BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.
Uingereza ni nchi ya Anglikani
Misiri ni nchi ya Kiislamu
Israel ni nchi ya Kiyahudi

Tanzania ni nchi ya imani gani?.
 
Hapo tatizo ni nini? Ni kufahamu Idadi ya Waislam? Waislamu wepi? Suni, Shia au Ansalisunna? Ushauri wangu kuhusu hilo, waislam wajipange na wajihesabu. Inamaana waislam hawana mfumo wa kuhesabiana? Mnaweza kuomba ushauri kwani ni kweli huenda mpo wengi sana japo wengi wenu hautasaidia kama kila mmoja hatafanya kazi wala kusomesha watoto na kushirikiana kitaifa na kimataifa.
 
Baada ya kujua idadi ya wana imani fulan!, nini kitafata?

Kwetu wafuasi wa dini za asili itatusaidia kutafuta mbinu za kuzaana sana: tutaongeza idadi ya wanawake, tutaomba msaada kwa wanasayansi watusaidie kupata dawa ya kuwafanya wanawake wazae hata kama wamekoma kuona hedhi, tutakuwa na uhakika wa kupata raisi wa nchi hii kutoka kwenye kundi letu, tutaanzisha....naota mchana eti! Ngoja niende kwenye kijiwe cha gahawa naweza kupata point zingine.

Wasiosoma ni chakula cha waliosoma- by one of jf members.
 
Maamuzi ya kupinga sensa? Itakuwa ni ujinga usiopingika kama unakuwa ni mnafiki wa mambo yenye maendelea bila sababu yeyote ya msingi ntashindwa hata kuwashangaa na hata wewe unaewasapot

Wewe ni great thinker, soma vizuri between the lines sio unakurupuka, wamesema kama haitawekwa kipengele cha dini watakataza watu wao wasishiriki na hili limetokana na WAKATOLIKI kutoa takwimu zao kuwa wakirisito wako wengi zaidi ya waislmu WANAULIZA NA WEWE JIULIZE usiwe mshabiki tu kwa kuwa si muislamu, WAPI WAMEPATA TAKWIMU HIZO? na KWANINI WATOE TAWKIMU ZA DINI? jibu ni kwa sababu wanataka kujustify kuwa tofauti ya waajiriwa serikalini ambayo inaonesha wakirisito wapo wengi ni kwa sababu hata hesabu inaonesha kuwa waislamu wachache nchini! HILO HALIKUBALIKI, watuelze WAPI WAMEPATA HIZO TAKWIMU, na kuondoa wasiwasi huo basi sensa iweke hicho kipengele KWANINI MNAOGOPA?
 
Naomba uniwekee hizo takwimu zilizotolewa na wakatoliki hapa.
 
Hapo tatizo ni nini? Ni kufahamu Idadi ya Waislam? Waislamu wepi? Suni, Shia au Ansalisunna? Ushauri wangu kuhusu hilo, waislam wajipange na wajihesabu. Inamaana waislam hawana mfumo wa kuhesabiana? Mnaweza kuomba ushauri kwani ni kweli huenda mpo wengi sana japo wengi wenu hautasaidia kama kila mmoja hatafanya kazi wala kusomesha watoto na kushirikiana kitaifa na kimataifa.

Maneno hayo! Ukijifunza kuukubali ukweli hata kama unakuumiza basi wewe ni MTU HURU!
 
Nakumbuka sensa iliyopita kuna jamii ya watu waligoma kuhesabiwa na wakamwambia mkuu wa mkoa kuwa ili wahesabiwe ni lazima kwanza wapelekewe nyama ya pundamilia na gunia tatu za bange,kwa mtazamo wangu angalau naona walikuwa na madai ya msingi kulikn hawa wanaogoma sasa!

Jamani dini zingine! Kweli ni janga la dunia.nashauri wale wote wanaoshawishi watu kupinga mipango halali ya serikari sheria ichukue mkondo wake ,serikali amka acha kulala nchi hii inasambaratika.
 
Baada ya kutafakari kwa muda sasa nimeona nitoe maoni yangu ya kuunga mkono matakwa ya BAKWATA kutaka udini uwemo katika zoezi la sensa. Hoja hii ni ya msingi kabisa kwa maendeleo ya taifa letu na hasa kwa lengo la kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Pamoja na kuukubali msimamo huo, nina masharti machache yatakayo ambatana na kuingizwa kwa huo udini kwenye sensa:

1. Sambamba na udini, kuwepo na kipengele cha kiwango cha elimu cha mtu na mahali alikosomea

2. Kuwepo na kipengele cha miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii iliyotekelezwa na taasisi zisizo za serikali mf. maji, afya kuona kama ni wangapi wananufaika nayo.

Mambo haya ninaamini yatakuwa kumbukumbu nzuri sana kwa vizazi zijavyo. :A S 101:
 
Usitake kuwasemea Waislam hujui chochote kuhusu Uislam mkuu nani kakwambia ndoa za Waislam lazima zifungishwe na Sheikh? Kwa taarifa yako hata kama wewe ni Muislam mtoto wako anaolewa hunaweza kufungisha hiyo ndoa...halafu hakuna sehemu yoyote Waislam wamesema wao ni wengi wanachokiomba wanataka kujua wapo wangapi ili iwe rahisi kwao kupanga mambo yao wameomba kama raia.

Hivi Bakwata wakihitaji kujua idadi ya waislamu kupitia misikitini hawatapata idadi inayotakiwa? Kwa akili ya kawaida kabisa mtu ungefikiri kuwa kuhesabu waumini eneo la ibada ndio njia sahihi ya kupata idadi ya waumini halisi kuliko kwenda mitaani ambako uwezekano wa kukutana na waumini jina ni mkubwa mno!
 
Waislam jihesabuni wenyewe muwe na sensa yenu mkae nayo kichwani kwenu iwasaidie kwa imani ya dini yenu, acheni kusumbua watu. Mlitaka mahakama ya kadhi mkaambiwa anzisheni cjui mmefikia wapi, sasa mmeibuka na sensa, jihesabuni wenyewe iwasaidie wenyewe hii ya Sensa ya Serikali ni kwa taifa zima wenye dini na wasiokuwa na dini
 
WANA FORUM TUWE WAUNGWANA NA TUJADILI KISOMI BILA UNAFIKI!!!!!!!!!!!!!!!!

Tuna zaidi ya wiki moja tunajadili suala la sensa na kipengele cha dini. naomba niulize kisha nijibu maswali yafuatayo;

1- Sensa ni nini?
sensa ni zoezi la kuhesabu watu wakazi katika eneo husika likisimamiwa na chombo halali kilicho na dhamana ya kufanya hivyo. Aghalabu, sensa ya kitaifa hufanyika kila baada ya miaka kumi.

2- Lengo la sensa ni nini?
Lengo kuu la sensa ni kujua idadi ya watu kiumri, kijinsia, kimakzi ktk eneo husika, kikazi(ajira) na kidini (hapa ndiyo penye utata)

3-Kipengele cha dini kiliwahi kuwekwa kwenye dodoso ya sensa hapa nchini?
ndiyo. sensa za mwaka 1957 na 1967 zilikua na kipengele cha dini

4-Kipengele hicho cha dini kilichangia kuvunja amani nchini?
hapana hakijawahi kusababisha uvunjifu wa amani kwa kuwekwa kwenye sensa?

5- Kwa nini kiliondolewa? na nani?

sababu hazijulikani lakini nadhani rais wa kwanza alikiondoa ktk dodoso ya sensa ya tatu 1977 kwa kuhofia jambo moja. Sensa zote mbili zilionesha Waislamu ni wengi hapa nchini. hali halisi ikaonesha kuwa Waislamu ni wachache sana katika ajira za sekta ya umma (serikalini). ikumbukwe kuwa Waislamu waliogopa kupeleka watoto wao katika shule za kikoloni (wazungu) wakihofia watabadilishwa dini. hali hii ikafanya idadi ya wasomi waislamu kuwa ndogo. Mwalimu Nyerer hakuzuia Waislamu kusoma. ni khofu wa wazee wenyewe wa Kiislamu. naweza kusema walikosea na kwa upande mwengine walikua sahihi. Vile mwalimu alikua mwana saikolojia, aliona HATARI ya kuwa na watu wengi hapa nchini wenye asilimia kiduchu ktk idara za serikali. JAMBO LA KWANZA, BILA KULISHAURI BUNGE, MWL AKAAGIZA KIMYAKIMYA KIONDOLEWE KIPENGELE CHA DINI KTK SENSA.

simlaumu mwalimu katika hili. ALITAKA KULINDA UMAJO WA NCHI. narudia tena. ni wazee wenyewe wa kiislamu ndiyo walihofia watoto wao kubadilishwa dini wakisomesha ktkt shule za misheni.

kama mnavoelewa, mtu akiwa na cheo ofisini, anapopata habari ya ajira HUMFAHAMISHA NDUGU YAKE AU JAMAA WA KARIBU AU RAFIKI YAKE. bila kutarajiwa, kadri miaka ilivyozidi, wakristo wakawa wameshamiri maofini kwa asilimia kubwa sana. NAMLAUMU BABA WA TAIFIA KWA JAMBO MOJA. baada ya kugundua hatari iliokuepo, angejitahidi kufanya mkakati maalumu wa kuwasomesha waislamu wachache na kuwasimika ktk ajira ya umma ili kulazimisha ongezeko la idadi yao. nadhani hili hakulifanya! hali imeendelea hivyo hadi hii leo.

6-KWA NINI AKINA PONDA WANALALAMIKA?

sasa hivi ukienda kwenye ofisi za serikali kama TRA, VYEO VYA JUU POLISI (kuwepo said mwema juu kabisa siyo kigezo tosha), VYEO VYA JUU JESHINI, WIZARA ZOTE ZA SERIKALI .... nk utakuta ofisi zimekaa kama parokia fulani. wakristo watupu (najua hili kwa wakristo ama hawasilioni au wanaliona na wanalijua). wapo waislamu ambao wamesoma (japo hawajawafikia wakristo) lkn waislamu walio wengi wanapata rizki katika biashara, muziki, mpira, uvuvi, kilimo, umachinga na kazi ngumu kama kusukuma mikokoteni na kubeba mizigo (hawajui wala kunusa WHITE COLAR JOBS). vijana wengi wa kiislamu wnabwiya unga. wanaishia la saba! kaka zao wanashindwa kuwasaidia kwa SABABU HAWAMO SERIKALINI. HAWANA MSHAHARA WA MWISHO WA MWEZI. wasomi waislamu hili wanaliona na wanalijua. AKINA PONDA WANAONA ILI UNFAIR TREATMENT iliyokuepo kipindi cha mwalimu imetapakaa na kukua hadi hii leo. kwa anae jua maana ya govt adminstrtve strcture pamoja na local gvt system, hawezi kuema ooohhh mbona rais na makamu ni waislamu? thats nothing! kwenye wizara na halmashauri nchini waislamu ni chini ya asilimia 9. hawakutaka wenyewe. serikali kama mzazi haikuweka mkakati wa kukosoa kosa lililofanywa na wazee kuogopa shule za kimisheni (sina uhakika kama ni kosa kwa sababu kweli baadhi walibadilishwa au walilazimika kutumia majina ya kikristo ili wakasome. bob makani ni mmoja wao).

7-MADAI YA PONDA NI YAPI?
ponda anasema "enough is enough. tutumie sensa kama gia ili tujue idadi kisha yaje madai ya kuuliza mbona waislamu ni asilimia 35, 40 50 au 55 lakini kwenye ajira asilimia 9!!!!!!!?" NI BOMU AMBALO LIPO NA LITAPASUKA. NATABIRI KUWA kama kipengele cha dini hakitawekwa, waislamu watatafuta haki ya uwiano kiajira kwa njia ambazo zitavunja amani.

USAHURI WANGU
NI wakati muafaka tuache kuweka majivu kwenye moto tukidhani umezimika. UKWELI NI KWAMBA KIJANA WA KIISLAMU ANAPOKWENDA SERIKALINI KUOMBA KAZI, hujihisi kwa anakwenda parokiani. na akitaja jina la kiislamu, huangaliwa na walakini. hili jambo linawasononesha waislamu kuwa hivyo katika nchi yao licha ya kupigania UHURU WA NCHI HII NA KUMPOKEA NYERERE DSM NA KUMKABIDHI TAA KISHA TANU

nimeandika kwa nia njema. nitafurahi nikijibiwa kwa hoja bila ya ushabiki wa kidini wala matusi
 
Baada ya kutafakari kwa muda sasa nimeona nitoe maoni yangu ya kuunga mkono matakwa ya BAKWATA kutaka udini uwemo katika zoezi la sensa. Hoja hii ni ya msingi kabisa kwa maendeleo ya taifa letu na hasa kwa lengo la kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Pamoja na kuukubali msimamo huo, nina masharti machache yatakayo ambatana na kuingizwa kwa huo udini kwenye sensa:

1. Sambamba na udini, kuwepo na kipengele cha kiwango cha elimu cha mtu na mahali alikosomea

2. Kuwepo na kipengele cha miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii iliyotekelezwa na taasisi zisizo za serikali mf. maji, afya kuona kama ni wangapi wananufaika nayo.

Mambo haya ninaamini yatakuwa kumbukumbu nzuri sana kwa vizazi zijavyo. :A S 101:

Samahani mkuu, please justify your assertions in red fonts, ni nini msingi na kwa jinsi gani udini utakavyochangia maendeleo ya taifa letu.
 
..mtaa ninao kaa kuna jamaa kaoa mke muislam..kambadili dini..na kawa mkristo na huyo dada kafunga ndoa kanisani pale st peter..ila jina lake limebaki la kiislam...huyu katika hiyo sensa unamuhesabu dini gani..ikiwa jina la kwenye vywti ni Aisha..lkn kabatizwa na anasali kanisani kwa jina la Irene...

...pia angalia mafundisho mengi siku hizi( kwa wakatoliki)..kuna waislamu wengi tu wako na wote hao wanabadili dini na kuwa wakristo..ila watabaki na majina yao yale yale ya zamani kiislamu..lkn anaingia msikitini...

ndugu zangu waislamu inabidi mjipange..maana hawa akina kakobe wamewasilimisha wengi kweli kweli...

..ni maoni na mtazamo wangu..
 
Kikwete atachoka mwaka huu.Ni bora awe anaenda zake kubembea Jamaica na kumuona 50 cents kila baada ya mwezi maana hii nchi kila siku watu wanalete tu matatizo na kumpa stress.Sema nashukuru rais ni muislamu atajua jinsi ya kudeal nao.naogopa ban ningeongea ukweli mwingine ambao ungeudhi watu.Ngoja na mimi nitoe takwimu zangu nasikia na sisi wakatoliki ni asilimia 38 Tanzania .hahaha.mtajibeba mwaka huu.
 
Wewe shida yako nini? Mbona nyie mna TAG, Catholics, Lutheran and etc hamsemi? Hakuna kinachogawanyika huu ni upumbavu kwasababu suala la dini ya mtu lina umuhimu katika mipango miji ya nchi. Mfano Uingereza hamuwezi tu kujenga msikiti au kanisa hadi upewe kibali na halmashauri ya jiji. Sasa unadhani kwanini wamesisitiza halmashauri ndio zitoe vibali? Tatizo lenu mnasumbuliwa na UDINI TU!!!! Suala la dini lina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu . Dini itatusaidi kujua yafuatayo nawaelekezi nchi vihiyo wa udini:-
a. Tufahamu katika kila eneo ni nyumba za ibada ngapi zijengwe (misikiti, makanisa au masinagogi) na vile vile maeneo ya kuzikana yatengwe kiasi gani yaani makaburi. Hivyo basi dini itatusaidia katika mipango miji nchini mwetu.

b. Tufahamu sababu za kurudi nyuma kimaendeleo (mfano waislamu) je imesababishwa na wao wenyewe? taasisi au mfumo mbovu uliopo?

c. Tufahamu mfumo wa nchi kiutendaji unakuwaje tukijumuisha na imani za watu kama sehemu ya maisha yao mfano ni likizo ngapi ziwepo katika nchi kama sikukuu za mapumziko. Uingereza mfano au Marekani hawana kitu kinaitwa public holiday for Eid but wana public holiday for Christmas, New Year, St. Patricks etc. Saudi Arabia, UAE, na Oman hawana sikukuu za Christmas and New Year. Ni kwasababu ya sensa wameona hakuna umuhimu wa kupumzika siku hizo. Sasa taarifa hizo hakuna mahali zinatoka zaidi ya katika sensa ILIYOANDALIWA NA SERIKALI YA MLIPA KODI!!!!

d. Kufahamu pia usambazi wa vyakula nchini. Mfano waislamu wana mwezi mtukufu wa ramadhani na huwa wanatumia vyakula vya aina fulani nchini. Vile vile wakristo wana Kwaresma huwa pengine wanatumia vyakula vya aina fulani. Hatuwezi kufahamu hilo bila ya kuwepo takwimu sahihi.

Hembu nipeni nyie sababu za msingi kisiwepo kipengele cha dini zaidi ya fear zilizogubikwa na imani za ubaguzi wa kidini???

Yani misikiti hujengwa na halmashauri? Chakula kinalimwa na serikali ili wawape wakati wa ramadan? Hebu kuweni na akili, waislam yani mnakuwa na mambo kama ya watoto! Au mke mdogo! Kila siku malalamiko dah! Haya wakristo tutachanga pesa tuwaletee mihogo na tende wakati mnashinda njaa mchana maana usiku mzima mnakula kama mchwa!
 
kama tumeweza kuondoa kipengele cha dini ya mtu kwenye sensa, tuende mbali zaidi kwa kufanya na yafuatayo:
-biblia na quran viondolewe pale ikulu yetu kwenye shughuli zote za kiserikali;
-biblia na quran viondolewe pia kwenye shughuli za bunge na mahakama zetu;
-mavazi na alama zote za kidini ziondolewe kwenye shule, vyuo na ofisi za serikali na za umma;
-viongozi wetu wa serikali na dola wasiende kwenye hafla za kidini na nyadhifa zao.
Tumekuwa na dini muda wote wa uhai wetu kama taifa. Ufisadi uko palepale; uzinzi uko palepale; maovu yote tunayo tu. Masuala ya dini tumwachie mtu na mungu wake.

u r appreciated
hii ndio njia sahihi
 
WANA FORUM TUWE WAUNGWANA NA TUJADILI KISOMI BILA UNAFIKI!!!!!!!!!!!!!!!!

Tuna zaidi ya wiki moja tunajadili suala la sensa na kipengele cha dini. naomba niulize kisha nijibu maswali yafuatayo;

1- Sensa ni nini?
sensa ni zoezi la kuhesabu watu wakazi katika eneo husika likisimamiwa na chombo halali kilicho na dhamana ya kufanya hivyo. Aghalabu, sensa ya kitaifa hufanyika kila baada ya miaka kumi.

2- Lengo la sensa ni nini?
Lengo kuu la sensa ni kujua idadi ya watu kiumri, kijinsia, kimakzi ktk eneo husika, kikazi(ajira) na kidini (hapa ndiyo penye utata)

3-Kipengele cha dini kiliwahi kuwekwa kwenye dodoso ya sensa hapa nchini?
ndiyo. sensa za mwaka 1957 na 1967 zilikua na kipengele cha dini

4-Kipengele hicho cha dini kilichangia kuvunja amani nchini?
hapana hakijawahi kusababisha uvunjifu wa amani kwa kuwekwa kwenye sensa?

5- Kwa nini kiliondolewa? na nani?

sababu hazijulikani lakini nadhani rais wa kwanza alikiondoa ktk dodoso ya sensa ya tatu 1977 kwa kuhofia jambo moja. Sensa zote mbili zilionesha Waislamu ni wengi hapa nchini. hali halisi ikaonesha kuwa Waislamu ni wachache sana katika ajira za sekta ya umma (serikalini). ikumbukwe kuwa Waislamu waliogopa kupeleka watoto wao katika shule za kikoloni (wazungu) wakihofia watabadilishwa dini. hali hii ikafanya idadi ya wasomi waislamu kuwa ndogo. Mwalimu Nyerer hakuzuia Waislamu kusoma. ni khofu wa wazee wenyewe wa Kiislamu. naweza kusema walikosea na kwa upande mwengine walikua sahihi. Vile mwalimu alikua mwana saikolojia, aliona HATARI ya kuwa na watu wengi hapa nchini wenye asilimia kiduchu ktk idara za serikali. JAMBO LA KWANZA, BILA KULISHAURI BUNGE, MWL AKAAGIZA KIMYAKIMYA KIONDOLEWE KIPENGELE CHA DINI KTK SENSA.

simlaumu mwalimu katika hili. ALITAKA KULINDA UMAJO WA NCHI. narudia tena. ni wazee wenyewe wa kiislamu ndiyo walihofia watoto wao kubadilishwa dini wakisomesha ktkt shule za misheni.

kama mnavoelewa, mtu akiwa na cheo ofisini, anapopata habari ya ajira HUMFAHAMISHA NDUGU YAKE AU JAMAA WA KARIBU AU RAFIKI YAKE. bila kutarajiwa, kadri miaka ilivyozidi, wakristo wakawa wameshamiri maofini kwa asilimia kubwa sana. NAMLAUMU BABA WA TAIFIA KWA JAMBO MOJA. baada ya kugundua hatari iliokuepo, angejitahidi kufanya mkakati maalumu wa kuwasomesha waislamu wachache na kuwasimika ktk ajira ya umma ili kulazimisha ongezeko la idadi yao. nadhani hili hakulifanya! hali imeendelea hivyo hadi hii leo.

6-KWA NINI AKINA PONDA WANALALAMIKA?

sasa hivi ukienda kwenye ofisi za serikali kama TRA, VYEO VYA JUU POLISI (kuwepo said mwema juu kabisa siyo kigezo tosha), VYEO VYA JUU JESHINI, WIZARA ZOTE ZA SERIKALI .... nk utakuta ofisi zimekaa kama parokia fulani. wakristo watupu (najua hili kwa wakristo ama hawasilioni au wanaliona na wanalijua). wapo waislamu ambao wamesoma (japo hawajawafikia wakristo) lkn waislamu walio wengi wanapata rizki katika biashara, muziki, mpira, uvuvi, kilimo, umachinga na kazi ngumu kama kusukuma mikokoteni na kubeba mizigo (hawajui wala kunusa WHITE COLAR JOBS). vijana wengi wa kiislamu wnabwiya unga. wanaishia la saba! kaka zao wanashindwa kuwasaidia kwa SABABU HAWAMO SERIKALINI. HAWANA MSHAHARA WA MWISHO WA MWEZI. wasomi waislamu hili wanaliona na wanalijua. AKINA PONDA WANAONA ILI UNFAIR TREATMENT iliyokuepo kipindi cha mwalimu imetapakaa na kukua hadi hii leo. kwa anae jua maana ya govt adminstrtve strcture pamoja na local gvt system, hawezi kuema ooohhh mbona rais na makamu ni waislamu? thats nothing! kwenye wizara na halmashauri nchini waislamu ni chini ya asilimia 9. hawakutaka wenyewe. serikali kama mzazi haikuweka mkakati wa kukosoa kosa lililofanywa na wazee kuogopa shule za kimisheni (sina uhakika kama ni kosa kwa sababu kweli baadhi walibadilishwa au walilazimika kutumia majina ya kikristo ili wakasome. bob makani ni mmoja wao).

7-MADAI YA PONDA NI YAPI?
ponda anasema "enough is enough. tutumie sensa kama gia ili tujue idadi kisha yaje madai ya kuuliza mbona waislamu ni asilimia 35, 40 50 au 55 lakini kwenye ajira asilimia 9!!!!!!!?" NI BOMU AMBALO LIPO NA LITAPASUKA. NATABIRI KUWA kama kipengele cha dini hakitawekwa, waislamu watatafuta haki ya uwiano kiajira kwa njia ambazo zitavunja amani.

USAHURI WANGU
NI wakati muafaka tuache kuweka majivu kwenye moto tukidhani umezimika. UKWELI NI KWAMBA KIJANA WA KIISLAMU ANAPOKWENDA SERIKALINI KUOMBA KAZI, hujihisi kwa anakwenda parokiani. na akitaja jina la kiislamu, huangaliwa na walakini. hili jambo linawasononesha waislamu kuwa hivyo katika nchi yao licha ya kupigania UHURU WA NCHI HII NA KUMPOKEA NYERERE DSM NA KUMKABIDHI TAA KISHA TANU

nimeandika kwa nia njema. nitafurahi nikijibiwa kwa hoja bila ya ushabiki wa kidini wala matusi

Safi sana nasubiri hoja za msingi against kuweka kipengele cha dini. Ninachokiona ni kejeli na enough is enough nimewaambia THE SLEEPING GIANT IS AWAKENING. Muda wa kuwaona waislamu ni just waswahili umeisha it is about time tuwe tunaheshimiana na kufahamishana hamna kengine.
 
1. Aise wakati mwingine huwa naionea huruma serikali ya JK. Yaani kuna vi-issue vingi kweli vya kushughulikia aisee.

2. Ulegevu wa serikali ya CCM utafanya rais ajaye awe na wakati mgumu sana kuweka mambo sawa. Maana serikali inanywea kwenye mambo fulani yasiyo ya msingi kwa msukumo wa watu fulani. Sitashangaa kama serikali ikinywea kwenye issue hii. Simwoni mtu anayeweza ku-handle hii issue kwa hekima (ktk serikali) na ikaisha vizuri na sensa ikaendelea kama ilivyokusudiwa.

3. Hata kama serikali ikinywea na kukiingiza kipingili cha dini (nimesema sitashangaa) takwimu zikionyesha waislamu ni wachache kuliko wakristo, utasikia tena issue nyingine. Watasema takwimu zimepikwa maana wao wanajua wako wengi (ingawa hawana basis yeyote ya kuamini hivyo) na wanataka serikali (kupitia sensa) iwasaidie kuthibitisha wanachoamini.

4. Serikali ikinywea na kuweka kipengele cha dini madhara yake yanaweza kuwa makubwa kama ikitokea idadi ya waislamu ikawa ndogo kuliko wanavyodhani viongozi wao. For some reasons ni rahisi kuwa-mobilise waislamu kufanya fujo kuliko kuwa-mobilize wakristo kufanya fujo (huu ni ukweli mchungu). Historia imelithibitisha hili.
 
Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.

Dini itatusaidiaje katika kuleta maendeleo? Justify
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom