji, yenyewe pia ikaamua kujenga Bandari ya Lamu - kwa sababu zilezile ambazo zimeifanya Tanzania kuwa na mpango wa Bagamoyo.

Hadi sasa, nchi hizi mbili zinashindana katika kuhakikisha ipi inakuwa ya kwanza kufanikisha mradi huo ambao unatarajiwa kuleta picha mpya ya ukuaji wa uchumi wa mataifa haya mawili jirani.

Bandari ni mojawapo ya maeneo ambayo yana fursa kubwa katika ukuaji wa uchumi na majirani hawa wote sasa wanatafuta wawekezaji katika miradi ya bandari lakini kwa kuiunganisha na ile ya miundombinu ya reli za kisasa.

Hata hivyo, kwa maana ya ukubwa na umuhimu, mradi wa Bandari ya Bagamoyo una faida kubwa na muhimu zaidi kwa Tanzania kwa sababu ya faida kubwa za viwanda na kilimo zitakazosababishwa moja kwa moja na uwepo wa bandari hiyo.

Rais Samia atafanya nini?
Katika muda wote aliowahi kuwa Makamu wa Rais, Samia hajawahi kutoa kauli yake rasmi kuhusu mradi wa Bagamoyo. Hata hivyo, sasa akiwa Rais, ni wazi washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya sasa.

Akiwa Rais, huenda washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na CCM , watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya sasa.

Dhana ya hofu dhidi ya Wachina ina mashiko miongoni mwa Watanzania wengi na ukweli kwamba hofu hiyo ilitangazwa na Rais Magufuli hadharani na katika namna ambayo ilikuwa rahisi kueleweka kwa Watanzania, inampa Rais Samia fursa ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuondoa mambo ambayo yanaweza kuwa hayana maslahi kwa taifa lake.

Bahati nzuri ambayo Watanzania wanayo kwasasa ni kwamba Samia ana asili ya Zanzibar na anajua nini maana ya bandari - pengine kuliko viongozi waliozaliwa mbali na pwani.
View attachment 1751788View attachment 1751789View attachment 1752847
Wajenge wasijenge mimi na familia yangu hatuna cha kupoteza wala cha kugain.
 
Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo hauepukiki

 
Back
Top Bottom