Baba wa Mwimbaji wa Injili aliyeimba "Mnatuona Nyani tu" ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuendesha Kanisa bila kibali

Mchungaji Pastor Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa Mnatuona Manyaji amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.


Taarifa kutoka kwa Maria Sarungi

===

View attachment 2766356
kwa kweli swala hili serikali imekosea pakubwa sana nitamkumbuka kwa nyimbo nzuri
 
Kwa nini nyumba ya ibada iwe na usajili serikalini katika nchi inayotoa uhuru wa kuabudu kikatiba kwa kila mtu?
Unaweza kuabudu 'roho' ukiwa nyumbani kwako.

Kitendo cha kutenga eneo la pamoja kwa ajili ya huduma sio tu za 'kiroho' tayari mnafanya makutano yanayohitaji ithibati ya ulinzi wa watu wanaokutana.

Kwanini usajili wa nyumba za ibada unafanyika Wizara ya Mambo ya Ndani wakati usajili wa Asasi za Kiraia unafanyika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, hali ya kuwa na dini ni miongoni mwa Asasi za Kiraia?
 
Mtu anakaa miaka mitatu bila kibali, Hawa wakaguzi wa vibali walikua wapi miaka yote Hio mitatu, hawakufanya ukaguzi? Wao wamechukuliwa hatua Gani sasa??

Tukiitwa manyani tunaanza kulalamika

Shenzi
Siku zite iko hivi, Ukiwa Mstaarabu
hata kama una mapungufu watu hukupuuza ila ukijikuta mjanja watu watataka wakuonyeshe kua hujui.
Ukiamua kukosoa wenzio hakikisha uko smart.
 
Mchungaji Pastor Mwakipesile ambaye mtoto wake Sifa Bujune alikamatwa kwa kosa la kusambaza uongo kwa kuimba wimbo wa Mnatuona Manyaji amehukumiwa miaka mitatu jela kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.


Taarifa kutoka kwa Maria Sarungi

===

View attachment 2766356
Miaka yote hiyo anafanya huduma take hawakuona kabla kama hana kibali?kuna jambo lingine labda.naamini atatumikia kifungo kwa furaha ktk imani.
 
Mtu anakaa miaka mitatu bila kibali, Hawa wakaguzi wa vibali walikua wapi miaka yote Hio mitatu, hawakufanya ukaguzi? Wao wamechukuliwa hatua Gani sasa??

Tukiitwa manyani tunaanza kulalamika

Shenzi
Suala zima la serikali kutoa kibali kuruhusu ibada linavunja haki za binadamu za watu kwenye kujiamulia wenyewe na uhuru wa kuabudu. Linavunja katiba ya Tanzania kwenye Freedom of Conscience.

Maana yake ni kuwa, badala ya watu kuamua waabudu vipi, serikali ndiyo inawaamulia waabudu vipi.

Badala ya watu kuchagua ibada zao ziweje, serikali ndiyo inawaamulia kuwa ibada zenu zitakuwa hivi, msipoenda tunavyotaka, tunawanyima vibali.

Msimseme rais, tunawanyima vibali.

Huu ni uvunjaji wa katiba ya Tanzania na haki za binadamu.
 
Kwa nini nyumba ya ibada iwe na usajili serikalini katika nchi inayotoa uhuru wa kuabudu kikatiba kwa kila mtu?

Serikali hata kodi haikusanyi kutoka nyumba za ibada, sasa zinasajiliwa kwa nini?

Nikisema hii habari ya kusajili nyumba za ibada serikalini ni namna ya serikali kudhibiti ibada na kuingilia uhuru wa kikatiba wa kuabudu nitakuwa nakosea?
Serikali haingilii uhuru wa kuabudu....

Ila serikali ni lazima idhibiti vitu vyote kupitia SAJILI....

La kujiuliza.....yanapotokea makosa ya KIJINAI huko katika nyumba za ibada nayo serikali ikae pembeni ?!!!
 
Tah tah tah... Nyundo 3 kwa kufungua kanisa bila kibali hii kasi iendelee Tupunguze Wahuni.
Kuna wavunjaji wengi sana wa sheria nchini. Ila wamekuwa wakiachwa wafanue wapendavyo, kwa sababu tu hawayagusi maslahi yenu/hawawakosoi.

Hawa wanaojitokeza hadharani kuwakosoa, ndiyo mnawatafutia zengwe. Na huu ndiyo utaratibu wenu kwa miaka nenda. Kutisha/kuwakomoa wapinzani wenu..
 
Back
Top Bottom