Wanafunzi zaidi ya million 8 wako mashuleni wakati wake. Kabla yake chini ya million 4
Umewahi kujiuliza wakati Tanganyika inapata uhuru wake 1961 tulikuwa wangapi ukipata jibu jiulize Nyerere alitaifisha shule ngapi ili kuwawezesha wanafunzi wote bila kujali dini zao waweze kupata elimu.
Barabara zaidi ya kilomita 11,000 wakati wake. Kabla yake chini ya kilomita 5,000
Kikwete aliachiwa mipango mingi ya ujenzi wa barabara toka serekali ya awamu ya tatu.
Wanafunzi vyuo vikuu zaidi ya 130,000 wakati wake. Kabla yake hawafiki hata 50,000
Kikwete kajenga vyuo vikuu vingapi ?.Ni wanafunzi wangapi wamepewa mikopo na serekali wakati wa Nyerere elimu ilikuwa bure watoto wa masikini walisoma bila matatizo.
Zahanati kila kijiji.
Sijaziona hizo zahanati hata kama zipo nina hakika madawa,wataalamu na vifaa havitakuwepo.Wewe hujiulizi kwanini wabunge,mawaziri na wazito wengine kila wakiugua wanakimbizwa India kama hizo zahanati zingekuwa na vifaa na wataalamu kwanini safari za India zimekuwa zikiongezeka ?.
Tuna akiba ya fedha za kigeni ya zaidi ya miei minne hazina, kabla yake akiba ya siku 10 tu.
Hizi ni ndoto za mchana BOT hakuna akiba ya fedha za kigeni ya kutufikisha mwezi mmoja.
Tuna akiba ya chakula cha miezi 9 ijayo, kabla yake hatuna hata cha siku 10.
Utakuwa unaishi Dar nenda vijijini watu wanakula mloo mmoja wewe unadanganya watu tuna akiba ya chakula ya miezi tisa ijayo.Ukipita kwenye maghala ya hifadhi ya chakula ya serekali hakuna akiba ya chakula,hakuna fedha ya kununua chakula.
Tuna ma power tiller, matrekta yanayotolewa kwa mkopo nafuu kuendeleza kilimo, kabla yake? hata jembe la mkono hukopeshwi.
Kwi kwi kwi teh teh teh.
Bahati mbaya wewe si mkulima hayo matrekta ya mkopo ni siasa tupu wanaofaidika ni wanasiasa wenye influence kubwa mkulima wa kawaida hana nafasi.Power tiller hazifai katika baadhi ya maeneo hasa yale yenye ardhi ngumu na mfinyanzi.
Bakwata kama ni kweli hizi habari, nawaunga mkono. Utakuta wale wanaokataa sensa ni wale wanaoabudu binaadam wenzao, wasio na dini. Hivi inawakera nini haswa/ mbona polisi unaulizwa kabila?