Serikali yetu ni sikivu. Tuweke kipengele cha dini. Kwa Waislamu tuongeze washia, suni n.k. na sehemu/mikoa/wilaya walipo kwa wingi. Tufanye hivo hivyo kwa Wakristu (katoriki, sda, anglikana n.k). tusiiachie hapo, hata makabila yetu yote yaorodheshwe. Ni vizuri tujuane. Nakiri kuwa sijui faida ya hizo takwimu wala kama kuna tija yoyote itakayopatikana.
Ninachojua ni kwamba hizo takwimu zitaibua malumbano. Tutaweza hata kuhoji timu ya wanaondesha zoezi la sensa kama ina uwiano wa kidini , kikabila n.k. Tusipokuwa waangalifu yataligawa taifa kwa misingi ya udini na ukabila. Mzee Mwinyi aliwahi kuonya kwamba tumeshiba amani. Sasa tuchungulie sehemu nyingine.
Inaelekela baadhi yetu hawapati somo la yanayotokea huko nigeria, somali (pamoja na kwamba ni waislamu watupu), pakistani n.k. tuendeleee tu kuhamashishana kuchokonoa yanayotutengenisha badala ya yanayotuunganisha.
Tunaelekea kusiko, walah! Mungu Ibariki Tanzania.