BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

WANA FORUM TUWE WAUNGWANA NA TUJADILI KISOMI BILA UNAFIKI!!!!!!!!!!!!!!!!

Tuna zaidi ya wiki moja tunajadili suala la sensa na kipengele cha dini. naomba niulize kisha nijibu maswali yafuatayo;

1- Sensa ni nini?
sensa ni zoezi la kuhesabu watu wakazi katika eneo husika likisimamiwa na chombo halali kilicho na dhamana ya kufanya hivyo. Aghalabu, sensa ya kitaifa hufanyika kila baada ya miaka kumi.

2- Lengo la sensa ni nini?
Lengo kuu la sensa ni kujua idadi ya watu kiumri, kijinsia, kimakzi ktk eneo husika, kikazi(ajira) na kidini (hapa ndiyo penye utata)

3-Kipengele cha dini kiliwahi kuwekwa kwenye dodoso ya sensa hapa nchini?
ndiyo. sensa za mwaka 1957 na 1967 zilikua na kipengele cha dini

4-Kipengele hicho cha dini kilichangia kuvunja amani nchini?
hapana hakijawahi kusababisha uvunjifu wa amani kwa kuwekwa kwenye sensa?

5- Kwa nini kiliondolewa? na nani?

sababu hazijulikani lakini nadhani rais wa kwanza alikiondoa ktk dodoso ya sensa ya tatu 1977 kwa kuhofia jambo moja. Sensa zote mbili zilionesha Waislamu ni wengi hapa nchini. hali halisi ikaonesha kuwa Waislamu ni wachache sana katika ajira za sekta ya umma (serikalini). ikumbukwe kuwa Waislamu waliogopa kupeleka watoto wao katika shule za kikoloni (wazungu) wakihofia watabadilishwa dini. hali hii ikafanya idadi ya wasomi waislamu kuwa ndogo. Mwalimu Nyerer hakuzuia Waislamu kusoma. ni khofu wa wazee wenyewe wa Kiislamu. naweza kusema walikosea na kwa upande mwengine walikua sahihi. Vile mwalimu alikua mwana saikolojia, aliona HATARI ya kuwa na watu wengi hapa nchini wenye asilimia kiduchu ktk idara za serikali. JAMBO LA KWANZA, BILA KULISHAURI BUNGE, MWL AKAAGIZA KIMYAKIMYA KIONDOLEWE KIPENGELE CHA DINI KTK SENSA.

simlaumu mwalimu katika hili. ALITAKA KULINDA UMAJO WA NCHI. narudia tena. ni wazee wenyewe wa kiislamu ndiyo walihofia watoto wao kubadilishwa dini wakisomesha ktkt shule za misheni.

kama mnavoelewa, mtu akiwa na cheo ofisini, anapopata habari ya ajira HUMFAHAMISHA NDUGU YAKE AU JAMAA WA KARIBU AU RAFIKI YAKE. bila kutarajiwa, kadri miaka ilivyozidi, wakristo wakawa wameshamiri maofini kwa asilimia kubwa sana. NAMLAUMU BABA WA TAIFIA KWA JAMBO MOJA. baada ya kugundua hatari iliokuepo, angejitahidi kufanya mkakati maalumu wa kuwasomesha waislamu wachache na kuwasimika ktk ajira ya umma ili kulazimisha ongezeko la idadi yao. nadhani hili hakulifanya! hali imeendelea hivyo hadi hii leo.


6-KWA NINI AKINA PONDA WANALALAMIKA?

sasa hivi ukienda kwenye ofisi za serikali kama TRA, VYEO VYA JUU POLISI (kuwepo said mwema juu kabisa siyo kigezo tosha), VYEO VYA JUU JESHINI, WIZARA ZOTE ZA SERIKALI .... nk utakuta ofisi zimekaa kama parokia fulani. wakristo watupu (najua hili kwa wakristo ama hawasilioni au wanaliona na wanalijua). wapo waislamu ambao wamesoma (japo hawajawafikia wakristo) lkn waislamu walio wengi wanapata rizki katika biashara, muziki, mpira, uvuvi, kilimo, umachinga na kazi ngumu kama kusukuma mikokoteni na kubeba mizigo (hawajui wala kunusa WHITE COLAR JOBS). vijana wengi wa kiislamu wnabwiya unga. wanaishia la saba! kaka zao wanashindwa kuwasaidia kwa SABABU HAWAMO SERIKALINI. HAWANA MSHAHARA WA MWISHO WA MWEZI. wasomi waislamu hili wanaliona na wanalijua. AKINA PONDA WANAONA ILI UNFAIR TREATMENT iliyokuepo kipindi cha mwalimu imetapakaa na kukua hadi hii leo. kwa anae jua maana ya govt adminstrtve strcture pamoja na local gvt system, hawezi kuema ooohhh mbona rais na makamu ni waislamu? thats nothing! kwenye wizara na halmashauri nchini waislamu ni chini ya asilimia 9. hawakutaka wenyewe. serikali kama mzazi haikuweka mkakati wa kukosoa kosa lililofanywa na wazee kuogopa shule za kimisheni (sina uhakika kama ni kosa kwa sababu kweli baadhi walibadilishwa au walilazimika kutumia majina ya kikristo ili wakasome. bob makani ni mmoja wao).


7-MADAI YA PONDA NI YAPI?
ponda anasema "enough is enough. tutumie sensa kama gia ili tujue idadi kisha yaje madai ya kuuliza mbona waislamu ni asilimia 35, 40 50 au 55 lakini kwenye ajira asilimia 9!!!!!!!?" NI BOMU AMBALO LIPO NA LITAPASUKA. NATABIRI KUWA kama kipengele cha dini hakitawekwa, waislamu watatafuta haki ya uwiano kiajira kwa njia ambazo zitavunja amani.


USAHURI WANGU
NI wakati muafaka tuache kuweka majivu kwenye moto tukidhani umezimika. UKWELI NI KWAMBA KIJANA WA KIISLAMU ANAPOKWENDA SERIKALINI KUOMBA KAZI, hujihisi kwa anakwenda parokiani. na akitaja jina la kiislamu, huangaliwa na walakini. hili jambo linawasononesha waislamu kuwa hivyo katika nchi yao licha ya kupigania UHURU WA NCHI HII NA KUMPOKEA NYERERE DSM NA KUMKABIDHI TAA KISHA TANU


nimeandika kwa nia njema. nitafurahi nikijibiwa kwa hoja bila ya ushabiki wa kidini wala matusi

E Bana wewe una akili sana! Nafikili hii post yako MODS wataionganisha na main post kule juu.

Asante mwongozo, we ni zaidi ya mwogozo
 
Last edited by a moderator:
Aidha Kipengele cha Freemason kiwekwe pia ili kujua asilimia ya Watanzania ambao ni wanaimani wa dini hiyo
 
MMh! ama kweli ukishangaa ya Firauni utaona ya Ibilisi. Kumbe mnawa-mind waislamu kuwahesabu tu na si kuwapa haki zao mlizowadhulumu tangu 1884 na serikali za Kikoloni za Mfumo Kristo? Tulijua itaghata ndo maana tukasema hatushiriki. Eti mtu anafoka "Sasa hivi tulitakiwa tunaumiza kwa miaka 50 ya uhuru wetu mbona hali inazidi kuwa duni?"
Hali inazidi kuwa mbaya kwa sababu nchi inaoongozwa na wasomi!walioandaliwa na Mfumo Kristo wawe waislamu au wagalatia. Haya ndo matokeo ya dhulma, Seminari Zatamba Tena! Mbona hazioneshi kuikomboa nchi hii bali ufisadi mtupu? Ama sisi tutazidai haki zetu hadi mbele ya Mungu, mtatulipa hapa hapa tuende sambamba au mtalipa kuzimu.
 
watanzania tujikite kwenye issues za kuleta maendeleo ya nchi yetu,nakwambieni leo hii mtume muhammad angelikutana na yesu kristo wangekaa pamoja na kunywa kahawa sasa nyie wabishania nini? idadi ya waumini?? kama ni uisilamu nendeni afriganistan,syria iraq, pakistan n.k

Yesu na Muhammad wangekutana kivipi, kwani wewe hujui Yesu yupo wapi sasa hivi na Muhammad yupo wapi? Ebo!!
 
Twakimu kwa mujibu wa Bakwata zinaonesha idadi ya Waislamu kuwa wengi katika Katika Mikoa ya Pwani ambayo ni Dar es salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara. Kama vip Serikali iruhusu tu hichi kipengele cha Dini kwasababu hakitaniathiri Mimi Raia kutoka Kanda ya Ziwa kwani kwa Idadi yetu na Raslimali tulizonazo tunaweza kuwakabili hawa waislamu wa Pwani kwa mali na Nguvu. Nawatakia kila la Kheri Bakwata kwa Manufaa ya Waarabu ambao nao kwasasa Wanatawaliwa na Mkristo ( Mmarekani) Tehe he he nilikuwa napita tuuuuuuuuuuuu,
 
Kurahisisha harakati zenu unganeni na kikundi cha Uamsho mapema ili muwakomboe na Waislamu wa Dar ambao wanataka kuhamia Zanzibar
MMh! ama kweli ukishangaa ya Firauni utaona ya Ibilisi. Kumbe mnawa-mind waislamu kuwahesabu tu na si kuwapa haki zao mlizowadhulumu tangu 1884 na serikali za Kikoloni za Mfumo Kristo? Tulijua itaghata ndo maana tukasema hatushiriki. Eti mtu anafoka "Sasa hivi tulitakiwa tunaumiza kwa miaka 50 ya uhuru wetu mbona hali inazidi kuwa duni?"
Hali inazidi kuwa mbaya kwa sababu nchi inaoongozwa na wasomi!walioandaliwa na Mfumo Kristo wawe waislamu au wagalatia. Haya ndo matokeo ya dhulma, Seminari Zatamba Tena! Mbona hazioneshi kuikomboa nchi hii bali ufisadi mtupu? Ama sisi tutazidai haki zetu hadi mbele ya Mungu, mtatulipa hapa hapa tuende sambamba au mtalipa kuzimu.
 
Harooo Ntamahoro! Eti "These people are narrow minded", Kweli, are they or are you? You clever people, educated, civilized but drankards, fornicators, corrupt people. The country is under your leadership bro, you clever people. You know sometimes I remember the story of a psychitrist who wanted to find out who, among his patients is cured. He drew an image of a door on the wall using a piece of chalk and commanded the patients " Go out all of you". They began to struggle to open the door but one clever!educated guy like you just stood aside wondering about those opening the imaginery door!!! When asked why he isn't going out? He replied "I am just watching them, they are opening the door while I have the keys!!! The doctor said "I thought you are cured but now I know you are the C-r-a-Z-i-e-S-T".T-he t-he t-hee he he eheeeeee! ndo ninyi wagala. Think you are clever but you are just like that clever guy. We aren't narrow minded buddy, we are oppressed people, exploited people, ensalved people in the slavery of ignorance. You know what, was it not Martin Luther King who said "It is not the evil-doors who are to blame but those who keep quit about the evils". Just opne up your mind, how can a country develop when half of its population is systematically marginalized since colonial time? Do you read history books of rationally minded people or you are aaah busy with safari moja huanzisha nyingine? acheni bwana, mnaimaliz anji hii kwa udini wenu. You always think about Muslims with negativities no positivities because you are selfish, greedy, materialistic, febble-minded aaahh! Inatosha wka leo.
 
Endapo kipengele hicho kitawekwa basi kuna hatari kubwa kwa sensa hii kutokukubaliwa na upande mmoja, endapo upande mwingine wataonekana kuwa wengi; la hasha tunaweza tukajikuta watu wanaenda mahakamani kupinga matokeo ya sensa na kutaka sensa irudiwe.
 
Hawa wenzetu vipi?Tunasoma nao,tunafundishwa na walimu wale wale na kuishi nao mitaa sawa lakini mbona akili zao bado ziko tenge?Baada ya hili la sensa tusishangae wakianza kuomba ruzuku ya kujenga misikiti kutokana na asilimia ya waislamu nchini itakayotokana na matokeo ya sensa!
 
Nchi hii bwana naona Waislam wameamua kutupeleka kule Nigeria ambapo nchi imegawanywa pande mbili. Sasa sijajua Tanzania wakristo wako kanda ipi na Waislam wako kanda ipi.
Wakati watu tunafikiria jinsi ya kuibana serikali ili kupunguza ulafi wa maliasili za nchi na kuongeza kipato kwa mwananchi wa kawaida, kuna viumbe wanafikiria kujua waislam wako wangapi.
Hii sio akili bali ni matope.
Naona hii ndo wanajaribu kuvua magamba ya kondoo waliyokuwa wamevaa miaka yote na sasa tutawajua kwa rangi zao halisi.
 
Binaadam tumeacha kufanya yaliyo ndani ya uwezo wetu, mambo yanayohitaji akili na nguvu zetu katika kupambana na mazira yanayotuzunguka kwa minajiri ya kujipatia maendeleo na sasa tunataka kujivika jukumu ambalo hata tufanye nini hatutaliweza, hivi kwa kufikiri tu...sisi tuna uwezo wa kumtambua ni nani Mkristo na nani Muislam?

Nimeuliza hivyo sababu kufahamu hayo inahitaji uwezo wa kuujua Moyo wa mtu na dhamira ya matendo yake, upo juu ya upeo na uwezo wa mwanadam, labda kama lengo ni kujua wafuasi au watu wenye itikadi za dini.

MAZOEA YANAYOJENGEKA SIKU HIZI.

Kwa nini kila wakati tuishinikize serikali ifanye jambo fulani kwa ajili ya imani zetu? Mbona wakatoliki wao hufanya sensa yao? Kwa nini sisi kama jamii tulazimishwe kwachukulia watu wa imani fulani kama ni Venerable group? Na kwanini wajisikie amani kuwa katika kundi hilo?

Nijuavyo mimi dini si mzigo mdogo au mwepesi kiasi hicho, Dini ni gunia la misumari au kinyesi, pamoja na hayo mshika Dini si mtu wa kulia lia kuomba eti arahisishiwe mambo na mwanadamu mwenzake, mtu wa dini ni mtambuzi wa mazingira anayoyaishi na jukumu kubwa alilo nalo ni kuhakikisha anakuwa mtulivu na matendo yake yanashawishi wengine kuikiri imani yake, na siyo kujaribu kuiinua imani yake kupitia, malalamiko, kulialia, vitisho, hamaki.....hizi kisaikolojia ni dalili za mtu asiyejua anachokiamini bali kiupofu hivyo anajenga defensive mechanism ili asiulizwe maswali ya kimantiki yatakayo mhitaji kujenga hoja.

Namaliza kwa kusema Dini ni Mzigo kama huwezi kuubeba jitoe tu, utakuwa salama zaidi, kama una vikwazo unaviona unasababishiwa kupitia imani, basi mlilie Mungu wako na si mwanadamu.....kwa kuililia serikali kila wakati hapo mnaigeuza serikali Kuwa ndiyo MUngu wenu, mnajidharirisha hapo. Ni wajibu wa dini kuisimamia na kuitetea jamii, kaika hilo mnapaswa kuja na hoja za kidunia zitakazoeleweka na kuwagusa binaadam wa makundi yote bila kujali imani zao.

Excellent...!
 
Kuhesabu waumini ni kazi za madhehebu husika,kama dhehebu flani linataka kujuwa wasiokuwa dhehebu lao ni wangapi,basi wahesabu waumini wao, halafu hiyo namba waiminus kutoka kwenye namba ya sensa ya Taifa.Simple.
 
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

“Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

“Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

“Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

CHANZO: HabariLeo

si wawahesabu wanapoingia mlangoni.
 
Bakwata pia iagizeni Serikali ya JK ifanye sensa pia kwenye chama changu cha CCM kubaini idadi ya Wanachama kwa Dini Zao na kisha CCM isambaratishwe kwa Waislam wote wafukuziwe CUF na Wakristo wafukuziwe Chadema,then tuitishe uchaguzi Mkuu Tanzania tuone wapi wa Tashinda na kutawala Tanganyika. Huo ni mfano tu wa athari zinazoweza kujitokeza kwa waislamu kuendelea kung'ang'ania maswala ya Kidini ilihali wanabebwa sana hapa Tanganyika wangejua Waislam wengi ni majina tu na sio vitendo. huu ulikuwa mfano unaokaribiana na ukweli
Kuna kila dalili kuwa tunakoelekea ni kubaya chokochoko zimeanza yangu macho!..
 
Binaadam tumeacha kufanya yaliyo ndani ya uwezo wetu, mambo yanayohitaji akili na nguvu zetu katika kupambana na mazira yanayotuzunguka kwa minajiri ya kujipatia maendeleo na sasa tunataka kujivika jukumu ambalo hata tufanye nini hatutaliweza, hivi kwa kufikiri tu...sisi tuna uwezo wa kumtambua ni nani Mkristo na nani Muislam?

Nimeuliza hivyo sababu kufahamu hayo inahitaji uwezo wa kuujua Moyo wa mtu na dhamira ya matendo yake, upo juu ya upeo na uwezo wa mwanadam, labda kama lengo ni kujua wafuasi au watu wenye itikadi za dini.

MAZOEA YANAYOJENGEKA SIKU HIZI.

Kwa nini kila wakati tuishinikize serikali ifanye jambo fulani kwa ajili ya imani zetu? Mbona wakatoliki wao hufanya sensa yao? Kwa nini sisi kama jamii tulazimishwe kwachukulia watu wa imani fulani kama ni Venerable group? Na kwanini wajisikie amani kuwa katika kundi hilo?

Nijuavyo mimi dini si mzigo mdogo au mwepesi kiasi hicho, Dini ni gunia la misumari au kinyesi, pamoja na hayo mshika Dini si mtu wa kulia lia kuomba eti arahisishiwe mambo na mwanadamu mwenzake, mtu wa dini ni mtambuzi wa mazingira anayoyaishi na jukumu kubwa alilo nalo ni kuhakikisha anakuwa mtulivu na matendo yake yanashawishi wengine kuikiri imani yake, na siyo kujaribu kuiinua imani yake kupitia, malalamiko, kulialia, vitisho, hamaki.....hizi kisaikolojia ni dalili za mtu asiyejua anachokiamini bali kiupofu hivyo anajenga defensive mechanism ili asiulizwe maswali ya kimantiki yatakayo mhitaji kujenga hoja.

Namaliza kwa kusema Dini ni Mzigo kama huwezi kuubeba jitoe tu, utakuwa salama zaidi, kama una vikwazo unaviona unasababishiwa kupitia imani, basi mlilie Mungu wako na si mwanadamu.....kwa kuililia serikali kila wakati hapo mnaigeuza serikali Kuwa ndiyo MUngu wenu, mnajidharirisha hapo. Ni wajibu wa dini kuisimamia na kuitetea jamii, kaika hilo mnapaswa kuja na hoja za kidunia zitakazoeleweka na kuwagusa binaadam wa makundi yote bila kujali imani zao.
@Consigliere,serikali siyo Mungu,lakini serikali inawajibu ambao siyo wa kiimani,serikali ni lazima iwajibike kwa wananchi wake.
 
Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.

We kilaza kweli hivi Israel na Misri unaona kuko shwari huko?udini ndo unaowatafuna ss na watamalizana wenyewe kwa wenyewe,think out of box
 
Naona uamsho wamewadanganya mmesikiliza cd yao mkaona ndiyo nitoke vipi yenu.Hilo halitakubalika na wala halitatokea ndiyo maana mnaongea nyinyi kina Pengo, Malasusa na wengine wamekaa kimya wanajua na threat at all.Mchana mtaongea usiku mtalala


Hao ulio wataja, hawako kimya mbona wanasema kupitia kwa hiyo tume ya sensa na takwimu wakiongozwa na serikali yao kupitia kwa wasira...we! vipi? hawako kimya..wanaendesha kwa remote control mambo yote haya...chezea kanisa wewe? Kalagabaho
 
Kwani hata waislamu wangekuwa 99% ina implication gani kwa maendeleo ya taifa? Itasaidia kujenga shule zaidi, hospitali, maji safi, barabara umeme, n.k?

Mbona watanzania mnaacha kufuatilia na kushuguligikia mambo ya maana mnakeshea ujinga? Sasa hivi tulitakiwa tunaumiza kwa miaka 50 ya uhuru wetu mbona hali inazidi kuwa duni? Kwa rasilimali tulizo nazo madini, ardhi, watu, maji, bahari, milima mbuga za wanyama, amani, maziwa, mito hali nzuri ya hewa mbona umaskini unatumaliza! Mnakalia kutokwa mishipa ya shingo kutaka kujua waislamu na wakristu wepi wengi!! Au mnataka kutangaza taifa la kiislamu muwafukuze wakristu?

Mtanzania amka, umaskini, magonjwa, ujinga havichagui dini hata mnekuwa waislamu peke yenu isingewasaidia!!
Binafsi nilikwishaacha kujadili ishu za kidini hazina tija kwa taifa hili usipoteze muda kubishana nazo mkuu, umecomment poa sana tu big up.
 
Waislamu wanaumwa....mara zote uwa nasema naiheshimu sana dini ya Kiislamu, ila nawadharau na kuwachukia sana waislamu. Hasa hawa wenye njaa chini ya CCM D aka BAKWATA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom