Swali kwa Jaji Mkuu: Je, ni haki kwa kina Rostam Aziz kutozwa faini badala ya kifungo lakini kina Mbarikiwa kupewa kifungo badala ya faini?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1696045406403.png

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Mheshimiwa Jaji Mkuu,

Tarehe 29 Septemba 2023, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya, Paul Ntumo, alimhukumu kifungo cha miaka mitatu na nusu, Mchungaji Mbarikiwa Dickson Mwakipesile (39), baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuendesha huduma ya kikosi kazi cha Injili kabla ya kupata usajili kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kama sheria ya vyama vya kijamii inavyotaka.

Hukumu hiyo ilitolewa chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kijamii. Kifungu kinaipa mahakama mamlaka ya kutoa adhabu mojawapo kati ya tatu. Kuna:
  1. Ama adhabu ya kulipa faini, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha chini (minor offenses),
  2. Au adhabu ya kifungo, kwa makosa yenye ukubwa wa kati (intermediate offenses),
  3. Au adhabu zote mbili kwa pamoja, kwa makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses).
Kwa mujibu wa busara ya Mahakama ya Hakmu Mkazi wa Mbeya, kitendo cha kuendesha kanisa kabla ya kupata usajili ni "interdmediate offense" na hivyo kuamua kutoa adhabu ya kifungo kwa Mwakipesile.

Mchungaji Mwakipesile amekuwa anaituhumu serikali kwamba inawaona wanachi kama nyani au kenge. Yeye ni baba mzazi wa Sifa Bujune, Muimbaji wa Injili anayetuhumiwa kusambaza uongo kutokana na Wimbo wake wa “Mnatuona Nyani tu”,

View: https://youtu.be/JSVmJqUmbHg

Wakati huo huo, kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini).

Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, chini ya Sheria ya Kanuni za Adhabu inayotaja yenye mfumo wa adhabu sawa na mfumo wa adhabu uliomo kwenye sheria ya vyama vya kijamii uliotajwa hapo juu. Mwishowe mahakama iliona kwamba Akram alifanya "minor offense." Hivyo Akram akatozwa faini, badala ya kupewa adhabu ya kifungo.

View: https://youtu.be/-FWpqOItZrI

Kabla ya hukumu ya kesi hii, Mchungaji Mbarikiwa alidai kwamba amekuwa anaendesha huduma za kikanisa kwa miaka mitatu kwa kutumia kibali cha serikali. Pia alidai kuandamwa na vyombo vya dola, kwa kiwango kilichosababisha kifo cha mtoto wake.

Binti yake aitwaye Sifa aliwekwa rumnde kwa siku nne kwa tuhuma za kuimba wimbo wa uchochezo, lakini akashitakiwa mahakamani kwa kosa la kusambaza uwongo. Mchungaji Mbarikiwa alisema kuwa hii ilikuwa ni mikakati ya kumnyamazisha.

Mazingira ya kesi huu pamoja na hali ya kutotabirika kwa maamuzi ya mahakama kuhusu utaratibu wa kutamka adhabu kunazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Na tatizo liko hivi:

  1. Mahakama inayomheshimu jangili na kumtweza mchungaji au shehe ni mahakama ya hovyo sana.
  2. Mahakama inayomheshimu mwarabu na kumtweza Mbantu wa Mbeya haina haki ya kuitwa mahakama.
  3. Mahakama inayowatukuza wenye mali na kuwakandamiza makabwela sio mahakama kamwe.
  4. Mahakama inayotukuza watu wenye mamlaka ya kisasa na kutwatweza wanyonge inakuwa na watendaji ambao wana tatizo la ombwe la kimaadili.
  5. Kwa ujumla, mahakama inayokumbatia kanuni ya umachiveli, isemavyo kwamba "matokeo mazuri yanaweza kuhalalisha mbinu yoyote, hata kama ni mbinu haramu," haitakiwi katika Tanzania ya Nyerere.
Hivyo, tunapenda kutoa mapendekezo yafuatayo kwa vigogo wa nchi hii, na hasa wale wenye mapenzi mema, na wanaojali kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo, zile tunu kuu za taifa hili linaloitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:

1. Mheshimwa Jaji Mkuu achukue hatua za kulinda heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kuchukua hatua stahiki za kufuta uhiari wa kimamlaka (discretionary powers) walio nao mahakikmu na majaji katika hatua ya kutamka adhabu, kwa kuhakikisha sheria zote zinazotaja adhabu zinatoa vigezo vya kutofautisha kinaganaga kati ya aina zifuatazo za adhabu za kimahakama:

(a) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha ukomo wa chini (minor offenses) yanayostahili adhabu ya kulipa faini kama yakithibitishwa;​
(b) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha kati (intermediate offenses) yanayostahili adhabu ya kifungo kama yakithibitishwa; na​
(c) Makosa yenye ukubwa wa kiwango cha juu (aggravated offenses) yanayostahili adhabu zote mbili kwa pamoja kama yakithibitishwa.​
(d) Makosa yenye ukubwba wa kiwango cha ukomo wa juu kabisa (heinous offenses) yanayostahili adhabu ya kifo kama yakithibitishwa.​

2. Mheshimiwa Rais Samia atumie mamlaka yake kama Mkuu wa nchi kufuta mara moja adhabu aliyopewa Mchungaji Mwakipesile ili kuzuia matope yanayoweza kumrukia mabegani mwake, maana sasa ni wazi kwamba Mahakama inaburuzwa na serikali inayoongozwa na Rais Samia.

3. Rais Samia amwagize Waziri wa Mambo ya ndani, Mhandisi Hamad Masauni, kumpa Mchungaji Mwakipesile usajili aliouomba, maana, utafiti wetu unaonyesha kwamba, hatua zote zinazotakiwa kisheria tayari Mwakipesile amezifuata. Kanuni za utwala wa sheria na misingi ya Katiba ya nchi kuhusu uhuru wa kuabudu ifuatwe. Mwombaji asajiliwe, na kama akifanya ukiukaji aadhibiwe kihalali pasipo uhuni wa kutengeneza makosa ya kubumba.

4. Kamati za Ulinzi na Usalama mkoani mbeya zipanguliwe na kupangwa upya. Zinapanga na kutekeleza operation za kiusalama zenye sura ya uhalifu dhidi ya ubinadami, yaani umwagaji damu ya mtu asiye na hatia. "Individual prophylactic operation" iliyofanyika kwa kuua mtoto wa MchungajimMbarikiwa ili kumdhoofisha Mchungaji huyu ni mfano hai.

Tunawasilisha.

Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023

============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================

MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ​

1696045911682.png

Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu. Tazama vielelezo vya picha hapa chini.

Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.

Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.

Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:

1696045845981.png

1696045860930.png

1696045876995.png
 
View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Mheshimiwa Jaji Mkuu,

Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), wa huko Mbeya, jana amehukumiwa miaka mitatu jela chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kiraia. Kosa lake kuendesha Kanisa lisilosajiliwa. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.
Hii kesi ya Mdogo wake azizi ya Mwaka 2019 enzi za JPM nadhani kuna namna waliimaliza nje ya mahakama.
 
Huyo ndiyo mtu mweusi bana...Anayeweza kupindisha sheria waziwazi...na kuiba matrilioni ya pesa za umma huku mwananchi mwenzie hana uhakika hata wa mlo mmoja na anaweza kukata roho kisa hana pesa ya kununua Aspirin ili moyo wake upige vizuri.

Halafu tukitupiwa maganda ya ndizi huko nje tunalalamika eti tunabaguliwa wakati tunayofanyiana sisi kwa sisi ni zaidi ya unyani.

Batombaning'we! 😬😬😬

IMG_20230729_084104_495 (1).jpg
 
View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Mheshimiwa Jaji Mkuu,

Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), wa huko Mbeya, jana amehukumiwa miaka mitatu jela chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kiraia. Kosa lake kuendesha Kanisa lisilosajiliwa. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.

View attachment 2766819

Lakini, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe alitozwa faini, badala ya kifungo.

View attachment 2766818
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kufuta undumilakuwili huu.

============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================

MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ​

Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.

Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.

Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.

Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:

View attachment 2766815

View attachment 2766816

View attachment 2766817
Eti mbarikiwa? Mbarikiwa wa nini? Huyo mtu ni mwehu na anatengeneza "cult" ya wehu. Naipongeza Serikali kwa hatua madhubuti waliochukua. Naye Kibwetere alianza hivihivi akawateka watu kwa kusingizia dini kisha akawachoma moto.

Tusije ilaumu Serikali baadaye kwa kuendeleza vidhehebu uchwara
 
Matajiri wote hawafungwi miaka.....hata mimi sijawahi kuona.
Nikitazama historia ya googreyeo na Jeseon wanasiasa walifanyiwa interrogation kali sana na hata kuchinjwa hadharani wanapo kosea hili jambo limeifanya Korea zote mbili mpaka leo kuheshimu sana sheria. Tanzania tunacheza makida makida sana hasa baada ya utawala wa kwanza
 
Eti mbarikiwa? Mbarikiwa wa nini? Huyo mtu ni mwehu na anatengeneza "cult" ya wehu. Naipongeza Serikali kwa hatua madhubuti waliochukua. Naye Kibwetere alianza hivihivi akawateka watu kwa kusingizia dini kisha akawachoma moto.

Tusije ilaumu Serikali baadaye kwa kuendeleza vidhehebu uchwara
Kama ni Ukibwetere wakitakiwa waanze n Mwamposa na Geordave
 
View attachment 2766809
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Mheshimiwa Jaji Mkuu,

Mchungaji anayeitwa Mbarikiwa Mwakipesile (39), wa huko Mbeya, jana amehukumiwa miaka mitatu jela chini ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya vyama vya kiraia. Kosa lake kuendesha Kanisa lisilosajiliwa. Kifungu kinatoa fursa ya kulipa faini u kifungu, au vyote kwa pamoja. Mahakama imeamua kutoa adhabu ya kifungo.

View attachment 2766819

Lakini, Akram Aziz, mdogo wake Ristam Aziz, alikabiliwa na kesi ya mashtaka 75 ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za Serikali, silaha za aina mbali mbali na risasi zake (tazama Kkiambatanisho hapa chini). Kesi yake iliendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwishowe alitozwa faini, badala ya kifungo.

View attachment 2766818
Undumilakuwili huu unazitia doa mahakama za Tanzania, ambazo utendaji kazi wake unasimamiwa na Jaji Mkuu. Hivyo, tunatoa wito kwako Mheshimwa Jaji Mkuu: tunaomba ulinde heshima ya Mhimili muhimu unaoitwa Mahakama kwa kufuta undumilakuwili huu.

============KIAMBATANSHO KUHUSU KESI YA MDOGO WAKE ROSTAM AZIZI==================

MUHTASARI WA KESI YA MDOGO WAKE BILIONEA ROSTAM AZIZ​

Mnamo 30 Oktoba 30 2018, saa 7 mchana maeneo ya Msasani, Jijini Dar, Akram Aziz, mdogo wake Rostam Aziz, alikamatwa na vyombo vya dola akiwa na nyara mbalimbali za serikali zikiwemo Pembe za ndovu.

Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.

Ilifahamika kuwa amekuwa ni “Mastermind” wa ujangili nchini kwa muda mrefu sana na ndiye kinara wa mauaji ya tembo na wanyama wengine kwenye mbuga zetu.

Taarifa za uhakika zilisema kuwa mtandao huo wa ujangili ulikuwa unasimamiwa na Kaka yake Rostam Aziz pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali katika awamu zilizopita. Hatimye Akram alitiwa hatiani na kupewa adhabu ya kulipa faili badala ya kifungo. Picha zifuatazo ni baadhi ya silaha alizokamatwa nazo:

View attachment 2766815

View attachment 2766816

View attachment 2766817

Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
30 Sep 2023
Hakimu wa hii kesi atakuwa na mwisho mbaya sana, matokeo ya kutumika mithili ya toilet paper utaishia kwa Septic chambee tuuu.
 
Nikitazama historia ya googreyeo na Jeseon wanasiasa interrogation kali sana na hata kuchinjwa hadharani wanapo kosea hili jambo limeifanya Korea zote mbili mpaka leo kuheshimu sana sheria. Tanzania tunacheza makida makida sana hasa baada ya utawala wa kwanza
Ukiiba kuku huambiwi ulipe faini unapigwa miaka mitatu jela ila vigogo( waliotunga sheria) wakiiba Bilions za umma wanaambiwa walipe faini za milioni 20.

Zile sheria zinatungwa kimkakati sana na ndio maana wanashirikiana kuhakisha hakuna Mabadiliko ya Kikatiba
 
Hakimu wa hii kesi atakuwa na mwisho mbaya sana, matokeo ya kutumika mithili ya toilet paper utaishia kwa Septic chambee tuuu.
Duniani mambo hayako hivyo.....huyo utaona anapanda na vyeo kwa ujasiri wake.

Anapiga hela za kutosha na utamwona akikwe mapipa hapa na pale kula bata ulaya na marekani.

Dunia hii mambo yanavyokwenda ni kunyume nyume.
 
Ilithibika kuwa Akram (Iqram) ni jangili wa muda mrefu na upekuzi uliofanyika nyumbani kwake ulibaini kuwa Akram anamiliki silaha nyingi kinyume cha sheria, pamoja na mihuri mingi bandia ya taasisi za serikali ambapo alikutwa na “vibali feki” vya uwindaji vingi sana.
Hii kesi ilikuwa konki😆😆😆
 
Back
Top Bottom