Chanjo inaposubiriwa huku Uhasama Ukitamalaki

Chanjo inaposubiriwa huku Uhasama Ukitamalaki

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,062
Ni wazi kuwa kwa makamanda wengi suala la chanjo ni muhimu lililokuja likiwa limechelewa mno.

Inafahamika kuwa Chanjo hii imetufikia kutokea kwa tulioaminishwa kuwa ndiyo walio wachawi wetu wakuu yaani mabeberu.

Ni barakoa, PPEs, sanitizers nk? Vyote vikinasibishwa na upigaji wa mchawi beberu huyo dhidi yetu.

IMG_20210729_192941_480.jpg


Hata hivyo afueni hii imekuja kukiwa kumegubikwa na ndivyo sivyo za serikali zilizoanzia Mwanza. Mheshimiwa Mbowe yuko mikononi mwa wadaiwa wake kwa kinachoaminika ni kubambikiziwa kesi.

Ndivyo sivyo hii haina tija yoyote kwa serikali ya ya Samia Suluhu Hassan zaidi ya kuwa inapalilia nafasi kwa ajili ya mifarakano zaidi.

Inafahamika kuwa pana watu wamekufa ambao hawakupaswa kufa ila kutokana na uzembe na porojo zilizokuwapo kuhusiana na ugonjwa huu.

Ni wazi kuwa makamanda wamejipanga kusubiria chanjo wakiwa na mioyo inayovuja damu.

Upande ule kumejaa mamburula wasiotaka chanjo, huku makamanda wametuliza bolu wakidhihirisha chanjo yao tu. Makamanda wanashiriki vipi kwenye kampeni ipi?

Ni nani aliye mnufaika wa uhasama huu unaoendelea kumea?

Kwamba mchokozi hajulikani? Kwamba hajui nini matokeo ya mifarakano? Kwamba kadhamiria liwalo liwe?

Ndani ya siku 10 tutakuwa tumepata chanjo inshallah.

Yetu macho.
 
Anzisha thread inayohusu Corona, ukimaliza anzisha thread kuhusu Mbowe. Swala la Corona na vaccine lipo complicated sana. Kuna CCM kibao walio upande wa Gwajima na serikali na CHADEMA kibao walio upande wa Gwajima na serikali.

Kuchanganya kukamatwa kwa Mbowe na ishu ya Covid unaonekana umevuta bangi iliyochanganwa na mavi ya NYUMBU. Rudia kusoma uliyoandika uone kama yanaleta maana hata kwa mashabiki wako.
 
Mliyojitolea kufanya majaribio ya chanjo mjitokeze msianze kujishauri.
itvtz~p~CR6YCCUHYO1~1.jpg
 
😂😂😂😂😂😂 khaaaaaa!!

IMG_20210729_204920_339.jpg


Si tulikubaliana kila mtu anao na m@vi yake?
 
Anzisha thread inayohusu Corona, ukimaliza anzisha thread kuhusu Mbowe. Swala la Corona na vaccine lipo complicated sana. Kuna CCM kibao walio upande wa Gwajima na serikali na CHADEMA kibao walio upande wa Gwajima na serikali. Kuchanganya kukamatwa kwa Mbowe na ishu ya Covid unaonekana umevuta bangi iliyochanganwa na mavi ya NYUMBU. Rudia kusoma uliyoandika uone kama yanaleta maana hata kwa mashabiki wako.
Naunga mkono
 
Sijawahi ona gaidi anademand katiba mpya ni bongo tu

Wanasema ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni. Haya ndiyo yaliyo ya Firauni mkuu.

Acha tuchanjwe kwanza.
 
Kun mzee huku katoa notice kwa watoto wake hakuna kuchanja wakichanjwa wasirudi watafute pakukaa, kasema hataki kuishi na misukule🐒
Kwani hizi chanjo ni kwa watoto? Au ni jitihada za kuonyesha mtu ni mburula kiasi gani tu.
 
Kwani hizi chanjo ni kwa watoto? Au ni jitihada za kuonyesha mtu ni mburula kiasi gani tu.
Kuna wazazi mpaka wanawafundisha watoto wao wakiona wahudumu wa Afya wamekuja wakimbie, hivi inamaana wanaamini kabisa serikali imeamua kuua watu wake tu ?
 
Acha kuusimanga Mmea mtakatifu wa tahajudi.

Naamini bwana Melo analishughulikia ombi letu. "Mamburula kama hilo wala hatupendi hata kujua kama kuna pua lilijaribu ku-poke 😂😂😂!"

Ukweli mchungu makamanda wako resigned. Hawana nia ya kumwunga Mama mkono tena.

Hilo alijue pasipo na shaka yoyote.

Akale alikopeleka mboga.

Jumbe Brown BAK Mshana Jr
 
Kuna wazazi mpaka wanawafundisha watoto wao wakiona wahudumu wa Afya wamekuja wakimbie, hivi inamaana wanaamini kabisa serikali imeamua kuua watu wake tu ?

Msingi wa mada uko wazi, kwa tulipo makamanda wanaathirika chanjo yao kibao vyao.

Kwao hili linaelekea mwisho:

IMG_20210720_094159_438.jpg


Aliyepalilia mifarakano hii ngoja tuone ana mipango gani.
 
Ukweli mchungu makamanda wako resigned. Hawana nia ya kumwunga Mama mkono tena
Mimi katika mtizamo wangu binafsi nadhani tulifanya haraka labda tungesubiri kwanza tuonane na Raisi Samia face to face ambayo aliahidi mwenyewe ndio tungemueleza kuhusu Katiba mpya na time frame ya mchakato ni mawazo yangu binafsi.
 
Mimi katika mtizamo wangu binafsi nadhani tulifanya haraka labda tungesubiri kwanza tuonane na Raisi Samia face to face ambayo aliahidi mwenyewe ndio tungemueleza kuhusu Katiba mpya na time frame ya mchakato ni mawazo yangu binafsi.

Hapana mkuu. Mzizi wa fitina ulikuwa hapa:

IMG_20210704_051559_619.jpg


Hata kama Chadema angejiita ACT au hata CCM au hata kama angeshauriwa milele viduku walikuwa wamedhamiria. Palikuwa hapana mkutano pale:

 
Ndio maana nimesema kuwa huo ni mtizamo wangu Binafsi.

Mkuu mawazo tofauti ndiyo mwendelezo wa kufikia kulikokomaa. Mwamba Mbowe ni mpambanaji. Aliko ninaamini hana majuto:

IMG_20210728_134628_357.jpg



Anasema hajasikia. Anahitaji sauti zaidi. Bila shaka hata za bawacha juzi ni sehemu ya sauti hizo.

Tutafika tu.
 
Mkuu mawazo tofauti ndiyo mwendelezo wa kufikia kulikokomaa. Mwamba Mbowe ni mpambanaji. Aliko ninaamini hana majuto:

View attachment 1873360


Anasema hajasikia. Anahitaji sauti zaidi. Bila shaka hata za bawacha juzi ni sehemu ya sauti hizo.

Tutafika tu.
Mabadiliko yoyote makubwa yanahitaji Sacrifice,Mwamba na Shujaa wetu Freeman Mbowe atatuvusha.
 
Back
Top Bottom