Kuna thwawabu kubwa kwa wote wasimamao kuipigania haki kwa ajili ya wote. Kwa maana njia hiyo si kila mtu anaweza kuipita.
Njia hii si lazima kwa kila mtu kuipita. Waipitao njia hii ni wale tu walio na wito kamili. Kama ile iendayo uzimani, ina vikwazo vingi.
Kipi ambacho kamanda Mbowe, Heche au yeyote aliyeichagua njia hii iliyotukuka ambacho hakukifahamu?
Kwamba ni awamu hii sasa ndiyo ambayo eti ingeacha kubambika kesi wakati ikijaribu kukomaa ili, hali ya fursa kwao iliyopo sasa isiendelee kubakia? Labda iwe ni kurukwa na akili kuwa na matumaini kama hayo!
Inajulikana wazi kuwa katika harakati hizi madhara (consequences) haziwezi kuepukika. Kutakuwa na watakao kamatwa, watakao bambikiziwa kesi, watakao potezwa, na hata watakaokufa vile vile kama kwenye awamu ile.
Ni gharama kama hizi ambazo kina Julius Nyerere, Nelson Mandela, Solomon Mahlangu, Chris Hani, Kwame Nkrumah, Kenneth Kaunda, na wenzao wa aina hiyo, walizijua na bado hazikuwafanya kughairi. Wapumzike kwa amani mashujaa wetu watukuka hawa wa Afrika.
Makamanda Mbowe, Heche na wote waliokamatwa, watakaokamatwa, watakaopetezwa, kufa na hata ambao hawatakamatwa kwenye harakati hizi, kama ilivyokuwa kwa akina Nyerere, wako tayari kuzilipa gharama hizo kwa ajili Tanzania iliyo bora zaidi ya kesho.
Hakipo kitakacho simamisha jitihada hizi ambazo ni kwa maslahi yetu sote kama taifa wakiwamo watoto wetu na hata watoto wa watoto wetu.
Wito kwenu nyie mnaobambikizia watu kesi hadi maaskofu na hata wazee wastaafu:
"La msingi zaidi ongezeni magereza. Ikibidi ili kuwapunguzia gharama, muwafahamishe tu wapi mngependa kukutana nao mkayafanye yawapendezayo. Kwa hakika watakuja wenyewe kwani wanacho kihitaji ni haki yao tu, iliyopo kwa mujibu wa katiba."
Itambulike kuwa kumedhamiriwa kwelikweli. Kama mnachagua shari dhidi ya maelewano, uchaguzi huo utakuwa ni wenu na utapokelewa kwa mikono miwili.