Chahali kama unadindisha rudi upambane hapa. Angalau CDM Mbowe yuko hapa, w ulikimbia kama Jike!
 
Mataga hamuoni hata aibu kuwa na cha kuongea kuhusu cdm Mbowe au Lissu?

Nini ambacho cdm, Mbowe au Lissu hawakukijua:


Kimya kingi? Mbona walisema kina mshindo mkuu? Wewe waona kimya?


Ninyi tulieni hapo hapo. Tuna ya muhimu zaidi kwanza.



 
Mbowe alijua kuwa atakamatwa na kuunganishwa na wenzake ktk kesi ya Ugaidi case no.63/2020, kesi hii ilikuwepo na wasaidizi wa chadema ni miongoni mwa watuhumiwa wa ugaidi.

Viongozi wenzake hawakumsaliti kwa sababu wanafahamu jambo lolote likiwa mbele ya mahakama hakuna jinsi zaidi ya kupambana kisheria na sio kuendelea kuvunja sheria kama walivyo fanya Bawacha.

huwezi kushinikinza taratibu za kisheria kwa maandamano au kukaidi ktk nchi inayo fuata utawala wa sheria, Mbowe kapelekwa mahakamani na hatua zingine za kisheria zitafuatwa.

viongozi wenzanke hawajamsaliti bali wanaheshimu Utawala wa kisheria.

unataka waikemee na kuilazimisha mahakama wamtoe Mbowe?! kweli hilo limekaa sawa? hapana.
 
Ukiacha hayo tu.
Kitendo cha Mwenyekiti kukamatwa halafu hakuna hata alieumizwa kilinishangaza.

Nikasema tuna safari ndefu bado.
 
Facts na ujue kucheza na Akili ya mtanzania.

Na hii kwa uchunguzi wangu umetokana kuwa Dar ndo jiji lenye Taswira ya Tanzania.
Hivyo wenyeji wa Dar ni hasa watu wa Pwani watu hawa sio wakorofi wapenda mapenzi na Ghahawa mtu kama huyu hiweziwambia andamane wala aburuzane na Police.

Asantee Tanzania asante Nchi yangu

Nakupenda Tanzania.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
🤣🤣
Mkuu wangu eee...
Komredi eee...karibu kijiweni kwangu Majohe unywe kahawa na Al Kasus mujarabu.....

Siye hatuna tabu....

Wateja wangu wanakunywa kahawa na vijana wenzangu "kubeti" katika masimu yao makubwa.....

#AmaniKwanza
#UtulivuKwanza
#HatunaNchiNyingineZaidiYaTanzania
#KaziIendelee
 
Watawala wamezidiwa nguvu za HOJA kukabiliana na Chadema.CCM haiwezi kukabiliana na Chadema kwenye uwanja wa siasa sawa.Freeman Mbowe ndiye MHIMILI wa siasa za upinzani.Ni jabali la siasa za Tanzania.Bila nguvu za dola kukabiliana na Mbowe na chama chake,CCM tungeshaisahau.

Kwa hiyo, kunahitajika umakini mkubwa katika maamuzi yao kipindi hiki ambacho mwenyekiti wao yupo gerezani.Hapa ndipo Chadema inapopaswa kuonysha kuwa Chadema ni Taasisi .Ukimya wao umekuwa mzuri mno maana umewapa nafasi ya kutafakari zaidi namna bora ya kupata ufumbuzi.Mbowe ni mtu imara na jasiri.ATAVUKA SALAMA na ataushangaza ulimwengu.
Nawapongeza Chadema kwa utulivu wao.Kesho siyo mbali.Tusubiri.
 
Ndiyo aina ya Watanzania ambao wana ufinyu mkubwa wa kupambanua mambo. Wao kuteswa na kubambikiwa kesi FEKI Viongozi na Wanachama wa Chadema ni shangwe na furaha kubwa, ngoja wabambikiwe kesi FEKI wao.
Una usalama gani, unafiki tu!
 
wewe kijana ni mpumbavu,tena kijana uwe na adabu.yaani unawasaminisha watanzania wote na Yule mtuhumiwa wa ugaidi!?. enzi za nyerere ungewekwa ndani na bakora za makalio za kutosha !
 
Katika nyakati za karibuni huyu Kigogo2014 alitumiwa na Chadema kama msemaji wao kwa kutukana viongozi wengine wa upinzani kama wasiofaa na kuwa chama cha upinzani kilichopo ni chadema tu.

Kigogo2014 akaonekana ndio mtu wa maana kuliko hata wanachedema wakongwe. Ila kwa tunaojua huyu bwana hana lolote la maana hasa baada ya waliokuwa wakimpa taarifa wakati wa JPM kuondolewa maeneo yao ya kazi.

Alipokosa ajenda ndio akajifanya kuipenda sana chadema ili abaki kuwa relevant kwenye mitandao. Leo baada ya Mbowe kuwekwa kizuizini anawatukana sana chadema kuwa wamekaa kimya hawafanyi lolote kuhusu mbowe. Hivi alitaka wafanyaje labda katika mazingira tulionayo.

Hili liwe funzo kwa wanasiasa kushabikia hustlers wa mitandao kama kigogo asiyekuwa na ajenda na anayetaka kuwa juu ya kichwa cha kila mtu. Amewatukana sana akina zito, lipumba na mbatia mkakaa kimya. Leo anawatukana chadema wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…