BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Hao wanaohesabu watu wasithubutu kuniuliza dini yangu unless wawe wana mpango wa kunijengea nyumba ya ibada kwenye compound yangu.. Vinginevyo dini yangu itabaki kuwa yangu na haitamsaidia mwingine yeyote..
 
Ebu tuongelee 'Kisayansi' hili swala.....kwenye 'Sensa', kama ilivyokuwa kwenye scientific survey nyingine...lazima uwe na 'definition' ya variables zako. Sasa kama dini inalazimishwa iwe mojawapo...lazima uidefine...na pia udefine 'criteria' za kumuita huyu ni 'muIslamu' na yule ni 'mKristo'.

Sasa swali....'muIslamu' ni nani na 'mKristo' ni nani? Kwa juu juu tu mtu unaweza kudhani ni rahisi kujibu..si huyu anaitwa Juma, Rashidi, Fatma, Shamsa..wazazi wake ni waIslamu bla bla blaa...au huyu anaitwa Joseph, Richard, Faith, Sasha...wazazi wake ni waKristo bla bla blaa.....Is that scientific enough kudefine variable ya uDini kwenye sensa? Je mtu kuwa dini fulani ni jina tuu lenye mahadhi ya hiyo dini au wazazi wake kuwa waumini wa hiyo dini?

Naamini kuna vigezo/misingi kadhaa vya kuweza kujua kama mtu ana imani thabiti ya kiIslamu au kiKristo..ambayo haiwezi kujibiwa na swali moja tu kwenye questionnaire ya sensa kama' Dini:...........' How sure you are kuwa atakachojaza mtu ndio imani yake...utakuta mlevi fuska anaitwa Jafari au Geophrey umuhesabu kama muIsalmu au mKristo, kisha utambe sisi tuko wengi zaidi tunadeserve mgawanyo mkubwa zaidi wa rasilimali!? Upuuzi mtupu..
Safi sana Riwa.............. I second you 100% umetackle hii hoja from a scientific angle, umenifurahisha Daktari.
 
Hivi huyu Rais wetu wa sasa aliyebakiza miaka yake miwili Na nusu aondoke Na Chama lake ana MSHAURI kweli BABU HUYU..!! Akifanya mchezo muda wake uliobaki utamletea huzuni ya milele..

Nilisikia kwamba washauri wake wote walimkimbia Kwa sababu alikuwa anawatosa..Kabaki Wassira.. Sasa huyu aliyewahi kukiasi Chama toka lini akawa mshauri mzuri.. Ushauri wake utakuwa umautimauti tu, kwanini serikali isikae Na viongozi hawa wa Dini Na kuwauliza Chanzo cha vurugu zao badala ya kuwaona wapuuzi wanaostahili kumwagiwa Maji ya uchungu Na virungu.. Hata Kama kweli ni wapuuzi Lakini bado ni raia halali Wa JMT.. Wanastahili kusikilizwa Na kuelekezwa wanachodhani ni Hoja Na mtagundua ni nani Yuko nyuma ya mapazia Haya ya chokochoko.

Sasa serikali iko kimya, inaachia raia wahukumiane.. Na hukumu ya raia ni ubaguzi Na Chuki vitazuka.. Kwanini serikali hii sio SIKIVUU..

Mrisho.. Muda wako uliobaki ni kidogo.. Usipobadili mwelekeo nakwambia Utaona 2 years Kama gunia la Miaka Elfu ..

Rais kawaletea demokrasia iliyotukuka na anaendelea leo bado unamuona hajafanya kitu?

Kumbuka Mawaziri wote ni washauri wa Rais, sasa tuambie Baraza la Mawaziri kabaki Wassira tu? kwi kwi kwi teh teh teh !

Huna zaidi ya huo *****? kuna Rais aliyefanya mengi mema zaidi ya Kikwete Tanzania hii? weka tuone kama hujakuta Kikwete kafanya zaidi kwa muda mfupi sana.

Natamani katiba mpya impe uwezo wa kugombea tena aendelee kwa miaka mingine itakayokuwa kwenye katiba mpya.
 
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

"Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi," alisema Shehe Kundecha.


Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

"Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?" Alihoji.

Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

"Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini," alisema.

Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

CHANZO: HabariLeo
Amini usiamini UTUMWA namba moja ni kufuata IMANI ya jamii nyingine ukaacha ya asili yako!.
 
Waislam jamani mbona hamuelewi wala hamueleweki wala hamtaki kuelewa.
Inabidi tuanze kuwajadili kwanini hamuelewi na hamtaki kuelewa coz inawezekana mna Sababu Maalum.

BAKWATA wameshindwa kujua idadi ya Waumini wa dini ya Kiislam ktk nchi yao mpaka Serikali ije iwafanyie? Bakwata inafanya nini au uwepo wake una faida gani kwa Waislam kama hata kasensa cha waislam hawajui.

Serikali haina dini, waislam wanailazimisha serikali iwe na Dini, swali linakuja Je serikali itafuata dini gani?

Waislam wanatakiwa waende shule kama shule(elimu Dunia) badala ya Chuo(madrasa) ili tuweze kwenda sawa.
Sote sisi ni binadamu na sote tupo Duniani sasa mahali tunatofautiana ni hapa:
Muislam yuko Duniani lkn anasoma kwa bidii kabisa Elimu Akhera(Life after Death) halafu anaitumia hiyo elimu akhera kuishi duniani.
Dini nyingine wao wanasoma elimu dunia iwasaidie kuishi duniani kwasababu wanaishi duniani. Suala la kumuomba mungu linabaki kuwa ni la Mungu na siyo kuchanganya. Mfano mdogo hapa ni kwamba leo hii muislam hataki kumpeleka mtoto shule ya elimu dunia akasome japo Maendeleo ya jamii ajue kufanya hata ka-research cha sensa ya waislam pale Magomeni Kagera ili aisaidie BAKWATA hapana, yeye amejikita kwenye madrasa(Chuo, kama wanavyoita) akisoma elimu Akhera namna atapata thawabu kwa mungu kama atapigania Tanzania, Africa, na Dunia nzima wakabadilika na kuwa Waislam. Hapo ndipo tofauti inakuja. Muislam anataka sensa ya waislam kwa mujibu wa dini ya kiislam lkn hataki kusoma jinsi ya kufanya hiyo sensa anataka afanyiwe na watu waliosoma elimu duniani then aiingize kwenye elimu akhera kisingizio imepitishwa na dini.
 
Huyo anayewatia ujinga watanzania kawapata kweli.....

Mnapigania dini huku madini yenu yanasombwa...........
Mnabishania dini huku maliasili zinabebwa......

Kweli ngozi nyeusi inasikitisha............
BADILI TABIA, I salute!!!:clap2:... What a word!!!

AND , That is why it is inevitable, naturally speaking to have National and Community tragedies ... "As the only way to bring people to their sense"

AND Mark my worlds tukiendelea with this kind of nonsense ... The National Tragedies isnt far ...it will eventually come as the only way of National Enlightenment!! Tutakuwa na UTU WA TAIFA in place! Na utu haujui dini, kabila jinsia ila ndio Utanzania kamili na Umoja wetu katika kupambana na Ustawi na Maendeleo ya kila mmoja wetu!!

Bila majanga yaliyosheheni Maumivu ya kutosha, Mwanadamu mara nyingi hawezi kupevuka na kufikia FIKRA TIMAMU! :coffee:
 
Wewe shida yako nini? Mbona nyie mna TAG, Catholics, Lutheran and etc hamsemi? Hakuna kinachogawanyika huu ni upumbavu kwasababu suala la dini ya mtu lina umuhimu katika mipango miji ya nchi. Mfano Uingereza hamuwezi tu kujenga msikiti au kanisa hadi upewe kibali na halmashauri ya jiji. Sasa unadhani kwanini wamesisitiza halmashauri ndio zitoe vibali? Tatizo lenu mnasumbuliwa na UDINI TU!!!! Suala la dini lina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu . Dini itatusaidi kujua yafuatayo nawaelekezi nchi vihiyo wa udini:-
a. Tufahamu katika kila eneo ni nyumba za ibada ngapi zijengwe (misikiti, makanisa au masinagogi) na vile vile maeneo ya kuzikana yatengwe kiasi gani yaani makaburi. Hivyo basi dini itatusaidia katika mipango miji nchini mwetu.

b. Tufahamu sababu za kurudi nyuma kimaendeleo (mfano waislamu) je imesababishwa na wao wenyewe? taasisi au mfumo mbovu uliopo?

c. Tufahamu mfumo wa nchi kiutendaji unakuwaje tukijumuisha na imani za watu kama sehemu ya maisha yao mfano ni likizo ngapi ziwepo katika nchi kama sikukuu za mapumziko. Uingereza mfano au Marekani hawana kitu kinaitwa public holiday for Eid but wana public holiday for Christmas, New Year, St. Patricks etc. Saudi Arabia, UAE, na Oman hawana sikukuu za Christmas and New Year. Ni kwasababu ya sensa wameona hakuna umuhimu wa kupumzika siku hizo. Sasa taarifa hizo hakuna mahali zinatoka zaidi ya katika sensa ILIYOANDALIWA NA SERIKALI YA MLIPA KODI!!!!

d. Kufahamu pia usambazi wa vyakula nchini. Mfano waislamu wana mwezi mtukufu wa ramadhani na huwa wanatumia vyakula vya aina fulani nchini. Vile vile wakristo wana Kwaresma huwa pengine wanatumia vyakula vya aina fulani. Hatuwezi kufahamu hilo bila ya kuwepo takwimu sahihi.

Hembu nipeni nyie sababu za msingi kisiwepo kipengele cha dini zaidi ya fear zilizogubikwa na imani za ubaguzi wa kidini???

Naomba kuwaulizeni jamani...hivi huyo Mungu (ambaye wote nyie wakristo na waislam mnadai mnamuamini) mbona sijaona popote pale anadai anataka ajue idadi ya wale wanaomuamini? Ngozi nyeus tabu sana!
 
BAKWATA wasitafute kujihalalisha na kukubalika kwa Waislaam wenzao kwa hoja nyepesi kama hizi:
-Walitaka tujiunge na OIC;
-Wakataka mahakama ya kadhi ianzishwe na kugharamiwa na kodi zetu;
-Sasa wanataka tufanye sensa ya Waislaam kwa kodi zetu.
BAKWATA wana mengi mazuri wanayoweza kuwafanyia Waislaam bila ya kuishinikiza serikali yetu kwa lolote. Nchi yetu haina DINI na itabaki hivo hata kama Waislaam watakuwa asilimia 95 ya idadi ya WATANZANIA wote.
 
Nina hakika kipengele cha dini kikiingizwa utasikia sensa imetumia mfumo kristo.
Mkuu, kipengele hicho kikiigizwea watasema hawawaamini wakristo, hivyo mawakala/data clerk wote itabidi wawe waislam kwasababu wakristo wanatuhumiwa kuwachakachua.

:confused2::confused2:sijui kama wanajua wanachokitaka!!
 
Rais kawaletea demokrasia iliyotukuka na anaendelea leo bado unamuona hajafanya kitu?

Kumbuka Mawaziri wote ni washauri wa Rais, sasa tuambie Baraza la Mawaziri kabaki Wassira tu? kwi kwi kwi teh teh teh !

Huna zaidi ya huo *****? kuna Rais aliyefanya mengi mema zaidi ya Kikwete Tanzania hii? weka tuone kama hujakuta Kikwete kafanya zaidi kwa muda mfupi sana.

Natamani katiba mpya impe uwezo wa kugombea tena aendelee kwa miaka mingine itakayokuwa kwenye katiba mpya.
Kafanya nini?
 
Ebu tuongelee 'Kisayansi' hili swala.....kwenye 'Sensa', kama ilivyokuwa kwenye scientific survey nyingine...lazima uwe na 'definition' ya variables zako. Sasa kama dini inalazimishwa iwe mojawapo...lazima uidefine...na pia udefine 'criteria' za kumuita huyu ni 'muIslamu' na yule ni 'mKristo'.

Sasa swali....'muIslamu' ni nani na 'mKristo' ni nani? Kwa juu juu tu mtu unaweza kudhani ni rahisi kujibu..si huyu anaitwa Juma, Rashidi, Fatma, Shamsa..wazazi wake ni waIslamu bla bla blaa...au huyu anaitwa Joseph, Richard, Faith, Sasha...wazazi wake ni waKristo bla bla blaa.....Is that scientific enough kudefine variable ya uDini kwenye sensa? Je
mtu kuwa dini fulani ni jina tuu lenye mahadhi ya hiyo dini au wazazi wake kuwa waumini wa hiyo dini?

Naamini kuna vigezo/misingi kadhaa vya kuweza kujua kama mtu ana imani thabiti ya kiIslamu au kiKristo..ambayo haiwezi kujibiwa na swali moja tu kwenye questionnaire ya sensa kama' Dini:...........' How sure you are kuwa atakachojaza mtu ndio imani yake...utakuta mlevi fuska anaitwa Jafari au Geophrey umuhesabu kama muIsalmu au mKristo, kisha utambe sisi tuko wengi zaidi tunadeserve mgawanyo mkubwa zaidi wa rasilimali!? Upuuzi mtupu..

Hebu twende kisayansi maana umejileta anga zangu:-

Tudefine what is a variable first ? A variable is something you used to measure in order to get an information from the data.

Turudi katika swali lako tuanze na kipengele cha dini hebu tuchanganue ni swali gani utauliza ili uweze kujua huyu muislamu, mkristo au pagani? Jibu ni kumuuliza katika forms WEWE NI DINI GANI? Jibu atakalolitoa hapo haijalishi ni John, Rashid, Musa au Richard kwani ni yeye ndiye anayejua ni dini gani anafuata kama mpagani, mormons, muislamu, mkristo.

Tukishalipata hilo jibu tunapokusanya data tunabainisha wafuasi wa kikristo wapo wangapi, waislamu , waabudu ngombe na mbuzi etc. Suala la authenticity ya data litategemea unataka kufanya nini? Siku zote data zinazokusanya primary zinahitaji kuwa verified na ndio maana UMUHIMU WA TAASISI ZA KIDINI ZIWEPO KATIKA ZOEZI HILO LA KUKUSANYA TAARIFA.

You are talking non-sense as suala la imani is very relevant kwani ukiitazama Tanzania sasa hivi haina mipango miji kabisa tumekaa kama chooni nyumba zinajengwa kiholela, nyumba za ibada zimejengwa maeneo mengine ambapo kuna waumini hawafiki hata wawili? Huo ni upuuzi and to be honest it is absolutely ridiculous!!!
 
Correction...ni dini moja tu inayoleta migogoro duniani...dini yenye kutoa matamko tunayojadili hapa...!

Na kwa kukuongezea tu,

Wakristo na waislamu huwa mnaungana na kuwa kitu kimoja katika kuwashambulia watu wasioamini katika dini zenu au wale wasiomuamini Mungu wenu (ambaye mnaamini yuko mmoja tu)...cha ajabu mkiwa wenyewe huwa hamuelewani kabisa kuhusu huyo huyo Mungu na ndio chanzo cha hizo vurugu zenu...kubishana na kuuana kwa Mungu ambaye hata kwenu bado hamjamuelewa!
 
Nimesikiliza Redio Africa, wakimhoji Sheikh mmoja(kiongozi) nikastuka. Kwa maoni ya Sheik huyo, dhumuni kubwa ni kuwawezesha Waislamu kupanga vyema miakakati ya elimu. Anadai, kama ilivyo sasa hivi ni vigumu kujua ni vijana/watoto wangapi wapo ambao watahitaji kusomeshwa madrasa. Bila kuwa na Takwimu sahhihi za waislamu nchini ni vigumu kupanga masuala yote yanayohusu elimu na mengineyo.

Kauli ile imenishangaza sana! Kumbe Waislamu hatujui idadi yetu! Inawezekana kweli? Nilidhani tunaweka kumbukumbu maana hata tunapofungisha ndoa ni lazima tunapotoa cheti cha ndoa tumwandikishe aliyeoa na anayeolewa. Mbona ukienda makanisani unapata kumbukumbu zote, siku muumini alizaliwa, alizaa, alibatiza nk. Tujipange sisi wenyewe sio lazima mambo yetu ya dini yategemea hisani ya Serikali! Serikali haihitaji takwimu kuhusiana na imani yetu, kabila letu na tusilazimishe mambo. Waachieni watawala ya kwao sisi tubaki na ya kwetu
 
Kwani hata waislamu wangekuwa 99% ina implication gani kwa maendeleo ya taifa? Itasaidia kujenga shule zaidi, hospitali, maji safi, barabara umeme, n.k?

Mbona watanzania mnaacha kufuatilia na kushuguligikia mambo ya maana mnakeshea ujinga? Sasa hivi tulitakiwa tunaumiza kwa miaka 50 ya uhuru wetu mbona hali inazidi kuwa duni? Kwa rasilimali tulizo nazo madini, ardhi, watu, maji, bahari, milima mbuga za wanyama, amani, maziwa, mito hali nzuri ya hewa mbona umaskini unatumaliza! Mnakalia kutokwa mishipa ya shingo kutaka kujua waislamu na wakristu wepi wengi!! Au mnataka kutangaza taifa la kiislamu muwafukuze wakristu?

Mtanzania amka, umaskini, magonjwa, ujinga havichagui dini hata mnekuwa waislamu peke yenu isingewasaidia!!

Nimekugongea thanks mkuu, manake bado nilikuwa natafakari faida watakayoipata katika hili. Halafu likanijia swali, je wanafaham kuwa kuna nyumba/koo/kaya ambazo zimechangamana katika dini zote hizo? Kwamba mama mkristo baba muislam & vice versa? Naunga mkono serikali katika hili wasiyumbishwe kama wanataka hizo data waitishe sensa yao kwani hesabu hazidanganyi kama ni mbili itakuwa hiyo hiyo iwe imehesabiwa na serikali au dini.
 
Huyo anayewatia ujinga watanzania kawapata kweli......
Mnapigania dini huku madini yenu yanasombwa...........
Mnabishania dini huku maliasili zinabebwa......


Kweli ngozi nyeusi inasikitisha............
Watanzania tumelogwa................ Na aliyetuloga keshakufa!!!!!!!!!!
 
Naomba kuwaulizeni jamani...hivi huyo Mungu (ambaye wote nyie wakristo na waislam mnadai mnamuamini) mbona sijaona popote pale anadai anataka ajue idadi ya wale wanaomuamini? Ngozi nyeus tabu sana!

Ulijiuliza swali hilo ulipokuwa unaenda huko kuabudu ? Acheni udini wenu huo hamna hoja za msingi zaidi ya kuleta blah blah tu.
 
Wewe ni shia au suni maana hao si wamoja pia katika mipango yao kama ilivyo kwa wakristo pia ambapo kuna waanglikani, wakatoliki n.k. Inayofanya sensa ni serikali sasa wanadini wanataka takwimu za nini. Tatizo la Waislamu ni utawala uliogawanyika ambapo kupata idadi hao kwa sensa yao wenyewe ni kikwazo. Mfano. Utakuta shehe wa Tabora anaitwa kuja kufungisha ndoa hapa Lindi lakini shehe wa hapa Lindi hajui na hana taarifa yoyote. so, kumbukumbu ya msikiti wa hapa Jirani hawana records. Ni kukosa busara kwa Bakwata kutokuwa na mipango yake ya kujijua yenyewe na watu wake bali kutegemea vya bure toka serikalini. Yawezekana serikali ikawakubalia but matokeo yakaja kuwa wakristo wako wengi na hapo waislamu watakuja na hoja ingine ya kuwa takwimu zimechakachuliwa na hivyo NBS iundwe upya ili na dini zishiriki. Waislamu ni tatizo kubwa mno!!!

Usitake kuwasemea Waislam hujui chochote kuhusu Uislam mkuu nani kakwambia ndoa za Waislam lazima zifungishwe na Sheikh? Kwa taarifa yako hata kama wewe ni Muislam mtoto wako anaolewa hunaweza kufungisha hiyo ndoa...halafu hakuna sehemu yoyote Waislam wamesema wao ni wengi wanachokiomba wanataka kujua wapo wangapi ili iwe rahisi kwao kupanga mambo yao wameomba kama raia.
 
Kafanya nini?

Wanafunzi zaidi ya million 8 wako mashuleni wakati wake. Kabla yake chini ya million 4

Barabara zaidi ya kilomita 11,000 wakati wake. Kabla yake chini ya kilomita 5,000

Wanafunzi vyuo vikuu zaidi ya 130,000 wakati wake. Kabla yake hawafiki hata 50,000

Zahanati kila kijiji.

Tuna akiba ya fedha za kigeni ya zaidi ya miei minne hazina, kabla yake akiba ya siku 10 tu.

Tuna akiba ya chakula cha miezi 9 ijayo, kabla yake hatuna hata cha siku 10.

Tuna ma power tiller, matrekta yanayotolewa kwa mkopo nafuu kuendeleza kilimo, kabla yake? hata jembe la mkono hukopeshwi.

Kwi kwi kwi teh teh teh.

Bakwata kama ni kweli hizi habari, nawaunga mkono. Utakuta wale wanaokataa sensa ni wale wanaoabudu binaadam wenzao, wasio na dini. Hivi inawakera nini haswa/ mbona polisi unaulizwa kabila?
 
Hakuna correction hapo, nyie wote wale wale tu, kazi kubishania miungu wa kigeni...kutawaliwa kifikra ni ukoloni wa kutisha na mbaya kabisa!
Mungu wa kigeni or Mungu wa kienyeji , matatizo yatatoka wapi kama kila mtu atajali imani yake tu? Huyo Mungu wako wa kienyeji si ndiyo ameishia kuua albino,wazee vikongwe na mifugo kwa kutambika? Huko kutawaliwa kwako kifikra umekuona kwenye dini tu? mbona karibu kila kitu ni cha kikoloni? Mkuu kama umeamua kuabudu mbuyu, joka kubwa, kwenda kanisani, kwenda msikitini nk ni choice yako, cha muhimu hapa ni kutoanza kuingilia imani za watu wengine na kuleta chokochoko kama hizi tunazoziona...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom